Wewe binafsi unakubaliana na hayo majibu ya Quran? Na kama ndio unakubaliana nayo basi kwanini isiseme roho ipo wapi ila inasema roho inatolewa? Yaani kabla haijatolewa mda huo inakuwa katika sehemu gani ya mwili?
Grace, wacha nieleze kidogo kuhusu maneno ya Allah kuhusu Roho; Kwanza mimi nayakubali majibu ya Quran kwa asilimia zote. Sina wasi wasi hata kidogo na kuamini Qurani.
Pili, sasa wacha nieleze kuhusu Roho. Roho ni siri ya Allaah (‘Azza wa Jalla), hakuna ajuaye siri hiyo hata Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) hakujulishwa. Anasema Allaah (Subhaanau wa Ta’aalaa) katika Quran tukufu:
Na wanakuuliza kuhusu roho. Sema: “Roho ni katika amri ya Rabb wangu. Na hamkupewa ujuzi isipokuwa kidogo tu.” [Al-Israa: 85]
Kwa hiyo hakuna yeyote yule awezaye kuumba roho hata ya kidudu, na Allaah (‘Azza wa Jalla) Ametoa changamoto kwa wanaoabudu na wanaoabudiwa pasi Naye kwamba hawataweza kamwe kuumba roho hata ya nzi kama Anavyosema;
Enyi watu! Imepigwa mfano basi isikilizeni kwa makini! Hakika wale mnaowaomba badala ya Allaah hawawezi kuumba nzi japo wakijumuika kwa hilo. Na nzi akiwapokonya kitu chochote kile hawawezi kukiambua tena. Amedhoofika mwenye kutaka matilabu na mwenye kutakiwa.
Grace, nakueleza kuwa, hali hiyo ya roho kuwa katika asili yake inaitwa asili ya maumbile, na imaanisha pia ni kuelemea katika Dini ya haki inayowapasa wana Aadam wote waifuate, na kwamba wajiepushe na upotofu kama Anavyosema Allaah (Subhaanahu wa Ta'aalaa):
Basi elekeza uso wako kwenye Dini yenye kujiengua na upotofu inayoelemea haki. Umbile la asili la kumpwekesha Allaah Aliyowaumbia watu. Hakuna mabadiliko katika uumbaji wa Allaah. Hivyo ndio Dini iliyonyooka sawasawa, lakini watu wengi hawajui. [Ar-Ruwm: 30]
Grace, namalizia kwa kukuelezea kuwa, kwa ufupi kwa mujibu wa Allah sisi wanaadamu tumepewa elimu ndogo ya Roho. Nakuhakikishia hutapata maelezo ya kina kuhusu Roho kwa mtu yeyote hapa duniani.