Hivi kuna ubalozi hata mmoja umeanza kujenga ofisi za ubalozi Dodoma?

Hizi nyumba zifikishwe na hiyo meli Dodoma port pale ndiyo zitawahi kuwasili kuliko kupitia Dar port.
 
Asante ila nisikusumbue nauliza hapahapa, samahani niliambiwa eti kujenga Ihumwa ni lazima uwe na building permit ambayo nasikia ni kazi sana kuipata, ni kweli mkuu? Namimi Nina plot huko next year nitaanza ujenzi, asante sana

Kwa mujibu wa taratibu Za miji yetu ujenzi unahitaji vibali,lakini Kwa Dodoma ni rahisi kuliko Dar lakini unaweza kuanza uku ukishughulikia kibali
 
Uamuzi wa Serikali kuhamia Dodoma huenda ukasaidia kuifanya Dar ipumue kidogo walau maana imejaa almost!
Kila siku maingizo mapya yanaingia Dar imagine msongamano wa watu unaweza kuwa mkubwa zaidi kiasi gani?!

Vinginevyo Kuwe na mikakati mingine ya kukuza miji mingine ili kulifanya juju la Dar kupumua

Ni mtazamo tu
 
Si mlisema december 2018 mtakua mmehamia Dodoma? Kwanini bado hamtaki kuacha mkoa wetu?
 
Kwa ukimya huu,inawezekana hizi nchi haziko tayari kuhamia Dodoma ikiwemo hata kufungua ubalozi ndogo kama walivyofanya China na Ujerumani.
Hujui kitu
Kama nchi ina ubalozi kamili,lazima ofisi iwepo kwenye .mji wa makao makuu ya serikali
Ni suala la muda tu,watajenga wengine hawakua na bajeti hiyo,na nchi zingine hazipo vizuri kifedha
 
Mbona serikali ishahamia huko ila foleni haipungui
 
Mbona serikali ishahamia huko ila foleni haipungui

Inaonekana kana kwamba haijapungua kwakuwa msongamano ulikuwa mkubwa sana kiasi kwamba hata badiliko dogo la serikali kuhamia Dodoma linakuwa halipelekei kule kupungua kwa foleni kuweza kuonekana moja kwa moja!

Nazani itakuwa imepungua lakini kwa kiasi kidogo sana !

Na mambo ya kuboresha ili kupunguza msongamano ni pamoja na kuboresha miundombinu kwa kuongeza ukubwa wa barabara mfano kutoka double road kwenda Tripple road , kuongeza barabara za pembezoni/mitaani kutengenezwa na kutumika, Halmashauri ya Jiji kuacha kutoa vibali vya ujenzi maeneo ya mijini na barabara kuu, miji ya mikoa mingine kuendelezwa kimkakati n.k
 
Twende Dodoma,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…