Hivi kesi ya Mbowe ni ya kitaifa au kimataifa?

Sawa kwani wasiwasi wako ni nin? si mmesema ushahidi upo tele wala hamja bambika mtu safari hii! kwanza kwa kuwa serikali inatuhumiwa na umma kubambika ingefaa for the public interest the case should be televised.
 
Mimi nadhani, nchi za nje watakuwa wanakuja kwa counterpart wao ili ajisikie wako wote kusudi aendeleze biashara za chanjo na aendelee kuwa mtii. Hivi Iran na China hawakuwa na wawakilishi?

Kuhusu Kesi ya Mbowe, itakuwa ni ya kimataifa kwa kuwa kama inavyoonekana ni muasisi na anaongoza Magaidi wa Kitanzania waliokuwa amboni, mkuranga, rufiji, kilwa na sasa wako Msumbiji.
 
Kwa hiyo magaidi waachwe tu bila kushughulikiwa kisa wawekezaji wasiache kuja?
 
Kwani wale masheikh wa uamsho nao si walipewa kesi ya ugaidi, hali ya uwekezaji ilikuaje?
 
Hivi kwa mfano Mbowe akifia mahabusu. Je Rais atatuma salamu za pole kwa familia ya “Gaidi”?
Sijui lini tutamgeukia Mungu na kuomba msamaha!
Nchi imekuwa ya kukomoa, kupakazia, uongo, ukatili, unyanyasaji na uzandiki, Ee Mola wetu tufanyie wepesi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…