Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Chief nakukumbusha kubet pia ni haramu.
 
Sasa mkuu we unadhani mtu mwenye maisha magumu Tz atakuwa na maisha mazuri akienda huko Ulaya Marekani etc?
Mtu anapigwa na maisha hapa Tz je huko? Si yatamua kabisa?

Your reasoning is illogical.

So mtu kama ni maskini kijijini akifika mjini lazima maisha yamchape pia? Ingekua hivyo watu wangeacha kufurika Dar kila siku.
 
Your reasoning is illogical.

So mtu kama ni maskini kijijini akifika mjini lazima maisha yamchape pia? Ingekua hivyo watu wangeacha kufurika Dar kila siku.
Huyu Wordsworth namkubali sana nimeshindwa kumjibu hapo.
 
Siyo wote wanaoenda Ughaibuni wanatoboa Maisha,wapo wanao toboa,na vilevile wapo wanaofeli! Ni Kama huku Nyumbani,siyo wote uliosoma nao wametoboa life!! Maisha ndivyo yalivyo,Muwombe Mungu akupe mwisho mwema!!
 
mtoto wa mwenye nyumba wangu karudi ana kama week 2 hapa, amekaa miaka 10 nje na yeye hivyo hivyo picha kibaoo alichorudi nacho ni rasta na kingereza tu bas zaidi kila siku ananipiga virungu.

Ni kweli ulaya shughuli ni nyingi na mtu kuingiza 500$ ni kawaida na wengi ukiwaambia hivi wakiwa bongo wanaipigia hesabu wanaona ni bonge la hela lakini kwa nje ni hela ndogo tu.

hivyo unakuta mtu anaingiza mathalani 10000$ per month lakini anataka kuishi maisha ya starehe na sawa kama wenyeji

hivyo kujikuta mwezi mzma hana anacho save na kujikuta anabakia na 100$ au zero kabisa,maana ulaya ugali nyama tu unaweza range mpka 50 -100$

hapo bado hujala milo mitatu,transport,gesi,kodi, nk maana kila kitu ni hela ndo maana kule kama ukioa kila mmoja kwenye ndoa anachangia 50/50
 
Sio kweli kwamba kila anaye kwenda ulaya hafanikiwi, inategemea ulienda kwa malengo gani.

Mfano mzuri ni mimi mwenyewe kabla sijaenda US nilikuwa nimeajiriwa Bongo kipato changu kilikuwa cha kawaida sana, mara baada ya kwenda huko na kukaa kwa muda usiozidi hata miaka minne maisha yangu niliyabadilisha kwa kiasi kikubwa… hivi tunavyoongea nimeweza kujenga nyumba mbili za kisasa na viwanja kadhaa mjini, nasomesha wadogo zangu shule za private nina usafiri mzuri ambao vijana wengi wa mjini wanautolea macho. Kitu nilichojifunza wengi wakifika nje hubweteka na kuiga maisha ya watu wa ulaya na kusahau walipotoka.
Kitu kingine wabongo wengi wanapokwenda nje huwa hawaendi kwa kufuata utaratibu wa nchi husika wao huwa wanajiripua mara baada ya kufika huko huwachukua muda mrefu kutafuta makaratasi ya kuwawezesha kuishi kihalali, kwa muda wote ambao wanafight kupata hayo makaratasi huishia kufanya kazi za kawaida ambazo kipato chake ni kidogo hivyo wanashindwa kufanya saving.
 
Tatizo kubwa ambalo nafaham lilimpata jamaa mtaani alienda majuu kufika kule badala ya kusoma akaanza kufanya kazi, hizi wanaita box, kapiga box wee lakini bills pia zipo juu, kwahiyo pesa anayopata inaishia kwenye bills, baada ya miaka kadhaa visa ikaisha akarudi.

Alirudi na computers na vifaa kadhaa akafungua biashara ya ki-stationery ambayo baada ya muda ikafeli.

Miaka na miaka bado anapambana kujitafuta kurudi katika mstari, waliobaki hapa walisoma chuo wakapata kazi/biashara wamemuacha mbali sana....

Kwahiyo tuseme wasio na kazi profesisonal huko majuu wanastruggle sana ila wenye kazi professional nadhani ndio wanatoboa.
 
Acha kufananisha mtu mwenye Rav 4 used , nyumba Goba na mtu aliyerudi na cheni,hereni ,phone na kutaka kufikia hukohuko Goba mnakodis....Ni mafuta na maji
Hahahaa! Wewe mwanamke umenifurahisha sana
 
Kwahiyo Joannah jamaa likiamka asubuhi linawasha redio na kuweka mizinga yake mezani. Linapiga Vodka moja linakuita linawasha kimoja linapumzika. Anapiga bia kadhaa anakuita tena anawasha cha pili mwendo ni huo hadi usiku.
Fedha zikiisha anapiga simu kwa mama yake hahaaa.
 
Waarabu wenyewe wanazimia Ulaya na NA. Ushawahi ona mtu anatoka nchi za ME au North Africa au Somalia anataka kwenda arabuni? Wanazikandia wakiwa kwao ila Wote wanataka Kuja kiwanja Mzee. Kiwanja is where it's at.
Nchi zenye amani Kama UAE,OMAN,QATAR kwa mtafutaji wa kazi naona Kama zinafaa au nakosea mkuu?
 
Inategemea na nchi…mchiz wangu alikaa UK akasema pale ni shidaaa ila alipo hamia norway akatoboa..ana mawe balaa
 
Kuwin maisha inategemea na akili ya mtu na malengo yake aliyojiwekea haijalishi yupo nchi gani,discipline,attitude na kumtegemea mwenyezi Mungu ndio kila kitu katika maisha,

Mleta mada anaposema "wengi" walioenda nje wamefeli ni anatumia hisia tu kufikia hiyo conclusion yake,au itakua ameamua tu kujifariji,hiyo reseach kaifanyia wapi na sample yake ilikua watu wangapi?

Kama mleta mada umetendwa na diaspora hilo ni tatizo lako pambana,kuponda diaspora hapa hakuwezi kuyabadili maisha yako,mind ur own business.
 
Nchi zenye amani Kama UAE,OMAN,QATAR kwa mtafutaji wa kazi naona Kama zinafaa au nakosea mkuu?

Huwezi linganisha uchumi wake na nchi kama USA au CA. Wengi wanaenda hizo nchi kufanya kazi za ndani na ujenzi kwa malipo madogo sana.

Watu wengi kwenye hizo nchi nao wanawish kwenda mbele kwenye fursa zaidi but it's a start kama uwezo wako unaishia hapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…