Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.

Naona umetolea mifano ya wakosaji tu hao walienda kupambana ni kama hapa bongo tu. Mbona mtu akitoka Mwanza akaenda kupambana Mpanda asitoboe hamgombi. Au katoka kwenu huko Kazulambita to Dar mjini kupambana akifail hammsemi.

Karibu whyskey hapa za madiaspora waliorudi na mi c class na kuporomosha mijengo huku ufukweni
 
Kwa inavyoonekana;
1. Ni Slay Queen mmoja aliye date na hao wabeba box wote watatu kwa nia ya kuitafuta fursa mwisho wa siku akaliwa bila kuambulia chochote.
2. Purposeless guys (a branch in bad boyhood ) in a strange way, they are attractive to women. Jobless men have enough time, energy and attention for sex and other adventures.
3. Kuna dhana ya kuwadharau watu/ vijana wanaoishi kwa kutegemea wazazi wao. Kimsingi siyo kosa wala dhambi kwa mtu yeyote wa umri wowote kuishi kwa kuwategemea wazazi wake iwapo wazazi wanao uwezo na upendo wa kumuhudumia. Hata kama una miaka 50 na wazee wako wana 80 na mawe ya kutosha, wewe kula bata achana na kelele za Vyura.

Kama kweli watu waliopo Nyumbani wanaishi vizuri na kuoana kama ulivyosema, kusingekuwepo na makundi ya Slay Queens wanaotembeza maqu kwa wabeba box na kupekuwa wallets zao kisha kutoa report.
 
Wengi walioko nje ya nchi hawanaga mbele wala nyuma, kijana wabongo anamzidi maendeleo Kuna mwingine namjua kakaa Uingereza more than 25 ila alirudi akiwa njaa Kali hana mbele wala nyuma, akarudi ndio kufungua duka la nguo tena akiishi kwa kutegemea Kodi ya nyumba iliyoachwa na wazazi wake, bahati nzuri akapata mwanamke ni Dr ndio kamuoa yeye yupo yupo tu, wengine nawafahamu wako Marekani na Wana maisha magumu mama Yao ni mstaafu ndio huwatumia hela za ku survive, in short wengi walipelekwaga nje na wazazi wasome ila Sasa ni mizigo wanategemea hao wazazi wao na wamepoteza focus za life

Mkimaliza mtupatie na wale wenye mafanikio sio kuwanywea biere tu na henessy wakirudi
 
Huyo wa kwanza na stori yako ya kudanga ni nani alie feli maisha kati yako na yeye? Hapo imeshadhihirisha wewe ndo umeshafeli maisha maana unadanga

Hao ndio wanategeaga diasporas na mikwanja yao wjibebishe wale happy weee zikiisha wasepe wadange mwingine. Wengine wanaingia kwny mahusiano hayo na hisabati za kujimimba kabisa wanatega mafanikio.
 
Hao ndugu zenu wanawakomboa sijakataa,wanawatumia Dollars sawa,hao Ni wachache katika kundi la wengi waliolowea huko...Huyo nduguyo ana mradi wowote hapa nyumbani?amejenga?ukute siku ya kurudi huku Ni mwendo wa kufikia apartment za jangwani sea breeze baada ya miezi sita kwa mama magomeni

Dah kwa comment zako naona unatafuta vya urithi wa mume by hooks and crooks.
 
We si kuna comment yako humu umewatetea hao wa south A ukasema bora hata hao kidogo wana nafuu[emoji848][emoji848]

Inaelekea mchizi ni mmendeaji sana wa diaspora na washamtumia sana na hivi wakirudigi wanakuaga fire moto na warm blooded down dipping.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Miaka ya Sasa sio miaka ya 1900s ambapo mtu akienda nje anaonekana Kama kawin Sana maisha,miaka ya Sasa Mambo yamebadilika Sana Dada watu wanaona kawaida Sana mtu kwenda huko,hii ni kutokana na baadhi yenu mnaorudi mkiwa hoi bila chochote na uraibu juu,wakati uliowaacha unawakuta wamefika mbali.Kama wewe umefanikiwa mshukuru Mungu Ila wengi wao Hali sio shwari,tunawaona tunaishi nao....Hakuna mtu wa kukuonea wivu eti kisa Ni Diaspora hakuna
Sasa Joannah kipi kimebadilika kutoka miaka hio ya 90 huko Europe na sasa watu hawa win tena wakienda?

Mimi naona uko peke yako unayeona ulaya ni pa kawaida, itisha hapo mkutano wa wanaotaka kwenda ulaya uone watakavyojaa maelfu!

Kisha usitudanganye watu wako better huko Tanzania, wakati familia nyingi hazipati milo mitatu and majority lives under 2 dollars per day...

Mwisho km wewe uko Dar usitufokee, jenga kwenu Chitoholi ,lol, ..sio wote wanokuja Dar,wanarudi vijijini wakiwa successful,the same as ulaya...kila mtu apambane na hali yake popote alipo!..lol
 
Wana mbwembwe Sana kila saa utasikia nilivyokua Texas,Mara nilivyokua Ibiza Bora mradi watu wajue alishaenda huko khaaa!
Inategemea na lengo lako la kwenda nje. Kama ulienda kupiga picha basi utarudi na albam ya picha. Ila kama wewe ni fighter ukikaa nje miaka kumi tu ukiwa serious unatoboa vibaya sana
 
wengi walioko marekani naowafahamu wamefika mbali Sana kimaisha huku dar wanamajengo mengi tu ya maana Ila Kuna baadhi pia naowafahamu walikuwa uingereza huwezi kuamini maisha yao .Mimi naona it's depend na mtu na mtu..

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Marekani patamu Zaidi kuliko UK
 
Joannah , Joline Kato , cariha na wengineo, si kweli kwamba ukipita katika mkoa wa Tabora ukiwa kwenye garimoshi na ukachungulia dirishani ukamuona ng'ombe mweusi, basi ng'ombe wote katika mkoa wa Tabora ni weusi!!

Mimi mbona nimekaa Miami (tamka 'Mayami') miaka mitatu tu nikarudi niko vizuri balaa, hadi leo napeta tu hapa mjini. Kama kuna mwana Jf anaijua Miami nimuelekeze nilipokuwa nakaa.
Chai. Ulikua Miami ipi?!
 
Ukiwa ulaya kutoboa africa ni rahisi saana ila ukiwa ulaya ni vigumu saana
Pili na vijana wengi wa africa wana fanya wakifika ulaya wana badirisha lifestyle yao wanatumikisha pesa vibaya saana
Ndo maana wengi wao wanaishia kuwa maskini lakini kwa wale wenye akili kutobowa ulaya ni kitu raisi saana tena saana zaidi ya saana
 
Hizi ndio thread zinazowapa Wabongo faraja moyoni.
Kwa kweli nashangaa kejeli na chuki zilizopo humu dhidi ya watu waliopo nje.

Mimi naamini penye - (negative) Pana + (positive) pia. Penye waliofeli Kuna waliofaulu pia. Bahati mbaya failure ndiyo inaonekana na kupigiwa kelele zaidi. Ni husda. Ni kwa sababu hatupendi kuzidiwa.....

Binafsi nawafahamu watu 3 waliohamia Dsm miaka 20+ wakaja kurudi Kijijini kukata miti ya familia kuchoma mkaa. Mmoja wao kaondoka kabla sijaanza darasa la 1 karudi nikiwa nimehitimu shahada. Wakati huohuo Kuna wengi tu wametusua life humuhumu Dsm. Kuna Mama yupo zake USA kila Mara anaporomosha nyumba za kupangisha hapahapa bongo. Kufeli ama kufaulu kupo popote iwe ndani na hata nje ya nchi, it's all about our mind, and mind your own business.
 
Back
Top Bottom