Lipo tatizo ndiyo.
Umekuta kasichana kajanja wachaa!
Kabla haujajieleza kakakupashua, huyo mkamwana wangu yupo vizuri[emoji3][emoji3][emoji3][emoji3]!
Ukweli ni kwamba, bila ya msukumo wa kimapenzi, na kumbukizi ya ngono uzembe, hauwezi hata siku1 kuanza kuhangaika kuunguza vocha kumpigia X wako.
Amekuwa ni ndugu yako umjulie hali?
Ujinga ujinga wa namna hiyo ndiyo huwa ni chanzo cha kufanya watu warudiane bila kujali waliachana kwa taathira kiasi gani mpaka walimwengu wanachwa vinywa wazi na kubakia tu kusema.." wapenzi wagombanapo..."!
Penzi lililofubaa lipo mfano wa uraibu wa sigara halifai kuchokozwa, likiguswa linaripuka na kuripuka!
Unaambiwa uraibu wa sigara unamtesa sana mtu anapoacha kuvuta.
Sasa kama ameshinda majaribu hayo, basi mtu huyo asije akajaribisha kuweka sigara mdomoni kamwe, akijaribu atarudi kwenye uraibu wake haraka sana, tofauti na mtu ambaye hajawahi kuvuta!
Na kwa suala la mapenzi ni hivyo, ukianza tu kumpigia simu, tayari hapo unakuwa umepata msukumo, hasa kwenu vijana, alfajiri "kitu" kinasoma hadi kinakuuma na hauna pa kushika, kwanini usimpigie simu kumbembeleza huyo x wako?
Nani anakuwa kakukataza?
Msichana mjanja kakutolea nje kakuweza kweli, mbona pole?
Lakini sasa usimkatie tamaa, kama umemmiss na unahisi kumpenda kisawa sawa, achana na hii misimu, mtokee live piga naye stori muweke mambo yenu sawa, umtangazie nia na umuoe kabisa kumkata ngebe zake!
Dah!