Hivi kuna tofauti gani kati ya kufunga mchana na kufunga usiku?

Hivi kuna tofauti gani kati ya kufunga mchana na kufunga usiku?

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
38,920
Reaction score
44,970
Kwa kawaida watu woote duniani hufunga usiku kucha na hufungulia asubuhi kwa kufuturu na chai, chapati, mayai n.k.., pia kuna watu wengine wao hupendelea kufunga mchana kutwa na kufuturu usiku/jioni kwa mihogo, ndizi.., magimbi n.k..., hivi tofauti ya makundi haya mawili ni nini hasa..??!

========================
Chai huitwa breakFAST sababu unavunja mfungo (Kufuturu).
 
Kwa kawaida watu woote duniani hufunga usiku kucha na hufungulia asubuhi kwa kufuturu na chai, chapati, mayai n.k.., pia kuna watu wengine wao hupendelea kufunga mchana kutwa na kufuturu usiku/jioni kwa mihogo, ndizi.., magimbi n.k..., hivi tofauti yamakundi haya mawili ni nini hasa..??!

Khaa!!! Wewe vipi mbona tofauti ipo kwenye post yako!! Usituharibie saum zetu bana
 
Francis Nadhani kwako wewe kufunga umeelewa ni kuacha kula na kunywa tu.
funga ni zaidi ya uijuavyo ni wajibu(kama una nia ya dhati)ya kutaka kujua basi soma.
funga ni nini?
madhumuni yake?
kanuni na sharti?
kwanini tufunge?
nani inamuwajibikia kufunga?
faida zake ni zipi?
kwani tufunge mchana na si usiku?
je sisi ndio wa kwanza kufunya ibada ya funga?
Pindi ukipata majibu naomba urudi uanzishe thread utueleze kwa kadri ulivyoielewa.
 
Kuna vitu unachanganya,kuna kufunga na kubadili ratiba ya kula badala ya kula mchana unakula usiku kucha alafu mchana kutwa unakua umeshiba,hivyo vitu ni tofauti.
 
Kuacha kula si kufunga, unaposema kuwa hujala i=usiku ni kuwa umefunga hiyo si sawa, je ni mara ngapi unaweza amka usinywe chai wala chakulacha mchana mpaka jioni ndo ule, je hiyo unaweza kuita ni kufunga, je wanao fanya diet kutokula asubuhi na mchana mpaka jioni ndo wale nao pia tunaita wamefunga? HAPANA.

Kufunga ni ibada, lazima iwe imepangwa na pawe za sababu maalum (lengo). Ibada ya kufunga ni moja ya ibada zenye nguvu sana kiroho ( kiisilamu na kikrosto). kufunga ni kujinyenyekeza, kuudhiri mwili, kuutiisha mwili. its to play beyond flesh and blood.

Ibada za kufunga zina historia ndefu, hata kabla ya kuingia kwa imani za kikrsto na kiisilamu. Kwa sababu kufunga ni swala la kiibada, hata mababu etu walikuwa na mfumo wa kufunga katika imani zao za jadi. Pia kutoka kwa shuhuda mbali mbali za waabudu shetani, pia nao wanakuwa na ibada za kufunga.

Unaweza kuamua kuacha kula milo ya asubuhi na mchana kwa siku maalum katika mwezi lengo si ibada ila kwa lengo maalum la kiafya, wataalamu wa afya wanaweza kulizungumzia hili.
 
Back
Top Bottom