Hivi kilimo bado ni uti wa mgongo wa Taifa?

Hivi kilimo bado ni uti wa mgongo wa Taifa?

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
57,761
Reaction score
216,011
1566446437625.jpeg

Kama Watanzania 75% wanategemea kilimo hivi tunategemea vijana waliozaliwa 2000 na kuendelea kutumia jembe la mkono katika kujipatia riziki?

Hizo ndiyo sababu zinazofanya vijana kukimbia kilimo na kukimbilia mijini au kutafuta ajira mbadala kama kuendesha boda boda. Ni mawazo yangu tu kama wale vijana walioteketea na moto Morogoro nusu yao wangekuwa mashamabani mbona tungeokoa nguvu kazi. Pamoja na kuwa kifowni mipango ya Mungu.

Badala ya vijana kukopeshwa bodaboda, simple farming machines pia zikitolewa kwa mkopo zitabadilisha mawaziri ya wengi kukimbilia mijini.

1566447152534.jpeg

Hii ni petrol cultivation tool.

1566447224335.jpeg

Wahusika tunaomba mliangalie hili.
 
Tatizo tunafanya kilimo kwa mazoea, Kuna wakulima wanafanya large scale lakini huwaambii kitu kuhusu kuacha jembe la mkono na hela ya kununua agro machines wanazo. Nimeona maonesho ya 8-8 sh mil 100 unapata planter, sprayer, harvester, majembe ya kulima matuta , kupalilia etc machines zote zina range 10-20m
 
Hii ndiyo mikopo ya kuwekeza kwenye vikoba vya vijana badala ya kuwakopesha bodaboda. Pia elimu ya ukulima bora, kwa mafanikio inabidi kuwekeza kwenye nguvu kazi ya vijana
 
Wa tz hatuwezi badilika kwa siku1 kikubwa nikutafuta taarifa sahihi kisha unazifanyia kazi ,na wasio amini watakuja kukuomba kazi ( ajira ) ndpo wataamini kua kilimo kinaweza kututoa ktk umaskini na kuwa na uchumi wa uhakika
 
ukisema kilimo kinalipa tusizungumzie madalali wa mazao au mfanya biaahara anaeleta kuuza mjini. tukisema kilimo hakilipi angalia upande wa watanzania wanaoishi kijijini ambao bila kwenda shamba watakufa njaa
 
Back
Top Bottom