mugah di matheo
JF-Expert Member
- Jul 28, 2018
- 6,307
- 12,410
- Thread starter
- #21
Maelezo yanatosha kabisaKiukweli hata mimi binafsi napata shida sana na huyu Mwakalebela wa Yanga. Baada ya kupata taarifa kuwa Mwakalebela ni mojawapo wa viongozi wa juu kabisa wa Yanga nilifurahi sana nikijua sasa ataleta changamoto mpya katika soka la Tanzania kutokana na historia yake ya kufanya kazi TFF na mtu mweledi sana Leodgar Tenga.
Nilianza kupoteza imani naye kama kiongozi mweledi pale alipoaanza kushabikia vitu vidogo kama nembo ya mdhamini na kipensi cha Zahera wakati ambapo Yanga ilikuwa inapita kipindi kigumu cha ukosefu wa fedha za kuendesha timu. Yeye kama kiongozi nilitegemea apambane na mambo makubwa ya namna ya kupata fedha za uendeshaji wa timu kwa wakati ule ambapo Yanga ilikuwa haina mdhamini.
Kwa vyovyote iwavyo Mwakalebela huyu wa sasa ndio "original" yule wa TFF ni feki na inaonekana bosi wake Leonard Tenga alikuwa anamfichia madhaifu yake mengi ya kiuongozi ambayo tunayaona leo.
Hamna cha kuongezea