Hivi kumbe kuna watu ni wachoyo mpaka kwenye chakula. Haya maisha ni hatari

Kweli upumbavu Ni kipaji, yaani hakina dawa.
Kama babako kakufukuza unategemea Nini kwa baba wa mwenzio.
KAMIPIGIE BABAKO MAGOTI WE KIMA
 
Mkuu una degree ya marketing kutoka UDSM! maana huu uandishi ni kama wa mtoto wa chekechea...BTW ulichoandika hapa ni kama unafanya mzaha ndo maana wachangiaji wengi wanaponda, wanategemea miaka 38 uwe na uwezo wa kujiongeza kwa namna moja au nyingine pamoja na changamoto lukuki za maisha ikiwemo ukosefu wa ajira. Ni kituko kwa mtu wa umri wako kuja humu kulalamika kuhusu kunyimwa chakula kwao na rafiki yako.
 
Ni dalili za kukosa radhi ya wazazi. Popote uendapo na chochote ufanyacho. Laana itakuandama. Kwa ushauri tafuta wazee wa karibu ukamuombe radhi baba yako. Utakua umeepuka udhalishaji na mateso ya dunia.
 
We jamaa, utakuwa una matatizo kisaikolojia ? Aisee mkuu nyie kwenu wote hamna akili kuanzia babako mpaka wewe mnatakiwa mwende mkaombewe, unalilia kukaa kwa watu na una miaka 38 ? kaka ivi kweli unajielewa ?

Sikiza hii stori hapa ya mimi nilivyoonfoka home na kuna misosi mingi sana na kila kitu.

STORI
Baaada ya kumaliza chuo nikaona maisha yanakuwa magumu kula na kula kulala nalala ila sipati hela nnayotaka mimi , NILIKUWA NNA DESKTOP KALI SANA NLIOKUWA NIMEIPIGA LINUX NLINUNUA POSTA LAKI SABA NIKAUZA LAKI NNE NA NUSU, nikamuaga maza nikasepa niakenda kupanga gheto dogo nikaingia mtaani nikapambana kiume sometimez nakula kibish Mzee akakubali me mpambanaji akanibust hela kidogo nikafanya mambo yangu nikapata mchongo kwene mihangaiko yangu hiyo hiyo nikajisomesha na postgraduates saivi mambo yanaenda na sijawah kulia lia na sijawah kurudi home hata kama sina hata kumi ,

USHAURI

UMEKUWA MZINGO NYUMBANI KWA WATU KIMBIA, kama babako hakutaki ndugu baki watakutaka. Sasa shule uliosoma mbona ni hopeless ? Mkuu na hii stori nlokupa ikawe changamoto na ikubadili maisha yako kwa jina la yesu,
 
Unafurahisha ufanyayoooooooo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…