ndege JOHN
JF-Expert Member
- Aug 5, 2015
- 25,030
- 61,298
Hivi kuna nchi yoyote duniani ambayo ni rahisi kuwa maarufu kama Tanzania maana kwa uchunguzi wangu nadhani tanzania inaweza kuwa Top ya nchi ambazo wananchi wake wana feed taarifa nyingi sana kuhusu maisha binafsi ya watu maarufu.
Mtu hajaamka bado yupo kitandani alfajiri tayari anajua nani ameachana na nan, nani ameonekana beach na boat akila bata, nani amefuta picha Instagram, star gani ame comment kwa fulani na nani amem-unfollow nani.asubuhi tu mapema unapelekwa Mbezi Beach na masaki kuangalia maisha ya fulani. Baada ya hapo unarudishwa Sinza kusikia tetesi za mwingine. Kisha unaelekezwa na juma lokole kinondoni kuangalia gari jipya la msanii. Ukichoka kidogo unaambiwa kuna mtu amepost status yenye mafumbo ambayo taifa zima linaijadili.Mchana utasikia uncle T kachambana na fulani,mara maimartha kavujisha jambo,mara bahari beach huko dudubaya katukana mtu,jioni zamu ya ma comediani kuna penzi jipya la comedian,mara kuna connection ya binti wa kigamboni..
Cha kushangaza hizi taarifa zinapatikana kila sehemu. media karibu zote Instagram pages, TikTok, YouTube channels, influencers, wachambuzi.....Wakati mwingine najiuliza, hii ni ishara kwamba Watanzania tunaishi kwa amani kama familia kiasi kwamba hatuna mambo mengi ya kutusumbua? au ni upendo tu wa kweli kwa tasnia ya burudani ?
Kwa sababu hata ukisema ni ukosefu wa kazi nakataa..maana wapo watu kibao wenye kazi zao kabisa lakini bado wanajua ratiba nzima ya mastaa kuanzia asubuhi mpaka usiku.