Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Unazingatia dini sheikh Allah akulipe wengi hubadilika wanapohama mazingira wanayoishi na kuitelekeza dini .....ungejibanza nchi za kiarabu kule au Turkey.
 
Huko mbali mnakofika wapi? Kupata ajira ya 1/2m, kununua RAV4 ya miaka 15 iliopita na kujenga Goba huko? Kila siku humu watu wanalia maisha magumu Tz leo hii mmefika mbaaali!
 
Huko mbali mnakofika wapi? Kupata ajira ya 1/2m, kununua RAV4 ya miaka 15 iliopita na kujenga Goba huko? Kila siku humu watu wanalia maisha magumu Tz leo hii mmefika mbaaali!
Ohooo! kimeumana
 
Unatafuta maisha kwenye migongo ya wanaume siyo
 
Kuna wanaofanikiwa na wanaofeli,mimi katika kukutana na waenda ughaibuni nimekutana na wengi waliofanikiwa na wachache sana waliofeli.

1.kuna jamaa alikuwa muhasibu washington dc alienda US akiwa bado mtoto akasomea kule akapata kazi ya uhasibu alipotaka kuowa akarudi bongo akaowa akarudi na mke state ,baada ya miaka kadhaa wakaachana na mke wake haikupita muda mrefu jamaa alirudi bongo akiwa kama mbili kasoro yaani kama mnara unapotea na kurudi akawa anatembea na begi la mgongoni akaanza kuzurura bila mpango ,akawa mwalimu wa tuition ya english course mtaani huku akili yake ikiwa haijakaa sawa,mara apandwe na hasira bila sababu alichotuletea ni stori za Washington dc na Notebook ya namba za simu za wazungu kama utahitaji kwenda basi atakuelekeza pa kufikia ,wanadai jamaa alidungwa sindano ya kumdumaza asiweze kurudi tena US...hakuna alichowekeza zaidi alifikia kwa dada yake akawa analala sebuleni mpaka leo sijui yuko wapi mwamba yasir Mziba.

Wengi wao mitaani wameachia mijengo ya maana na kuwasaidia familia zao kutoka kudharaulika kwa umasikini na kuwa na maisha ya wastani kibongo bongo sio mbaya,kidogo uhakika wa kula upo,elimu,afya,wanasaidia..kuna jamaa wakaribu wapo South Africa,USA, CANADA,ARABUNI wamebadilisha maisha ya familia zao na jamii kwa ujumla...Wabongo Twendeni nje tukatafute maisha ila tuwe na malengo na nidhamu tukumbuke kuwekeza Nyumbani tulipotoka tukipata ahueni ya maisha huko ughaibuni tuwashike mkono ndugu zetu waliobaki na wabongo wenzetu walioko huko.
 
Huko mbali mnakofika wapi? Kupata ajira ya 1/2m, kununua RAV4 ya miaka 15 iliopita na kujenga Goba huko? Kila siku humu watu wanalia maisha magumu Tz leo hii mmefika mbaaali!
Au spacio na ist
 
Hata wazungu wakija kutalii Africa huwa wanawatambia wenzao pia,tatizo Watz wengi umaskini wa fikra na roho mbaya
Sawa,unadhani hata Kuna Vita basi,ilimradi wewe upo comfortable na kupoteza muda huko wewe endelea...maana wahenga wetu walisema asojua maana haambiwi maana
 
Kinachokuuma nini kama tunapoteza muda ulimlipia mtu nauli kwenda ulaya,hayo ndio madhara ya kutumia 0713 badala ya akilii
Si unaona akili yako inakokupeleka,hayo ndio mnayopitia huko,,uraibu,ushoga,kunyanyaswa na wenye nchi zao Sasa hata mkishauriwa mnaanza matusi...pole Sana Nakuelewa unapitia magumu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…