Mtoa mada kukujibu,
kutwaa kombe la dunia si kigezo cha kuwa bora ila kuipa timu yako kombe la dunia ni kigezo cha kuwa bora miaka yote.
maradona, pele, zidane hawakuwa tu kwenye vikosi vilivyotwaa kombe la dunia bali wao wenyewe kwa kiasi kikubwa walibadilisha matokeo na kuzipa nchi zao makombe.
messi anajua chenga, anajua pasi za magoli, anajua kufunga na mambo mengi ya mpira, ila ikifika siku ya fainali ghafla anapotea, siku ambayo kila mtu anamuangalia yeye na wanategemea maajabu yake ndio siku anayopotea,
sasa kwa style hio unaniaminishaje ni mchezaji bora wa miaka yote? kwa kuwafunga alaves na granada?
hata huo mwaka ambao walifika fainali kombe la dunia messi hajafunga wala kutoa pasi ya goli kwenye hatua za mtoano, aliwaonea tu kwenye makundi.
wakati zidane anawavuruga vibaya sana brazili pale 1998 na kutwaa ubingwa, pele ndio kabisa kabeba mara 3 na akifunga magoli muhimu kila stage. maradona nae chenga zake zilikuwa ni siku muhimu alikuwa anahakikisha anafanya mambo makubwa pale timu inapo muhitaji.
Argentina wenyewe bado hawasemi messi ni bora kuliko maradona sembuse Dunia?