Hivi kuna mtu amewahi kukutana na bidhaa kwenye Ad na akaipenda ?

Hivi kuna mtu amewahi kukutana na bidhaa kwenye Ad na akaipenda ?

chai ya rangi

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2026
Posts
1,042
Reaction score
3,095
Unakuta kuna video umeitafuta unaiplay mara ghafla video ya matangazo inaibuka kama jipu alafu inakuhesabia muda ili uweze ku cancel, mimi binafsi hizi video huwa sizizingatii kabisa

Mara nyingi hata sijui zilikua zinaongelea nini, na kampuni hiyo inayojileta huwa moja kwa moja naiweka kwenye ignore list ya akilini.

Matangazo mengine ni ya kawaida lakini watangazaji wanatumia mentality kama wanaongea na mtoto mdogo. mfano kwenye kipindi kinachohusu mapishi atakwambia "hapa nimetumia maji ya kampuni X kupikia ndo maana chakula kinakua kitamu"

Yaani wanafanya kama wanaongea na watoto wa darasa la kwanza au la pili...

Kampuni bora kutangaza angalia kama koka au pepssi, wana deal na saikolojia yako hauwezi kusikia wanasema soda yao ni tamu.

Kampuni za kibongo nyingi zinatutangazia vitu vyao hadi unajihisi hapa natangaziwa na nadanganywa kwa kutuchukulia watazamaji kama wajinga au wenye akili ndogo ya kutangaziwa kitoto
 
mbaya zaidi unakuta bidhaa ulishainunua unaendelea kuoneshwa matangazo yake
 
Back
Top Bottom