Asante ila nisikusumbue nauliza hapahapa, samahani niliambiwa eti kujenga Ihumwa ni lazima uwe na building permit ambayo nasikia ni kazi sana kuipata, ni kweli mkuu? Namimi Nina plot huko next year nitaanza ujenzi, asante sana
Si mlisema december 2018 mtakua mmehamia Dodoma? Kwanini bado hamtaki kuacha mkoa wetu?Usiwe na haraka. Hata wizara za serikali bado hazikalamilisha ujenzi wa majengo yao pale mji wa serikali. Miundombinu hususani za lami bado pia hazijakamilika. Haya si masuala ya kukamilika ndani ya muda mfupi, tuwe na subira. Ni suala la muda tu balozi nyingi zitafungua makao yake makuu Dodoma. Kumbuka kwa sasa Dom hata international airport bado haina.
unataka kibarua cha kubeba zege, kama huna kazi njoo area d nikupe kazi
Hujui kituKwa ukimya huu,inawezekana hizi nchi haziko tayari kuhamia Dodoma ikiwemo hata kufungua ubalozi ndogo kama walivyofanya China na Ujerumani.
Uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma huenda ukasaidia kuifanya Dar ipumue kidogo walau maana imejaa almost!
Kila siku maingizo mapya yanaingia Dar imagine msongamano wa watu unaweza kuwa mkubwa zaidi kiasi gani?!
Vinginevyo Kuwe na mikakati mingine ya kukuza miji mingine ili kulifanya juju la Dar kupumua
Ni mtazamo tu
Mbona serikali ishahamia huko ila foleni haipungui
Dodoma haina mvuto,ilitakiwa tu kujenga mji mdogo wa shughuli za Bunge.
Hadi leo hawajui wanataka Didoma iwe nini?
Ila wakiweza kuweka miundo mbinu ya kisasa kuunganisha Dodoma na mikoa mingine barabara ,reli,na anga harafu wakaweza kutatua swala la maji,wakapanda miti yenye kivuli kwa wingi yenye uwezo wa kukinga vumbi.Labda baada ya miaka 20 kutokea sasa inaweza ikapata hadhi ya kuitwa mji mkuu.Lakini akija Raisi mwenye msimamo tofauti,Dodoma itabakia center ya shughuli za madini tu kama ilivyokuwa huko nyuma.