Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Nina washkaji zangu kama 11 hivi, Mmoja yuko JAPAN, Kyoto, Mmoja yuko UK, Brmingham, Mmoja yuko CANADA, Toronto, Mmoja yuko Denmark, Oslo, m1 yuko Namibia, Windhoek, Wa3 wako USA, Texas, California na Las Vegas Nevada, mwingine yuko zake South Africa, Cape town na mwingine anaishi TURKEY, Instanbul na wa Mwisho yuko Sehemu matata sana ARGENTINA, Iruya (Andes). Wote wana maisha mazuri tena sana wanasaidia sana ndugu zao. Ikumbukwe hawa wametokea maisha magumu tu, walikwenda huko kimasomo lkn wakabahatika kupata kazi.
Nilipata bahati ya kufika nchi 7 kati ya hizo, na niseme wazi anayeishi ARGENTINA yuko njema zaidi, yeye anafanya kazi kwenye hotel za hapo IRUYA, ana mke na watoto wa3 wazungu as You know Argentina haina wazawa weusi.

Wengi wanaotoka maisha safi kwenda nje kusoma wakirudi home wanakuwa tegemezi mifano iko mingi sana JUX ni mfano hai kabisa.

Wengi hawajitumi kwakuwa wanajua home kwao kuko njema.

Kuna jamaa tulikuwa nae Chuoni yeye Degree alichukulia Copenhagen Norway yaan hajielewi na sijui shida nini, na mwingine alitokaga kitambo ni kama bro kwangu alienda URUSI kusoma Udaktari ni mlevi sana, na ajabu anaijua dini (Muslim) ambapo aliwahi tuambia kuwa Russia kuna waislam wengi kuliko wakristo RC.

Kikubwa ni kujitambua tu. Mimi ni familia tu ila niliwahi kukaa Brazil miezi 6, nchi iko njema sana kazi nyingi nk sema changamoto ni kwamba mimi ni Muislam hivyo nililazimika kuhamia mji wa Rio de Janeiro ambako kidogo kuna misikiti angalua niweze kula chakula halali kwangu.

Vijana mupatapo fursa nje ya nchi ni muhimu sana kukumbuka shida za nyumbani na kujisevia kihela kidogo. Trick nzuri ni kutafuta demu wa kizungu afu unakuwa mwaminifu kwake maisha utayaona mtelezooooooo. Ref, MAD ICE yuko zake FINLAND, RAMA DEE Australia wanakula shushu kisa mbunye za kizungu.

Kuwa na maisha mabovu ni kujitakia.
Unazingatia dini sheikh Allah akulipe wengi hubadilika wanapohama mazingira wanayoishi na kuitelekeza dini .....ungejibanza nchi za kiarabu kule au Turkey.
 
Miaka ya Sasa sio miaka ya 1900s ambapo mtu akienda nje anaonekana Kama kawin Sana maisha,miaka ya Sasa Mambo yamebadilika Sana Dada watu wanaona kawaida Sana mtu kwenda huko,hii ni kutokana na baadhi yenu mnaorudi mkiwa hoi bila chochote na uraibu juu,wakati uliowaacha unawakuta wamefika mbali.Kama wewe umefanikiwa mshukuru Mungu Ila wengi wao Hali sio shwari,tunawaona tunaishi nao....Hakuna mtu wa kukuonea wivu eti kisa Ni Diaspora hakuna
Huko mbali mnakofika wapi? Kupata ajira ya 1/2m, kununua RAV4 ya miaka 15 iliopita na kujenga Goba huko? Kila siku humu watu wanalia maisha magumu Tz leo hii mmefika mbaaali!
 
Huko mbali mnakofika wapi? Kupata ajira ya 1/2m, kununua RAV4 ya miaka 15 iliopita na kujenga Goba huko? Kila siku humu watu wanalia maisha magumu Tz leo hii mmefika mbaaali!
Ohooo! kimeumana
 
Aisee tuko tofauti Sana,Kama Mambo yenyewe ndio hivyo nimekubali kweli Sina mapenzi ya dhati, siwezi kaa na mwanaume asiye na malengo Wala mwelekeo kisa penzi la dhati Hapana, NO!..Mimi binafsi naumiza kichwa mchana na usiku nalala masaa machache ili nitoboe maisha eti nikae nampenda mtoto wa mtu asiyeshughulisha kichwa chake...Hapana dada...Imani yangu yenyewe ya kiroho inamtaka mwanaume atafute kwa jasho mimi ni nani sasa nikae namvumilia mwanaume asiyetafuta.....we endelea na wapambanaji wanaozunguka duniani na kurudi na cheni na laptop ukiwaita mashujaa.
Unatafuta maisha kwenye migongo ya wanaume siyo
 
Kuna wanaofanikiwa na wanaofeli,mimi katika kukutana na waenda ughaibuni nimekutana na wengi waliofanikiwa na wachache sana waliofeli.

1.kuna jamaa alikuwa muhasibu washington dc alienda US akiwa bado mtoto akasomea kule akapata kazi ya uhasibu alipotaka kuowa akarudi bongo akaowa akarudi na mke state ,baada ya miaka kadhaa wakaachana na mke wake haikupita muda mrefu jamaa alirudi bongo akiwa kama mbili kasoro yaani kama mnara unapotea na kurudi akawa anatembea na begi la mgongoni akaanza kuzurura bila mpango ,akawa mwalimu wa tuition ya english course mtaani huku akili yake ikiwa haijakaa sawa,mara apandwe na hasira bila sababu alichotuletea ni stori za Washington dc na Notebook ya namba za simu za wazungu kama utahitaji kwenda basi atakuelekeza pa kufikia ,wanadai jamaa alidungwa sindano ya kumdumaza asiweze kurudi tena US...hakuna alichowekeza zaidi alifikia kwa dada yake akawa analala sebuleni mpaka leo sijui yuko wapi mwamba yasir Mziba.

Wengi wao mitaani wameachia mijengo ya maana na kuwasaidia familia zao kutoka kudharaulika kwa umasikini na kuwa na maisha ya wastani kibongo bongo sio mbaya,kidogo uhakika wa kula upo,elimu,afya,wanasaidia..kuna jamaa wakaribu wapo South Africa,USA, CANADA,ARABUNI wamebadilisha maisha ya familia zao na jamii kwa ujumla...Wabongo Twendeni nje tukatafute maisha ila tuwe na malengo na nidhamu tukumbuke kuwekeza Nyumbani tulipotoka tukipata ahueni ya maisha huko ughaibuni tuwashike mkono ndugu zetu waliobaki na wabongo wenzetu walioko huko.
 
Huko mbali mnakofika wapi? Kupata ajira ya 1/2m, kununua RAV4 ya miaka 15 iliopita na kujenga Goba huko? Kila siku humu watu wanalia maisha magumu Tz leo hii mmefika mbaaali!
Au spacio na ist
 
Hata wazungu wakija kutalii Africa huwa wanawatambia wenzao pia,tatizo Watz wengi umaskini wa fikra na roho mbaya
Sawa,unadhani hata Kuna Vita basi,ilimradi wewe upo comfortable na kupoteza muda huko wewe endelea...maana wahenga wetu walisema asojua maana haambiwi maana
 
Kinachokuuma nini kama tunapoteza muda ulimlipia mtu nauli kwenda ulaya,hayo ndio madhara ya kutumia 0713 badala ya akilii
Si unaona akili yako inakokupeleka,hayo ndio mnayopitia huko,,uraibu,ushoga,kunyanyaswa na wenye nchi zao Sasa hata mkishauriwa mnaanza matusi...pole Sana Nakuelewa unapitia magumu
 
Back
Top Bottom