Niambieni, kwa jinsi walivyosimama hapo na mwonekano wao,unadhani ni nani anayedhaniwa kuwa ndo anatakiwa asainishwe mikataba ya DP word?
Kati ya nchi ambazo watu wake ni jeuri, walisharidhika na umasikini wao, na mambo yao ni poa sana, na wenye uwezo wa kuuza chochote bila kufikiri ya badaye, na kwamba, kiwango gani watapata na ama hasara kiasi gani na wasijali kabisa, Ni Tanganyika! Ni watu ambao hawashughurishi kabisa bongo zao kuhusu vile Mungu amewekeza kwenye nchi yao, hawajui kabisa wafanye nini ili kitokee kile zaidi ya kuishia kubinafisisha!
Akili na mawazo yao, yapo kwenye kuwapa wengine waendeshe vitu vyao hata ikiwagharimu usalama wao, ni Tanganyika, Hii inamaa kuwa, nchi haina watalamu? Na ama walienda shule kukarili? Wasomi wetu hawawezi kuisaidia nchi?
Ni nchi ya watu ambao, mtu akiwacholea drafiti la uwongo na kweli la kibiashara, akajitahidi tu kuongea lugha ya Malikia, akahakikisha kuwa amewaaminisha faida kubwa kwenye mradi ule, kwamba watapata faida kubwa na hawatajuta, kiasi kwamba umasikini wa watu wao utakuwa ndo mwisho,, watapiga makofi na vigelegele na kuomba kusaini mkataba haraka bila hata ya kufanyia utafiti! Hii ni Tanganyika
Ni nchi ambayo watu wake hujitapa kuwa na CV kubwa halafu ukizileta kwenye utendaji wa kiufanisi, hauoni chochote!
Ni watu wabishi, wasiopenda kabisa kazi, waongeaji sana na wajuvi wa kupanga mipango, usimamizi sifuri! Ni watu wa kila kitu wataferi tu, Wasomi wa nchi hii wanaweza nini sasa, Kupiga kelele bila action??? Hovyo kabisa! Kwenye hili, Bado Magufuli anawaacha mbaali sana wasomi wetu!
Tumewahi kuaminishwa kuwa, mradi wa Gas ndio mwarobaini wa umasikini wetu na kwamba, tutauza umeme kwenye nchi zote zinazotuzunguka na itakuwa mwisho wa umasikini wa Watanzania,
Nazikumbuka sana hizo speech za Mh Mhongo kipindi hiko akiwa waziri wa Nishati na Madini
Tumebinafisisha mpaka bank sisi na ahadi ya kuuaga umasikini, lakini aaah wapi!
Tumebinafisisha Madini yooote yanayojulikana bado ambayo hayajulikani tu, kwa ahadi zilezile kuwa tunakwenda kuagana na utegemezi, lakini wapi, leo tunautegemezi mkubwa kuliko hata kabla ya kubinafisisha vitu vyetu
Kwani nchi yetu imepatwa na nini?
Sisi tuko sawa kweli??
Leo tena tunataka tuwape Bandari zetu waarabu wa DP word, hata kama ni hatari kwa usalama wa nchi yetu, ahadi ni zilezile kwamba, tunakwenda kuachana na utegemezi na watu wetu kuondokana na Umasikini!
Bado tu tunaendelea kuamini lugha hizi zilizoferi?
Kwani sisi tukiamua kuuwa bajeti ya wizara moja wapo ili tuwekeze kwenye hizi Bandari zetu, tukanunua vifaa ambavyo DP wanataka kuja nazo, hatutofanikiwa?