Hivi kuna ndege imeshatua Chato tangu baada ya mazishi?

"Hivi hapa wapi vile? Angekuwepo Siti karibu hapa angenitajia!" ananong'onezwa na kukumbushwa panaitwa Chato - anaitikia kwa nguvu "CHATOOO!"

Eti jamani hivi kuna ndege ambayo ishatua Uwanja wa Kimataifa wa Chato tangu baada ya msiba? Na kama ipo ilipeleka huduma gani?

Inasemakana pia hata wale twiga waliopelekwa kule Hifadhi ya Burigi na baadhi ya wanyama kama hao wengi wao wamekufa kutokana na kutoendena na ikolojia!
Twiga wa Burigi walikuwa wakipewa chai na maandazi, mlitaka waishije Sasa?
 
Usiku wa kuamkia leo ndege nyingi zilitua Chato, zikileta utitiri wa wageni kuja kutoa pole kwa wafiwa. Hii imepelekea kufikia hatua wananchi kujitokeza kwa wingi sana kuja kuunga mkono juhudi za marehemu kwa kuzishangaa.

Miongoni mwa ndege hizo ni Air Force ya USA, iliokia ikiendeshwa na Kepteni Mshana Jr ilimleta Makamu Wa Rais Kamala Harris kuja kumwakilisha Rais Wa Marekani na watu wake.

Kiwanja cha ndege chato kipo bussy sana kuliko hata cha KIA.View attachment 1742929
Hao wenye kaniki ndio wataalam wa makinikia, makenia au urubani?
 
Kama ningekuwa CEO wa ATCL kwa kwa kweli nisingekwenda viwanja vifuatavyo;
1. Chato
2. Mpanda/ Katavi
3. Songea
4. Iringa
5. Shinyanga

Ukisikia CAG anasema kwa mahesabu ya 2019/21, ATCL imepata loss ya Tsh 60 Bilion, ujue sababu ni kwenda kwenye viwanja vya peripheral.

FAST JET walioperate kwa faida kwa kwenda Mwanza, Kilimanjaro na Mbeya tu.

Hakuna haja ya kwenda kwenye mikoa kwa ajili ya kuwaridhisha wanasiasa. Huu siyo mwenge wa uhuru, bali ni biashara ambayo lazima izalishe faida
Huko kote abiria wapo wa kutosha tatizo bei zao sio realistic hata fast jet huko ulipotaja walikua wanaenda kwa gharama nafuu sana nakumbuka Dar mwanza ilikua 94k
 
Ni vyema hiyo hasara ikaangaliwa kwa upana zaidi kuliko ulipoishia kwa kuanzia aina ya ndege zilizopo na aina ya operations, maintenance, mikataba, na maeneo mengine. Kila kona ya Tanzania kuna Watanzania wanaohitaji usafiri wa ndege. Cha msingi ni kuzingatia aina ya ndege ya kupeleka na idadi ya route kwa wiki.
Kwani kabla ya ATCL kufufuliwa na Magufuli hao wa pembezoni walikuwa wanasafirije? Ilikuwapo FASTJET na Precision mahali ambapo ATCL haifiki.

Watu wanaopandia Chato walikuwa wanaopandia Mwanza kwa kupita kwenye kivuko
 
Huko kwote abiria wapo wa kutosha tatizo bei zao sio realistic hata fast jet huko ulipotaja walikua wanaenda kwa gharama nafuu sana nakumbuka Dar mwanza ilikua 94k
Kama ni kwa mtazamo huo basi hata Kazuramimba na Nangurukuru nako kuna abiria wengi.

Umetaja kuwa "Bei siyo realistic." Unapoongelea BEI una maanisha AFFORDABILITY. Kila mradi wa kiuchumi unaofanywa lazima uwe na feasibility study na business plan. Hapo ndipo kuna chapter ya Market au Affordability. Yaani ni nani watapanda na wana kipato gani?
FastJet aliweza kwenda Mwanza kwa Tsh 94,000 kwa sababu walikuwa hawana "overheads" za kwenda Katavi na Chato. Ina maana ndege yao ya Airbus ya abiria 120 ilikuwa inajaa kwa tiketi ya Tsh 94,000.

ATCL kwa kuwa wana cover overheads za Chato na Katavi ile Airbus inaruka na abiria 40 waliolipa Tsh 270,000

Kwa hiyo utagundua kuwa abiria wa Dar -Mwanza au Dar - Kilimanjaro, wanuziwa tiketi kwa bei ghali ili kuwalipia abiria wa Chato na Katavi.
 
Kwani kabla ya ATCL kufufuliwa na Magufuli hao wa pembezoni walikuwa wanasafirije? Ilikuwapo FASTJET na Precision mahali ambapo ATCL haifiki.

Watu wanaopandia Chato walikuwa wanaopandia Mwanza kwa kupita kwenye kivuko
Mimi nime jaribu kuangalia nchi nzima kwa upana wake sio Chato tu. Msingi wa post tangu ni kutoafiki kubana usafiri huo kwa mikoa michache kwa kufuata walichofanga Fast Jet kwa kwenda Mbeya, Kilimanjaro na Mwanza kwa mujibu wa mdau mmoja hapo juu.
 
Jibu ni Serikali iruhusu soko huria kwenye biashara. Namna walivyondolewa FAST JET ku- operate Tanzania matunda yake ndiyo haya.

Mimi naongea kwa perspective ya kibiashara
 
Air Tanzania wanaenda mara tatu kwa wiki boss.
 
Jibu ni Serikali iruhusu soko huria kwenye biashara. Namna walivyondolewa FAST JET ku- operate Tanzania matunda yake ndiyo haya.

Mimi naongea kwa perspective ya kibiashara
Nakuelewa lakini na wengi wanaongea hii issue wanasahau service perspective ya hiyo biashara kwa nchi. Ndio maana akina KQ kila mwaka hasara lakini hawafi.
 
Kwa KQ kwanza usijifananishe na ATCL hata kama wana pata hasara. Kwanza kuna tofauti katika umiliki. Majority shareholding ni Private. Pili mtandao wao uko embedded na Tourism
 
Sasa tofauti ni nini kwenye wao kuendelea kuwepo? Kwanini bado wanaendelea?
 
"Hivi hapa wapi vile? Angekuwepo Siti karibu hapa angenitajia!" ananong'onezwa na kukumbushwa panaitwa Chato - anaitikia kwa nguvu "CHATOOO!"

Eti jamani hivi kuna ndege ambayo ishatua Uwanja wa Kimataifa wa Chato tangu baada ya msiba? Na kama ipo ilipeleka huduma gani?

Inasemakana pia hata wale twiga waliopelekwa kule Hifadhi ya Burigi na baadhi ya wanyama kama hao wengi wao wamekufa kutokana na kutoendena na ikolojia!
Mkuu achana na ushabiki hata huipendi CCM na Chato kwa ujumla kaa kimya.
Ndege si kutua tu bali zinafanya safari yake Chato to Dar kwa wiki mara mbili.
Karibu Chato mkuu
 
FB_IMG_16175432518436816.jpg

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom