Hivi kuna mahusiano gani ya moto na hili balloon?

Ndugu Zangu Wasambaa Wanasema Hivi
"Wazungu Ni Wahambanyi Sana Waigaa Moto Mwe Kibuu "
Wazungu Watundu Sana Wamebeba Moto Kwenye Kibuyu
 
Mambo ya fizikia hayo mzee baba

Naona kuna mwamba kakupa jibu katika njia nyepesi.
 
Pitia hapa kama lugha inapanda!
Your browser is not able to display this video.
 
Jamaa anasema umuelezee kiswahili hayo haelewi

Sent from my LM-Q730 using JamiiForums mobile app
 
Umelewa, kwa iyo puto linapaa na jiko lile??
Jiko limefungwa kwenye uwazi wa chini ya puto juu ya tenga la abiria, jiko hili uwakaji wake unafanana na ule wa jiko la wanaochomea rejeta za magari.
Ninakuelewesha jinsi linavyofanya kazi wewe unanidharau kwa kuniita mlevi! Kisa, haupo mbele yangu!
 
Ukipasha hewa moto,inatanuka,ila uzito wake upo pale pale,sasa uwiano wake wa uzito na ujazo unakuwa mdogo maana ujazo/volume imeongezeka kutokana na kupashwa moto,wakati hewa ya nje,uwiano wake wa uzito na ujazo,unaendelea kuwa Sawa,(density),hapo Hilo puto litaanza kusukumwa juu,Kani/force ya kulisukuma juu itaongezeka kadri density yake(uwiano wa uzito na ujazo unavyopungua.litapaa mpaka pale uzito wake na Kani,nguvu ya hewa ya nje unalolisukuma utakapo kuwa Sawa,floatation law,ni kanuni hiyo hiyo,inayotumika,shilingi inazama baharini lakini,meli inaelea kwenye maji
 
Hapa nimegundua kuwa kunbe masimo ya sayansi yanaweza kufundishwa kwa lugha ya kiswahili kwani maneno mbadala wa maneno ya kiingereza kwa vitu vingi katika kiswahili yapo mengi, mfano;

Force = kani, Volume = ujazo, Mass= ujazo nene, Density = uzito nene, Temperature= jotoridi, Pressure=kani eneo nk.
 

Wazungu si wajanja ili tusiwe na uelewa wa haraka?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…