Hivi kuna ubalozi hata mmoja umeanza kujenga ofisi za ubalozi Dodoma?

unataka kibarua cha kubeba zege, kama huna kazi njoo area d nikupe kazi
 
Ok
Ila kuna mtu aliwahi kuuliza humu, nani anamiliki majengo ya ofisi za baloxi za nchi za nje, serikali au nchi husika?!
Wakihama haya majengo watafidiwa au watayauza kwa serikali?!
 
Muda waliopewa ukipita viwanja watapewa watu wengine wajenge halafu balozi ziwe wapangaji.
 

Kama kuna baadhi ya Vitu / Mambo ambayo nitamlaumu Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere japokuwa amelala Kaburini pale ' Mwitongo ' Butiama Mkoani Mara ( Musoma ) basi kimojawapo ni Kuamua au Kupendekeza Mji Mkuu wa Tanzania uwe ni Dodoma. Mpaka leo bado sijashawishika Kukubali kuwa Mji Mkuu wa Tanzania ni Dodoma. Kama ikiwezekana Watunga Sera waliangalie hili tena na ikiwezekana huko baadae Mji Mkuu uwe Mkoa wa Dar es Salaam kwani una karibia Sifa zote za kuwa hivyo lakini si kwa Mkoa wa Dodoma.
 
Ndo maana hujaona mtu akishobokea sana. Na pia Balozi nyingi zipo kwa ajili ya mashirika na taasisi za mabeberu.
Ubalozi wa China upo sana sana kwa ajili ya wafanyabiashara hivyo wao watapendelea kubaki Dar. Huko pengine watapeleka wawakirishi wa serikali zao au watakubali ingia gharama za kusafiri kila wakitaka onana na viongozi.
Fortress kama US Embassy haiwezi hama hivi hivi. Pale walipo ni safe haven wapo karibu na logistics zote
Na huu ndio ukweli mchungu.
 
Siku Magu akitoka madarakani,mrithi wake anaweza kuirudisha serikali Dar-es-Salaam na usishangae akaungwa mkono na watu wengi baadhi wakiwa ni wasaidizi wa karibu wa Magu leo hii.
 
Unajua sambamba na mambo menginre,sababu mojawapo ya hawa wazungu/mabeberu kutukumuunga mkono Magu huenda ni uamuzi wake wa kuhamishia serikali Dodoma.

Hili jambo nadhani hata wao hawalipendi ila hawawezi sema hadharanu na bila shaka wanatamani muda wake uishe aje mwingine arudishe serikali Dar.
 
Siku Magu akitoka madarakani,mrithi wake anaweza kuirudisha serikali Dar-es-Salaam na usishangae akaungwa mkono na watu wengi baadhi wakiwa ni wasaidizi wa karibu wa Magu leo hii.

Yaani hakuna Mkoa ambao umenikalia Kushoto na hata sishawishiki kwa haraka kwenda Kuutembelea kama wa Dodoma japo ni Mkoa ambao pia nina Ndugu zangu kadhaa tu huko wanafanya Kazi zao katika Sekta za Umma na zile za Binafsi.
 
Wanaweza kuendelea kukaa DSM kwa sababu usafiri wa anga na nchi kavu utaimarika sana muda si mrefu.....!!!( nawaza)
 
SGR itasababisha shughuli ziendelee kubakia Dar. Ndo maana balozi nyingi zimekaa kimya.
Pia security issues labda...
Ila ngoja tuone...
Japo naamini SGR itasababisha shughuli nyingi zibakie hapa
Wanaweza kuendelea kukaa DSM kwa sababu usafiri wa anga na nchi kavu utaimarika sana muda si mrefu.....!!!( nawaza)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…