Hivi kuna limit ya kiasi ambacho Serikali inaweza kukopa kwa mwaka?

Hivi kuna limit ya kiasi ambacho Serikali inaweza kukopa kwa mwaka?

Red Giant

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2012
Posts
15,657
Reaction score
20,967
Kawaida serikali hasa za kidemokrasia zinapenda sana kukopa. Wanakopa na kutumia watakavyo wakijua watakaolipa madeni ni wengine kabisa. Huu ni mfumo mbaya sana kama hakuna udhibiti.

Sasa kwa nchi yetu, je, kuna limit ya kiasi cha pesa ambacho serikali inaruhusiwa kukopa? Au kuna limit kwa awamu ya urais juu ya kiasi inachoweza kukopa?
 
Kama una mali nyingi ya asilia kama mafuta, madini, bandari, gesi n.k hakuna limit. Ila madhara yake ni makubwa huko mbeleni, kama Zambia, Mombasa, na kwingineko walivyokaribia kuziuza nchi zao kwa kushindwa kulipa madeni.

Ni hivi, kama una gofu kariako, tajiri anaweza kukukopesha kila mwezi milioni 5 na ukaweka dhamana gofu lako. Mwsho wa mwaka nitapoanza kudai madeni yangu na ukashindwa kulipa nitaitaifisha gofu lako la zaidi ya milioni 400 kwa kiwango cha chini ya milioni 100. Hapo ndio akili ya uchumi ilipo.

Akili kichwani!
 
Mabepari hawapendi limit ya aina hiyo, itawafunga mikono kula rasilimali za nchi.
Kawaida serikali hasa za kidemokrasia zinapenda sana kukopa. Wanakopa na kutumia watakavyo wakijua watakaolipa madeni ni wengine kabisa. Huu ni mfumo mbaya sana kama hakuna udhibiti. Sasa kwa nchi yetu, je, kuna limit ya kiasi cha pesa ambacho serikali inaruhusiwa kukopa? Au kuna limit kwa awamu ya urais juu ya kiasi inachoweza kukopa?
 
Kwa nchi kama USA kuna ukomo WA serikali kukopa(debt ceiling), juzi Kati biden alitaka kukopa kupita kiwango cha ukomo ila congress kukawa kuna upinzani. Ni mpaka congress waidhinishe.
 
Kama una mali nyingi ya asilia kama mafuta, madini, bandari, gesi n.k hakuna limit. Ila madhara yake ni makubwa huko mbeleni, kama Zambia, Mombasa, na kwingineko walivyokaribia kuziuza nchi zao kwa kushindwa kulipa madeni...
Na vipi sisi wakopaji, kuna sheria ya nchi inayolimit kiasi ambacho serikali inaweza kukopa kwa muda fulani?
 
Kwa nchi kama USA kuna ukomo WA serikali kukopa(debt ceiling), juzi Kati biden alitaka kukopa kupita kiwango cha ukomo ila congress kukawa kuna upinzani. Ni mpaka congress waidhinishe.
Kitu kama hiki. Nchi yetu inakitu kama hiki?
 
Back
Top Bottom