Vita ya China na India 1962 (Sino-Indian border conflict)
Hii ilikua vita kati ya China na India iliyotokea mwaka 1962. Mgogoro wa kugombea mpaka wa Himalaya wenye urefu wa km 3225 ndiyo iliyokua sababu kubwa ya kutokea vita hii. Kabla ya hapo kulikua na vurugu nyingi mpakani hasa baada ya vuguvugu la kutaka kujitenga jimbo la Tibeti mwaka 1959 na India kumpa hifadhi kiongozi wa Tibeti Dalali Lama.
Mwanzo wa Vita
India ilianzisha mrengo wa kwenda mbele ambapo waliweka kambi Zaidi ya 60 sehemu mbalimbali za mpakani mfano magharibi mwa
McMahon Line (Hili ni eneo la mpakani kati ya India na jimbo la Tibeti,ambalo India wanalitambua kama mpaka rasmi ila China hawalitambui kwakua wanaona ni sehemu yao) na eneo la mashariki ya
Line of Actual Control
(Hili nalo ni eneo la mpakani lenye utata wa umiliki wake hadi leo upande ukiwa India na mwingine China,eneo hili lipo kwenye majimbo ya zamani ya Jammu na Kashmir). Kutokana na mrengo huu wa India ambao ulikua na lengo la kuwatoa hofu raia wake wasione kama wamevamiwa na majeshi ya China, majeshi ya China nayo yalilazimika kujizatiti ili yasizingirwe mnamo tarehe 20 oktoba 1962 majeshi ya China yalifanya mashambulizi eneo la Ladakh kwenda mbele Zaidi ya majeshi ya India yakiteka maeneo ya Rezang la na Tawang.
Kusitisha vita
China ilitangaza kusitisha vita tarehe 20 Novemba 1962 na kuanza kujiondoa eneo waliolichukua la
Line of Actual Control. Sehemu kubwa ya vita hii ilipigwana sehemu za milimani kwenye mazingira magumu ikihusisha mapigano ya ana kwa ana. Vita hii haikuhusisha majeshi ya anga wala majini.
Hizi ni sababu mojawapo za India kushindwa kwenye hii vita;
Uongozi mbovu kwenye medani za vita
Ripoti zinaonyesha kulikua na kutokuelewana kwa majenerali kwenye uwanja wa vita,mfano walimpuuza general Thorat aliposhauri juu ya mrengo wa kwenda mbele(forward policy) na movement za jeshi la China ila walimpuuza matokeo wakajikuta wamezungukwa na majeshi ya adui wakapokea kipigo cha haja.
Maandalizi na mipango mibovu
Kukosekana kwa mipango mathubuti na maandalizi mabovu,wao waliamini katika kusonga mbele wakajikuta wanaishiwa na supply hasa silaha. Hii iliwavunja moyo wanajeshi wengi wakajikuta wamezungukwa na kushambuliwa na adui kutoka pande zote.
Kutohusishwa mapambano ya anga
Vita hii haikuhusisha mapambano ya angani kwa kipindi hicho India Air Force(IAF) ilikua na nguvu kulinganisha na wapinzani wao(China) ila ilitumika kugawa chakula na madawa tu. Matokeo yangeweza kuwa tofauti kama IAF ingeshiriki.
Utegemezi kutoka USSR
India walitegemea msaada kwa kiasi kikubwa kutoka USSR kwa kipindi hicho mahusiano ya India na USSR yalikua makubwa. Kilichotokea msaada haukupatikana kama ilivyotarajiwa kwani USSR nao walikua kwenye maandalizi ya vita na USA kutokana na mzozo wa makombora ya Cuba (Cuban missile crisis). Ikumbukwe mzozo huu ulikua kati ya tarehe 16 hadi 28 Oktoba 1962 na China walianzisha mashambulio ya nguvu kwa India tarehe 20 Oktoba 1962 ni kama waliwafanyia
timing hivyo India wakajikuta wanapigana kivyao kilichowatokea hawatakisahau.
Uongozi dhaifu
Waziri mkuu wa India kwa kipindi hicho Jawaharlal Nehru analaumiwa moja kwa moja kwa India kushindwa kwenye vita hiyo.
- Mwaka 1954 China walitoa ramani iliyoonyesha eneo la Aksai Chin ni lao japo eneo hilo lilikua lipo India, lakini viongozi wa India walipuuzia mfano waziri mkuu Nehru aliliambia bunge kuwa eneo hilo ni kame lisilovumilika kuishi,kama nchi imepoteza kidogo sana kwa kuporwa eneo hilo. Hili lilikua kosa kubwa ambapo baadae liliigharimu India.
- Mwanzoni mwa mwaka 1961 waziri mkuu Nehru alimchagua luteni jenerali Brij Mohan Kaul kuwa mkuu wa majenerali wa jeshi la India. Kaul akaja na mrengo wa kwenda mbele (wengi waliupinga mrengo huu) akijenga kambi za kijeshi maeneo ya mpakani yenye mgogoro hadi kujikuta ameingia maeneo ya China hii ilitafsiliwa kama uvamizi wa India kwenye ardhi ya China hivyo kuanzisha vita ambayo ingeweza kuepukwa.
- Maamuzi mabaya ambayo hayakuungwa mkono na jeshi, mfano mrengo wa kwenda mbele haukukubalika na majenerali wengi pia kuna ripoti zilionyesha waziri mkuu Nehru alidang’anywa na CIA juu ya matumizi ya ndege za kivita (IAF) kwamba zingefanya hali ya mzozo kuwa mbaya Zaidi.
Matokeo ya vita
Majeshi ya China yalishinda vita hiyo na kulichukua eneo la
Aksai Chin na kulimilikisha rasmi. Kwa upande wa India watu 3,250 waliuliwa, 1047 walijeruhiwa,1696 walipotea na 3,968 walichukuliwa mateka. Upande wa China watu 722 waliuliwa na 1,679 walijeruhiwa. Baada ya vita hiyo ukaribu na hali ya kuaminiana baina ya mataifa hayo imepotea hadi leo.