Hivi kuna maisha baada ya kifo?

BU LA BIBLIA: “Walio hai wanajua kwamba watakufa; lakini wafu, hawajui lolote kamwe, wala hawana malipo tena, kwa maana kumbukumbu lao limesahauliwa. Yote ambayo mkono wako unapata kufanya, yafanye kwa nguvu zako zote, kwa maana hakuna kazi, wala utungaji wala ujuzi wala hekima katika Kaburi, mahali unapokwenda.” *—Mhubiri 9:5, 10.

Siku ya ufufuo au kiama utafufuliwa
ni kama tu ulikuwa umelala kidogo hata kama ni miaka elfu moja imepita
Na hapo mbivu na mbichi zitafahamika
 
Asa hujajibu swali unaleta tu maneno walioandika binadamu kama wewe tofauti Yao ni wayahudi wa kale bac....hujasema why nzi hajaumbwa mfano wa Mungu ..hujaprove hata Kama wewe umeumbwa isitoshe mfano wa Mungu...unaleta tu hekaya za kale
 
Paka ana roho? Roho yake ikifa inaenda wapi...
 
Wanafunzi wanakimbia🤣🤣mtu anaroho mbaya ..si terms tu hizo jamani... 🤣🤣Hebu tupe evidence za msingi kuhusu Simu kweli tuanze kubishana ndo maana Africa tutaendelea kuoza
 
Kitabu hakijashushwa kimetamkwa na muarabu mmoja wa kale aliyekuwa mjanja mjanja...Hana tofauti na tb Joshua
 
So wayahudi tu ndo Wana vitabu vitakatifu..why usituletee vya wahindi, wachina, waarabu, wagiriki na si tuone
 
Wanafunzi wanakimbia🤣🤣mtu anaroho mbaya ..si terms tu hizo jamani... 🤣🤣Hebu tupe evidence za msingi kuhusu Simu kweli tuanze kubishana ndo maana Africa tutaendelea kuoza
Mkuu; Unasema wanafunzi kukimbia ni terms tu? Kwanini wasitumie terms nyingine? Inamaana hakuna ka-ukweli fulani hapo?
Kuhusu simu nilitumia kama utani lakini ni kukuonesha tu kwamba sio lazima kila kitu uone ndo uamini. Simu yako ikidukuliwa, unaweza kuongea na mtu ambaye sio mlengwa wako. Hilo hulijui?
Hivi na wewe unaona kweli Africa tutaendelea kuoza? Mbona umetumia neno zito hivyo kana kwamba ww sio Mwafrica? Waafrica tunayo mengi ya kujivunia japokuwa ukitulinganisha na wenzetu tunaonekana bado hatujawafikia - Tunakaza mwendo broo.
 
Paka ana roho? Roho yake ikifa inaenda wapi...
Mkuu, mbona nilisema roho huwa haifi? Kama unaamini paka ana Roho hilo ni ww unaamini hivyo. Mimi siamini hivyo. Labda unieleweshe/uniaminishe vinginevyo.
Ni hayo tu.
 
Asa hujajibu swali unaleta tu maneno walioandika binadamu kama wewe tofauti Yao ni wayahudi wa kale bac....hujasema why nzi hajaumbwa mfano wa Mungu ..hujaprove hata Kama wewe umeumbwa isitoshe mfano wa Mungu...unaleta tu hekaya za kale
Labda tukubaliane kutokukubaliana kuhusu uwepo wa roho.
Tukirudi kwenye maswali yako ya msingi kwamba eti 1. Nzi na Plasmodium wana Roho? Jibu langu ni Hapana. Wewe unasemaje hapo?
2. Wanaishi vipi bila roho?
Chagua: Nikujibu kisayansi au Kiimani au vyote kwa pamoja?. Lakini uzingatie kama tumekubaliana kutokukubaliana kuwepo kwa roho.
Karibu mkuu tujadili.
 
Uoneshe hiyo roho uli iona wapi na kujua ipo.

Vinginevyo roho hiyo ni dhana ya kufikirika tu haipo katika uhalisia.
Quote1. "Uoneshe hiyo roho uli iona wapi na kujua ipo."
Hakuna mahali (Place/Space)ila najua ipo kutokana na matokeo ya matendo au Utendaji wake.
Quote 2. "Vinginevyo roho hiyo ni dhana ya kufikirika tu haipo katika uhalisia". Jibu: Sawa kabisa
Sasa wewe Je, unaweza kuthibitisha hilo?
NB: Katika hoja kama hizi ni lazima kuwe na kigezo/vigezo vya kusimamia(Terms of reference) 1. Kama hoja inajadiliwa kwa mtizamo wa Kiimani au Kisayansi.
2. Wahusika katika mjadala wanalenga hatima gani (Target). Kama ni kubishana tu for the sake of Kubishana au ni Kushirikishana mang'amuzi (Experiance)
Kwamba ni Dhana (Hypothesis) ni lazima kuwepo na proof evidence ili ku-Nullify hiyo hiyo dhana kwamba kinachoaminiwa sio cha kweli, na hakipo. Basi tukuombe sasa ww utuwekee hiyo proof hapa kwa sababu mm naamini kichwa-kichwa tu.
 
Kwanini usiishi Sasa ndugu!? Kwan usubiri mpaka ufe!?.…Maisha ndio Haya, HAKUNA MAISHA BAADA YA KIFO!
Tena akae kwa kujua kuna watu washazikwa mamilioni ya miaka huko hata huenda tunapoishi na kujenga nyumba zetu miaka hii ni maeneo ya makaburi ya hao watu ila hatujui..
 
Kisicho kuwepo Hakihitaji uthibitisho wa kutokuwepo kwake kwa vile hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika.

Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika au kuhisika.

Sasa roho haipo kwa namna yoyote ile zaidi ya mawazo ya kufikirika tu.

Haionekani, Haishikiki, Haihisiki wala haisikiki
 
Nukuu 1. " Kisicho kuwepo Hakihitaji uthibitisho wa kutokuwepo kwake kwa vile hakipo kwa namna yoyote ile ya kuthibitishika".
Mhhhh! Sio kweli mkuu. Mbona mahakamani inathibitishwa kwamba Kosa linalodaiwa kutendwa na Mtuhumiwa halikutendeka? Wewe unashindwaje kututhibitishia hilo?
Nukuu 2. "Angalau kitu kinaweza kuwepo kwa namna mojawapo ya kuonekana, kushikika, kusikika au kuhisika".
Duh! Hapana sio kweli mkuu. Mbona hatujaweza kuona mawazo, kuyashika, kuyasikia au kuyahisi? Ila tunajua yapo na yanatumiwa na watu ili kupambana na changamoto za maisha (Usiniambie habari za sonona/msongo wa mawazo)
 
Mahakamani wanajua jambo fulani limetendeka kwamba lipo ndio maana wanahitaji uthibitisho.

Kama hamna jambo lolote lililotendeka ni kwamba halipo na haina haja ya kwenda mahakamani kutaka uthibitisho.
Mawazo yapo kwa kuhisika, sio kwamba hayapo.

Roho haipo kwa namna yoyote ile.
 
Hapana, hii research ilifanywa na nani? Kwamba mtu akifa roho inatengana na mwili?
 
Acha utani watu wapo kwenye majadiliano.
Tabia ni nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…