Hivi kumbe wanawake mnatuchukulia hivi! Da...

Ashangae nini...kwani hua hamjijui kama ni WAZURI au WABAYA??!Sidhani kama kuna mtu kipofu kiasi cha kutojijua yeye ni mtu wa aina gani!!

Sure?!
Check it again...
 
Sure?!
Check it again...

Niangalie wapi??!Nnaowajua wote naamini wanajitambua...hata wale ambao walikua hawajui baadhi nimesaidia kuwaonyesha.Achilia mbali kusikia kwenye redio...wao wanajulishwa uso kwa uso.Muulize mke wako we ni mtu wa aina gani...akiwa mkweli atakwambia hata yale ambayo ni negative kuhusu wewe.Sio mnasifiana tu bila kukosoana wakati makosa yapo!
 

Una hatari wewe!
Hivi akiniambia bwana we hunifikishagi pamoja na kujaribu mambinu yako yote hayo unategemea nini? Hii ndoa itaendelea kuwa ya furaha kama wakati huu anaponisifia kuwa mi ni kiboko, napagawisha?
Sio kila ukweli unajenga Lizzy, mwingine unabomoa...
 
Kwasababu hamuaminiki!!

Sio wote...baadhi yenu msio na mshipa wa aibu wala huruma.Hao wote waliojibu naamini wamejibu kutokana na experience...badilikeni mpendwe mpaka mchukie!

Umeona ee! Jamani wanaume badilikeni mkipendwa basi na nyie pendekeni!! Kuweni na huruma jamani watoto wa watu kila siku wanalia, hivi nyie mnajisikiaje?
 
Uuuufhh sijui niweke description gani ya hawa viumbe though cant get enough of them! Wengi wanapenda kulelewa nowday ' except my boy though huwezi jua ni mm nimepost hii' confidence ndogo yaani mfano mdada una kazi nzuri kwa wale walio serious wanataka meaningful relationship wanakimbia, marioo ndo wanakuja kwa kasi, wanapenda kuzaa hovyo nje bila ndoa, commitment kwao ni noop, zamani nilidhani wote c wa kuwaamini after dating dis naughty boy I believe c hawafanani kiivyoo kuna wa kutrust angalau 60%, wako obssessed na their look 'zamani I thought only ladies' yaani wanapenda miili kama ya akina Ali Kiba! lol wangeweza wangepaka powder kukava chunusi,
Zingine namalizia baadae ngoja niandike voucher hapa
 

Ukweli unajenga maana unampa mtu nafasi ya kujirekebisha!!Kwahiyo bora akukenyulie huku kila akiwa na wewe anamuwaza ex wake aliekua anamaliza kila kitu ili angalau asahau unavyompotezea muda wake kwakujifanya unajua kumbe unapapasa tu??!Msipende kusifiwa uongo....sifa za ukweli tu ndo zinaweza kukupa raha.
 
usijekuta hata mkeo alipiga simu na kushindilia msumari
 

Kila kitu na kila mtu ana maximum limit. Inawezekana yeye keshaona kuwa uwezo wa huyu mtu unaishia hapa hata afanyeje, na bado sifiki... (pengine hata mimi nimeliona hilo au hata huyo wako ameliona hilo), lakini anajua kabisa kuwa ndoa sio that easy reversible, kuwa kwa sababu hiyo aniache akatafute mwingine. Na tena kwa busara zake anajua kuwa mapenzi yanaendeshwa zaidi na saikolojia, na siku akitamka kuwa nampapasa tu, hiyo ndo atakuwa ameiweka rehani...

Hapa namaanisha kuwa hata wewe unatakiwa sometimes uone kuwa huyu ni mwenzangu (au mwenzetu), ngoja nimsitiri, na sio kila kitu umwage ukweli, hasa vile unavyojua kuwa haverikebishiki...
 
Kwanini visirekebishike??!Acha kujiendekeza...!
 
Umeona ee! Jamani wanaume badilikeni mkipendwa basi na nyie pendekeni!! Kuweni na huruma jamani watoto wa watu kila siku wanalia, hivi nyie mnajisikiaje?

Sawa dada yangu lakini usiombe nazi kwenye mtende... Usiombe wanaume wabadilike wawe zaidi ya wanaume. Vingine mnavyolalamikia kwa wanaume, vimeumbiwa kwenye uanaume wao, havibadiliki...
 
Kwanini visirekebishike??!Acha kujiendekeza...!

Sijiendekezi, but kasoro nyingine ni za kuumbiwa. Uliona wapi waridi isiyo na miiba?
 
Sawa dada yangu lakini usiombe nazi kwenye mtende... Usiombe wanaume wabadilike wawe zaidi ya wanaume. Vingine mnavyolalamikia kwa wanaume, vimeumbiwa kwenye uanaume wao, havibadiliki...

Ni maumbile gani hayo we unayoyasema? kutokuwa na huruma kwa wapenzi wenu? Ooh noo....!! by the way, thats not a defence, ebu fikiria kama nyie ndo mngekuwa mnatendwa na kulizwa kila siku mgefurahi tu nakuona ni maumbile yasiyobadilika?
 
Sijiendekezi, but kasoro nyingine ni za kuumbiwa. Uliona wapi waridi isiyo na miiba?

Kwahiyo ikiwa na miiba ndio????!Miiba ile inatoka na ndo maana yanashikika.Sipendi wala sifagilii watu wanaopenda kupokea/kutoa sifa tu hata kama kuna kosa.Niambie ukweli nijirekebishe badala ya kunichekea na kunisifia kinafiki huku moyoni unasema angejua.....!
 
Sipendi wala sifagilii watu wanaopenda kupokea/kutoa sifa tu hata kama kuna kosa.Niambie ukweli nijirekebishe badala ya kunichekea na kunisifia kinafiki huku moyoni unasema angejua.....!

Unapenda kuambiwa ukweli? Haya umeyataka mwenyewe sasa usilie. Wewe ka-Lizzy unatakiwa uache ujeuri. Uko kajeuri jeuri sana wewe. Kila kitu unataka ligi isiyo na kombe.

Halafu uache kubana pua. Umesikia? Haya hebu nenda jikoni ukapike cha jioni.
 
Sijiendekezi, but kasoro nyingine ni za kuumbiwa. Uliona wapi waridi isiyo na miiba?

Sasa mbona linashikika na miiba yake.... sembuse nyie kujirekebisha?!! Penye ukweli kubali usitetee tatizo bro!
 
Sasa mbona linashikika na miiba yake.... sembuse nyie kujirekebisha?!! Penye ukweli kubali usitetee tatizo bro!
Na wanaume jifunzeni kuwabeba na kasoro zao, kama unavyoshika waridi na miiba yake...

Mnatuhitaji kwa sababu sisi ni wanaume (sawa na sisi tunavyowahitaji kwa sababu mu wanawake), but ukimchukua mwanaume, unachukua package nzima, including madhaifu yake...
 

Ukieoa miiba sio waridi tena tena hiyo, inakuwa kitu ingine...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…