Hivi kuna sababu zipi zilizopelekea kushindwa kwa India katika vita ya 1962

Hivi kuna sababu zipi zilizopelekea kushindwa kwa India katika vita ya 1962

Mkuu thesym ni India waliokua wanategemea msaada wa USSR ila hawakuupata sababu USSR mambo yalikua magumu kwenye mzozo wa makombora ya Cuba akawapotezea (India). Wahenga hawakukosea "mtegemea cha ndugu,hufa masikini"
 
Naona mada ya jamaa mmeichinjia mtoni
Approach aliyoitumia kuwakilisha mada yake haipo sawa mkuu!.. Alitakiwa atuletee fact anazoona zinamsumbua kuliko kuja kuuliza nini kilitokea like hajui kabisa!!..which seemz ain't true!. lakini @enlightment kaanza tackle the Q!.
 
Hbr za mida Wakuu,

Hivi kuna sababu zipi zilizopelekea kushindwa kwa India katika vita ya 1962.Kwa sababu ya Mpaka kati ya China na India, Japo mgogoro bado Upo chini chini, mwenye sababu anisaidie maana nimefuatilia migogoro ya mipaka mingi sana.

Soo huwa sielewi kwanini India alishindwa vita iyoo?!!

Karibuni wakuu tulidadafue hili jambo..View attachment 750050


HABARI,
"Dabby Jr
Moja ya sabau kubwa ni LOGISTICAL FAILURE Kama unakumbuka na ulifatilia kwa karibu habari za vita hii jeshi la India liliishiwa chakula hasa front line pia lilipungukiwa na kiasi kikubwa cha vifaa kwa hiyo jeshi likawa dhaifu sana.

LUMUMBA
 
FUTA UZI WAKO
afu rudia kuandika vizuri kabisa na kwa heshima kama mtu anaehitaji kweli Msaada kisha usubiri uone majibu yake utakayopata na hutojuta kuwa hapa jukwaani ni hayo tu chief
Asante sana Chief
 
Vita ya China na India 1962 (Sino-Indian border conflict)
Hii ilikua vita kati ya China na India iliyotokea mwaka 1962. Mgogoro wa kugombea mpaka wa Himalaya wenye urefu wa km 3225 ndiyo iliyokua sababu kubwa ya kutokea vita hii. Kabla ya hapo kulikua na vurugu nyingi mpakani hasa baada ya vuguvugu la kutaka kujitenga jimbo la Tibeti mwaka 1959 na India kumpa hifadhi kiongozi wa Tibeti Dalali Lama.

Mwanzo wa Vita
India ilianzisha mrengo wa kwenda mbele ambapo waliweka kambi Zaidi ya 60 sehemu mbalimbali za mpakani mfano magharibi mwa McMahon Line (Hili ni eneo la mpakani kati ya India na jimbo la Tibeti,ambalo India wanalitambua kama mpaka rasmi ila China hawalitambui kwakua wanaona ni sehemu yao) na eneo la mashariki ya Line of Actual Control
(Hili nalo ni eneo la mpakani lenye utata wa umiliki wake hadi leo upande ukiwa India na mwingine China,eneo hili lipo kwenye majimbo ya zamani ya Jammu na Kashmir). Kutokana na mrengo huu wa India ambao ulikua na lengo la kuwatoa hofu raia wake wasione kama wamevamiwa na majeshi ya China, majeshi ya China nayo yalilazimika kujizatiti ili yasizingirwe mnamo tarehe 20 oktoba 1962 majeshi ya China yalifanya mashambulizi eneo la Ladakh kwenda mbele Zaidi ya majeshi ya India yakiteka maeneo ya Rezang la na Tawang.

Kusitisha vita
China ilitangaza kusitisha vita tarehe 20 Novemba 1962 na kuanza kujiondoa eneo waliolichukua la Line of Actual Control. Sehemu kubwa ya vita hii ilipigwana sehemu za milimani kwenye mazingira magumu ikihusisha mapigano ya ana kwa ana. Vita hii haikuhusisha majeshi ya anga wala majini.

Hizi ni sababu mojawapo za India kushindwa kwenye hii vita;
Uongozi mbovu kwenye medani za vita
Ripoti zinaonyesha kulikua na kutokuelewana kwa majenerali kwenye uwanja wa vita,mfano walimpuuza general Thorat aliposhauri juu ya mrengo wa kwenda mbele(forward policy) na movement za jeshi la China ila walimpuuza matokeo wakajikuta wamezungukwa na majeshi ya adui wakapokea kipigo cha haja.

Maandalizi na mipango mibovu

Kukosekana kwa mipango mathubuti na maandalizi mabovu,wao waliamini katika kusonga mbele wakajikuta wanaishiwa na supply hasa silaha. Hii iliwavunja moyo wanajeshi wengi wakajikuta wamezungukwa na kushambuliwa na adui kutoka pande zote.

Kutohusishwa mapambano ya anga
Vita hii haikuhusisha mapambano ya angani kwa kipindi hicho India Air Force(IAF) ilikua na nguvu kulinganisha na wapinzani wao(China) ila ilitumika kugawa chakula na madawa tu. Matokeo yangeweza kuwa tofauti kama IAF ingeshiriki.

Utegemezi kutoka USSR
India walitegemea msaada kwa kiasi kikubwa kutoka USSR kwa kipindi hicho mahusiano ya India na USSR yalikua makubwa. Kilichotokea msaada haukupatikana kama ilivyotarajiwa kwani USSR nao walikua kwenye maandalizi ya vita na USA kutokana na mzozo wa makombora ya Cuba (Cuban missile crisis). Ikumbukwe mzozo huu ulikua kati ya tarehe 16 hadi 28 Oktoba 1962 na China walianzisha mashambulio ya nguvu kwa India tarehe 20 Oktoba 1962 ni kama waliwafanyia timing hivyo India wakajikuta wanapigana kivyao kilichowatokea hawatakisahau.

Uongozi dhaifu
Waziri mkuu wa India kwa kipindi hicho Jawaharlal Nehru analaumiwa moja kwa moja kwa India kushindwa kwenye vita hiyo.
  • Mwaka 1954 China walitoa ramani iliyoonyesha eneo la Aksai Chin ni lao japo eneo hilo lilikua lipo India, lakini viongozi wa India walipuuzia mfano waziri mkuu Nehru aliliambia bunge kuwa eneo hilo ni kame lisilovumilika kuishi,kama nchi imepoteza kidogo sana kwa kuporwa eneo hilo. Hili lilikua kosa kubwa ambapo baadae liliigharimu India.
  • Mwanzoni mwa mwaka 1961 waziri mkuu Nehru alimchagua luteni jenerali Brij Mohan Kaul kuwa mkuu wa majenerali wa jeshi la India. Kaul akaja na mrengo wa kwenda mbele (wengi waliupinga mrengo huu) akijenga kambi za kijeshi maeneo ya mpakani yenye mgogoro hadi kujikuta ameingia maeneo ya China hii ilitafsiliwa kama uvamizi wa India kwenye ardhi ya China hivyo kuanzisha vita ambayo ingeweza kuepukwa.
  • Maamuzi mabaya ambayo hayakuungwa mkono na jeshi, mfano mrengo wa kwenda mbele haukukubalika na majenerali wengi pia kuna ripoti zilionyesha waziri mkuu Nehru alidang’anywa na CIA juu ya matumizi ya ndege za kivita (IAF) kwamba zingefanya hali ya mzozo kuwa mbaya Zaidi.
Matokeo ya vita
Majeshi ya China yalishinda vita hiyo na kulichukua eneo la Aksai Chin na kulimilikisha rasmi. Kwa upande wa India watu 3,250 waliuliwa, 1047 walijeruhiwa,1696 walipotea na 3,968 walichukuliwa mateka. Upande wa China watu 722 waliuliwa na 1,679 walijeruhiwa. Baada ya vita hiyo ukaribu na hali ya kuaminiana baina ya mataifa hayo imepotea hadi leo.





Asante sana mkuu
 
Wewe nawe shule ulienda kusomea ujinga???
1. "San" ndio nini? Andika "sana".
2. "Ujue" ndio lugha ya wapi? Andika "unajua".
3. "Maan" ndio utumbo gani? Andika "maana".
4. "Kweny" = "kwenye".
5. "Ua" andika "huwa".
6. Unapoandika kiswahili usichanganye na lugha za nje.
PUNGUAN WAHEID WEWE.
Umemtosha mkuu
 
Pamoja mkuu ila majibu ya swali wadau wameshayatoa.
Walau kidogo,maana mkuu nilikuwa nafatilia mgogoro wa mpaka kati ya India na Pakistan kwenye jimbo la Kashmir, sasa ndipo mambo yakawa mambo,kuwa kumbe hata sasa India na China kuna mtafaruko wa chini kwa chini.

Asante sana mkuu
 
Yeah hizo lugha ziishie Chit-Chat kama hawezi huku aombe uhamisho uzi upelekwe chit chat watu wakatumie lugha waonavyo!..Tuheshimu na majukwaa!
hahaaa....huku kafuata nini !!? kuna haja ya mods kuliwekea access hili jukwaa
 
Back
Top Bottom