Karibu hapa kwa malavidavi, nimerudi toka mamtoni na niko njema.....Kiasi tu ukilinganisha na muda waliopoteza huko
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Karibu hapa kwa malavidavi, nimerudi toka mamtoni na niko njema.....Kiasi tu ukilinganisha na muda waliopoteza huko
Wasalaam wanajamvi.
Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.
1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.
Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..
Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.
2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.
3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.
Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.
My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
Wengi walioko nje ya nchi hawanaga mbele wala nyuma, kijana wabongo anamzidi maendeleo Kuna mwingine namjua kakaa Uingereza more than 25 ila alirudi akiwa njaa Kali hana mbele wala nyuma, akarudi ndio kufungua duka la nguo tena akiishi kwa kutegemea Kodi ya nyumba iliyoachwa na wazazi wake, bahati nzuri akapata mwanamke ni Dr ndio kamuoa yeye yupo yupo tu, wengine nawafahamu wako Marekani na Wana maisha magumu mama Yao ni mstaafu ndio huwatumia hela za ku survive, in short wengi walipelekwaga nje na wazazi wasome ila Sasa ni mizigo wanategemea hao wazazi wao na wamepoteza focus za life
Of course nilikuwa na mahesabu...Hivi Kuna binaadamu anaingia tu kwenye mahusiano bila kufanya mahesabu?utakuwa mwehu......sijui labda nyie wanaume
Huyo wa kwanza na stori yako ya kudanga ni nani alie feli maisha kati yako na yeye? Hapo imeshadhihirisha wewe ndo umeshafeli maisha maana unadanga
Hao ndugu zenu wanawakomboa sijakataa,wanawatumia Dollars sawa,hao Ni wachache katika kundi la wengi waliolowea huko...Huyo nduguyo ana mradi wowote hapa nyumbani?amejenga?ukute siku ya kurudi huku Ni mwendo wa kufikia apartment za jangwani sea breeze baada ya miezi sita kwa mama magomeni
We si kuna comment yako humu umewatetea hao wa south A ukasema bora hata hao kidogo wana nafuu[emoji848][emoji848]
Sasa Joannah kipi kimebadilika kutoka miaka hio ya 90 huko Europe na sasa watu hawa win tena wakienda?Miaka ya Sasa sio miaka ya 1900s ambapo mtu akienda nje anaonekana Kama kawin Sana maisha,miaka ya Sasa Mambo yamebadilika Sana Dada watu wanaona kawaida Sana mtu kwenda huko,hii ni kutokana na baadhi yenu mnaorudi mkiwa hoi bila chochote na uraibu juu,wakati uliowaacha unawakuta wamefika mbali.Kama wewe umefanikiwa mshukuru Mungu Ila wengi wao Hali sio shwari,tunawaona tunaishi nao....Hakuna mtu wa kukuonea wivu eti kisa Ni Diaspora hakuna
Inategemea na lengo lako la kwenda nje. Kama ulienda kupiga picha basi utarudi na albam ya picha. Ila kama wewe ni fighter ukikaa nje miaka kumi tu ukiwa serious unatoboa vibaya sanaWana mbwembwe Sana kila saa utasikia nilivyokua Texas,Mara nilivyokua Ibiza Bora mradi watu wajue alishaenda huko khaaa!
Marekani patamu Zaidi kuliko UKwengi walioko marekani naowafahamu wamefika mbali Sana kimaisha huku dar wanamajengo mengi tu ya maana Ila Kuna baadhi pia naowafahamu walikuwa uingereza huwezi kuamini maisha yao .Mimi naona it's depend na mtu na mtu..
Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
Chai. Ulikua Miami ipi?!Joannah , Joline Kato , cariha na wengineo, si kweli kwamba ukipita katika mkoa wa Tabora ukiwa kwenye garimoshi na ukachungulia dirishani ukamuona ng'ombe mweusi, basi ng'ombe wote katika mkoa wa Tabora ni weusi!!
Mimi mbona nimekaa Miami (tamka 'Mayami') miaka mitatu tu nikarudi niko vizuri balaa, hadi leo napeta tu hapa mjini. Kama kuna mwana Jf anaijua Miami nimuelekeze nilipokuwa nakaa.
Miracle mile, wewe umeshafika Miami?Chai. Ulikua Miami ipi?!
Na wakienda nje wakirudi wanataka waonekane wamewahi kwenda nje,utadhani huko nje kuna maajabu yoyote[emoji23]ulimbukeni
Mwaka wa 7 huu nimejichimbia huku nakula watoto wa kilatino. Miracle mile ipo coral gables sio?!Miracle mile, wewe umeshafika Miami?
Wewe kweli uko Miami, Coral gables yeah!.. Unanyoosha barabara ya Lejeune kama unaelekea beach, mambo yakoje siku hizi huko? Ni miaka mingi tangu nirudi home.Mwaka wa 7 huu nimejichimbia huku nakula watoto wa kilatino. Miracle mile ipo coral gables sio?!
Kwa kweli nashangaa kejeli na chuki zilizopo humu dhidi ya watu waliopo nje.Hizi ndio thread zinazowapa Wabongo faraja moyoni.