Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Joannah

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2020
Posts
20,921
Reaction score
49,014
Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
 
Wasalaam wanajamvi.
Jamani Kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa,hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha?nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa.nitazielezea kufupi

1.Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala,ilisheheni mbwembwe za kila aina ,nilikuwa na wadada


Ogopa kitu kinaitwa ULIMBUKENI.

NDIO Jibu la mada yako
 
Back
Top Bottom