Hivi kuna ubalozi hata mmoja umeanza kujenga ofisi za ubalozi Dodoma?

Chezea Daslam wewe! "Mwenyewe" Dodoma hapajamnogea; itakuwa mabalozi! Tutabanana hapa hapa.

Sema anataka tumchukulie kuwa tayari ameshahamia rasmi eti kwa kutangaza tu kuwa amehamia wakati hakukaliki.
 
Dodoma haina mvuto,ilitakiwa tu kujenga mji mdogo wa shughuli za Bunge.
Hadi leo hawajui wanataka Didoma iwe nini?
Ila wakiweza kuweka miundo mbinu ya kisasa kuunganisha Dodoma na mikoa mingine barabara ,reli,na anga harafu wakaweza kutatua swala la maji,wakapanda miti yenye kivuli kwa wingi yenye uwezo wa kukinga vumbi.Labda baada ya miaka 20 kutokea sasa inaweza ikapata hadhi ya kuitwa mji mkuu.Lakini akija Raisi mwenye msimamo tofauti,Dodoma itabakia center ya shughuli za madini tu kama ilivyokuwa huko nyuma.
 
Wageni wengi hawataki kuhamia Dodoma ingawa serikali wanajitahidi wahamishie ofisi kuu ya Uhamiaji huko Dodoma na wizara ya mambo ya nje wote wahamie huko wapate kuwabana wageni vizuri.
 
Maduka ya vifaa vya ujenzi Dodoma yanafanya biashara sana kuna utitiri wa ujenzi wa nyumba mpya kila kona ya Dodoma sasa
 
Wengi wataweka ofisi ndogo za kibalozi
Rais akihama nao wataanza kuhamia na hasa uwanja wa ndege mpya ukikamilika na hudymu zote nuhimu zikiwa tayari. Huko Israel mabalozi wahamia Jerusalem sasa kutoka Tel Aviv kuifuata serikali.
 
Mbona Jiwe bado Yuko magogoni!!????
 
Kwa nyakati za sasa ni white elephant project na kupoteza kodi zetu na kusumbua familia za watumishi tu.Ilionekana Dodoma kipindi kile hakuna technology ya mawasiliano kipindi cha central govt mambo yote yalitakiwa kufanyika makao makuu mfano maombi ya uhamisho,ajira,afya,mafao,nk hoja hii ilikufa baada ya kupeleka madaraka mikoani shida zote zikimalizikia mikoani,Dodoma ilionekana ni katikati kwa maana ya usafiri wa ardhini hoja hio imekufa.Lengo pia lilikuwa ni kuwa mbali na uvamizi wa makaburu na wareno wasitushambulie Dodoma ilionekana ni salama hoja hio imekufa hakuna tena tishio hilo.
 
Ndo itakavokuwa ajae atarudi Dar then kodi zetu zitakuwa zimepotea bure
 
Uamuzi wa kuufanya Dodoma kuwa mji mkuu siamini kama ulikuwa sahihi:

1) Dodoma ni kama jangwa. Kiasili, Dodoma hauna mandhari nzuri kuanzia hali ya hewa mpaka uoto wa asili, n.k.

2) Dodoma ipo ndani kabisa ya rift valley, jambo linaloufanya kuwa mji wa hatari kuishi maana ni eneo ambalo lina uwezekano mkubwa siku moja kukumbwa na tetemeko la ardhi

3) Miji mingi mikubwa Duniani ni ile yenye shughuli nyingi za kiuchumi ambazo huchangiwa na uwingi wa watu, urahisi wa usafirishaji wa mali za viwandani na mali ghafi katika kuingiza na kutoa. Sifa hizo Dodoma haina.

4) Miji mikuu mingi Duniani ilipewa tu hadhi lakini ilikuwa tayari imejengeka. Haikujengwa ili iwe miji mikuu. Dodoma haikujengeka wakati inaamliwa kuwa mji mkuu. Matokeo yake ni serikali kulazimika kuujenga.

5) Mpangilio wa mji wa Dodoma kama mji mkuu ni ovyo sana. Dar es Salaam iliyopangwa na Wajerumani miaka ya 1800 ina mpangilio mzuri kuliko Dodoma iliyopangwa na waswahili wa miaka ya 1970! Wazungu wa miaka ya 1800 walikuwa na akili na uwezo wa kupanga miji kuliko wanaotajwa wataalam waswahili wa miaka ya 2000. Kati ya kada ambazo nadhani ni hovyo kabisa na isiyo na ufanisi ni Town planners. Hawa naamini ni Town Polluters. Dodoma haina barabara hata moja katikati ya mji ambayo ni pana.

Kwa Dar, walikopanga wataalam wa mipango miji wazalendo, wote mnajua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…