Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Wewe kweli uko Miami, Coral gables yeah!.. Unanyoosha barabara ya Lejeune kama unaelekea beach, mambo yakoje siku hizi huko? Ni miaka mingi tangu nirudi home.
Mambo yanaenda fresh tu. Nashangaa bi dada anavyoponda diaspora wakati huku kunazidi kutam tu.
Ngoja nimualike aje atoe ukurutu kichwani kwanza.😁😁
 
Shida ya watanzania habari za maanguko ya watu yanafurahiwa sana kuliko wafanikiwao....ndio maana wakianguka wawili wanakuwa maarufu kuliko hata ishirini waliofanikiwa.........

Mentality ya Tanzania sio kumuona mtu anainuka bali matazamio yake ni kumuona mtu anaanguka kwa hiyo mafanikio ya mtu ni kama shock kwake.........

Mentality hiyo imeanzia kwa wananchi mpaka kwa watawala ndio maana hata ukibuni au kuanzisha jambo lenye manufaa kwako na taifa kwa ujumla vikwazo vya kiserikali vinakuwa vingi kuliko kukuinua kwa makusudi kabisa....Hali ambayo ni tofauti kwenye mataifa ya Wenzetu......

AFRIKA kumejaa Hila na roho mabaya kwenye jamii mpaka kwa watawala ndio maana wafanyabiashara wengi wakubwa ni lazima wawe wanasiasa au wajisogeze karibu na wanasiasa kwa usalama biashara na mitaji yao.....

Pamoja na evidence za watu waliofanikiwa na kuinua familia zao lakini bado wanajikita na kuhanikiza kwa waliofeli tu ili mioyo yao ifurahi na ipate nafuu......

Mafanikio ni zawadi ya mtu mwenye bidii na nidhamu kwa kile anachofanya popote chini ya mgongo wa ardhi......

Mambo mazuri au mafanikio hayaji kwa kupiga porojo na kutokuwa na nidhamu bali kwa wenye bidii na nidhamu.......

Hata pepo(kwa wanaoamini) ya Mungu ambacho ni kipimo kikubwa cha mafanikio ya mwanadamu inakulazimu uwe na bidii na nidhamu kwenye mfumo wa taratibu za Imani yako na haipatikani kwa watu wavivu na wasio na nidhamu........

Ukijinasbisha na watu wenye mafanikio utaliona hilo lipo wazi.........

Mtu mvivu asiye na bidii na aliyeanguka kimaisha hutafuta watu wa kufanana nae ili ahalalishe uvivu wake na furaha yake na faraja yake ni kuona wengi wameanguka kama yeye.........

BADO NASISITIZA KWA VIJANA WATAFUTAO MAISHA KUWA POPOTE CHINI YA MGONGO WA ARDHI BIDII NA NIDHAMU KATIKA KILE UNACHOKIFANYA NDIO MSINGI WA MAFANIKIO PENYE FURSA......
 
Umenena vyema

Kitu wengi hawatambui michongo ya ajira unapata kwa connection Za uliosoma nao/wanaokufahamu ukipata chuo

Nakumbuka nilibahatika ajira mara baada ya kuhitimu na alienipa huo mchongo alikuwa ni Lecturer/mhadhiri wangu wa chuo kwakuwa aliona namna ninavyojituma na discipline niliokuwa nayo.

Baada ya kulamba ajira nikaongeza elimu and the rest is now History

Life is 90% luck 10% struggle
90% luck & 10% struggle??? Somebody’s Son Are you serious? So ulisoma utegemee bahati??
Umeishi frugally na kuwa humble yet your life depends on "luck"
 
Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
Pole kwa kuliwa kimasihara kwa tamaa na malengo yako kwake.
Mjanja hapo ni yeye dume. Wewe naona uliingia maboya kwa kudhani ndoa na maendeleo utayapata kirahisi rahisi hivyo. Nadhani umejifunza.
Ulaya ndugu unatoboa. Ni kutokana na malengo yako na utafutaji. Hata ufanye kazi gani, ukifanikiwa ku save, kubana matumizi na kuitumia vyema basi waweza kutoboa kwa haraka na kuwa maisha mazuri tu bongo.
Kambi popote. Ni wewe tu.
Twawajuwa wengi tu waliofanikiwa. Wazee kama lemutuz na vijana kama dogo janja.
Siku nyingine ebu geuza shingo na kutazama vijana wa kibongo kabla ya kuwashobokea wabeba maboksi.
Pia usitoe pipi kirahisi hivyo bila kufanya research ya mtarajiwa…
 
Karudi keshapoteza channel tayari..anyway sikatai wapo wanafanikiwa lakini majority Ni failure
Tatizo lako unaongea kwa kufata mkumbo ,Au unasikia tu story kutoka mtaani,
wengi waliokimbilia ulaya wamefanikiwa sana. wachache ambao hawajielewi wanarudi mikono mitupu .
Hivi unajielewa mtu karudi na miaka 40 unasama kashapoteza channel, wangap hapa bongo wanaumri kama huo na bado wanastruggle kutafuta maisha.
Huyo jamaa yako anamazingira mazuri ya kutoboa sii bongo ama njee akili ndio hana
 
Inategemea, walikuwa hata na hayo makaratasi ya kufanya kazi? Company yao, watu waku party tuu au lah, lengo lao ni kuishi kwa muda mfupi na kurudi tz au kubaki ulaya.
 
Hivi si warudi nyumbani..Kuna watu wanapenda Sana sifa zakijinga kwamba tunakaa Ulaya 😁
Lazima kurudi,?pensheni yangu nani atakula?
Hao wanaorudi wamechoka wazembe tu ,walifika wakalemaa kazi za hovyohovyo wakitoka ni kununua pamba kali ,party kibao wanajisahau.
Then hapo anataka badae arudi bongo.
 
Kwani hamruhusiwi kuondoka na hiyo pensheni lazima mlie hukohuko?kwani nyie si watu huru? anyways muwe mnawakumbusha hao wenzenu wanao jisahau
 
Hapa ndio uwezo wako wa kujenga hoja ulipoishia, ndio maana ma Legends wengi wanaikacha JF, kujibishana na mtu kama wewe ni kupoteza muda ambao ni wa thamani sana, nina log out!
Huna lolote unakaa kwa shemeji yako na kuanza kutoa hadithi za kiwaki
 
Tatizo lako unaongea kwa kufata mkumbo ,Au unasikia tu story kutoka mtaani,
wengi waliokimbilia ulaya wamefanikiwa sana. wachache ambao hawajielewi wanarudi mikono mitupu .
Hivi unajielewa mtu karudi na miaka 40 unasama kashapoteza channel, wangap hapa bongo wanaumri kama huo na bado wanastruggle kutafuta maisha.
Huyo jamaa yako anamazingira mazuri ya kutoboa sii bongo ama njee akili ndio hana
Mkumbo upi unaoungelea,?Mimi ndio nimeleta mada humu na nimeeleza baadhi ya matukio,na wadau wengine wamethibitisha scenarios walizokutana nazo kwa baadhi ya ndugu na jamaa,relax bro,acha kupanic Kama wewe ni miongoni mwao wanaozungumziwa basi jipange kuliko kuleta ubishi usio na mashiko....tatizo hampendi kusikia ukweli
 
Pole kwa kuliwa kimasihara kwa tamaa na malengo yako kwake.
Mjanja hapo ni yeye dume. Wewe naona uliingia maboya kwa kudhani ndoa na maendeleo utayapata kirahisi rahisi hivyo. Nadhani umejifunza.
Ulaya ndugu unatoboa. Ni kutokana na malengo yako na utafutaji. Hata ufanye kazi gani, ukifanikiwa ku save, kubana matumizi na kuitumia vyema basi waweza kutoboa kwa haraka na kuwa maisha mazuri tu bongo.
Kambi popote. Ni wewe tu.
Twawajuwa wengi tu waliofanikiwa. Wazee kama lemutuz na vijana kama dogo janja.
Siku nyingine ebu geuza shingo na kutazama vijana wa kibongo kabla ya kuwashobokea wabeba maboksi.
Pia usitoe pipi kirahisi hivyo bila kufanya research ya mtarajiwa…
Sema kulana kimasihara ,by the way kuliwa kimasihara Ni sehemu ya maisha ya kila siku ya mwanadamu anayekula na kushiba,ukute muda huu mkeo Yuko sehemu analiwa kimasihara tu.sasa sielewi hiyo pole yake inamaanisha nini maana hamna jipya hapo....Acha papara Kama unaoga nje tulia Soma Uzi ndio urudi...
Pipi inatolewa tu,Mungu anaangalia Moyo haangalii pipi...pita hivi
 
Inategemea na lengo lako la kwenda nje. Kama ulienda kupiga picha basi utarudi na albam ya picha. Ila kama wewe ni fighter ukikaa nje miaka kumi tu ukiwa serious unatoboa vibaya sana
Nakuamini
....basi wengi huwa hawana lengo au wanapoteza lengo
 
Hii mada tulishawahi kuiongelea hapa. Wengi Wabongo wenye bahati wanaoenda ughaibuni ni maboya. Wakifika kule wanaiga life style ya wenyeji,anasahau huku nyumbani anatakiwa afanye kitu.

Mfumo wa maisha ya ulaya ni rahisi sana kutoboa ili mradi tu ujitambue. Miaka 7 kukaa Ulaya kama unajitambua unarudi na hela ambayo kwa hapa bongo angeihangaikia maisha yake yote,asipate hata robo yake. Uwe tu na nidhamu ya pesa.Kule kuna kazi nyingi ambazo wenyeji hawataki kuzifanya wanaziona za kirock,kama udereva wa magari makubwa,kupanga mabox kwenye mashopaz,kurudishia bidhaa kwenye mashelvu. Na mshahara wake ni mnono,kiasi unaweza ukamzidi hata boss wa TRA kibongobongo. Kikubwa panga matumizi yako vizuri. Achana na starehe,starehe waachie wenyeji. Sasa unakutana na mbongo kama huyo wa kwanza anaiga life Style ya wenyeji,nae anakuwa hataki hizo kazi. Pili ni machinoo. Pombe kuanzia asubuhi,maisha ya kizungu sana. Huwezi kutoboa.

Kenya uwekezaji mkubwa mkubwa ule unaouona ni vijana wanaoishi ulaya. Ona vijana wa Nigeria pia,wametapakaa ulaya. Ona uwekezaji wao kwenye nchi zao.

Pia unawaona wasomali wanaamua liwalo na liwe wanasafirishwa kama mizigo ili mradi afike South Africa. Akifika South Africa kule ni njia tu ya kuunga ulaya. Na wakifika ulaya haichukui round anakuwa mfadhiri wa ndugu na jamaa zake huko kwao. Unafikiri pesa anaitoa wapi,kama sio kufanya kazi?. Wapo wanaoishia hapo south. Ujue yule uliemsafirisha leo kwa loli,na yule utakaeenda kumkuta South Africa miaka miwili ni tofauti sana. Miaka hiyo miwili atakuwa amepiga sana hatua kimaendeleo. Wanajituma sana wakifika huko tofauti na wabongo wanaoenda huko wengi wanapenda starehe. Mwisho wa siku wanaangukia kwennye sembe. Mpaka sasa vijana wa kibongo waishio south,wengi ni wezi na wauzaji na kutumia sembe ksbb ya kupenda starehe bila kufanya kazi.

Ipo mifano ya watu ninaowafahamu wanaopiga kazi ulaya. Wengine wameingia kule kwa gear ya kusoma,lakini wanapiga na kazi pia. Mmoja anajenga apartment 9 za ukweli mkoa fulani hapa nchini.

Kwa hiyo wengi hawafanikiwi ksbb hawajitambui,wanaendekeza starehe.
 
Mimi hata nikipiga chafya ya ki New York, wabongo wataona nimeamka na hasira.

Kwa sababu hawajazoea chafya ya ki New York.

Inapigwa ki agggressive aggressive mpaka anayepiga chafya anaonekana ana hasira.

Ndiyo maana mara nyingine nasoma tu.
Haya bwana Kiranga nimekulewa.
 
Swali zuri sana hili maana humu hoja nyingi za walioferi huyu kavuliwa kwenye part kirahisi sana alitegemea kwenda Ulaya kaona hamna kitu kaja na Uzi hapa...
Wewe uache ubongo wako u concentrate na mada iliyopo mezani hayo ya kuvuliwa Ni very minor hayakusaidii Wala hakuna maajabu yeyote hapo.
 
Hii mada tulishawahi kuiongelea hapa. Wengi Wabongo wenye bahati wanaoenda ughaibuni ni maboya. Wakifika kule wanaiga life style ya wenyeji,anasahau huku nyumbani anatakiwa afanye kitu.

Mfumo wa maisha ya ulaya ni rahisi sana kutoboa ili mradi tu ujitambue. Miaka 7 kukaa Ulaya kama unajitambua unarudi na hela ambayo kwa hapa bongo angeihangaikia maisha yake yote,asipate hata robo yake. Uwe tu na nidhamu ya pesa.Kule kuna kazi nyingi ambazo wenyeji hawataki kuzifanya wanaziona za kirock,kama udereva wa magari makubwa,kupanga mabox kwenye mashopaz,kurudishia bidhaa kwenye mashelvu. Na mshahara wake ni mnono,kiasi unaweza ukamzidi hata boss wa TRA kibongobongo. Kikubwa panga matumizi yako vizuri. Achana na starehe,starehe waachie wenyeji. Sasa unakutana na mbongo kama huyo wa kwanza anaiga life Style ya wenyeji,nae anakuwa hataki hizo kazi. Pili ni machinoo. Pombe kuanzia asubuhi,maisha ya kizungu sana. Huwezi kutoboa.

Kenya uwekezaji mkubwa mkubwa ule unaouona ni vijana wanaoishi ulaya. Ona vijana wa Nigeria pia,wametapakaa ulaya. Ona uwekezaji wao kwenye nchi zao.

Pia unawaona wasomali wanaamua liwalo na liwe wanasafirishwa kama mizigo ili mradi afike South Africa. Akifika South Africa kule ni njia tu ya kuunga ulaya. Na wakifika ulaya haichukui round anakuwa mfadhiri wa ndugu na jamaa zake huko kwao. Unafikiri pesa anaitoa wapi,kama sio kufanya kazi?. Wapo wanaoishia hapo south. Ujue yule uliemsafirisha leo kwa loli,na yule utakaeenda kumkuta South Africa miaka miwili ni tofauti sana. Miaka hiyo miwili atakuwa amepiga sana hatua kimaendeleo. Wanajituma sana wakifika huko tofauti na wabongo wanaoenda huko wengi wanapenda starehe. Mwisho wa siku wanaangukia kwennye sembe. Mpaka sasa vijana wa kibongo waishio south,wengi ni wezi na wauzaji na kutumia sembe ksbb ya kupenda starehe bila kufanya kazi.

Ipo mifano ya watu ninaowafahamu wanaopiga kazi ulaya. Wengine wameingia kule kwa gear ya kusoma,lakini wanapiga na kazi pia. Mmoja anajenga apartment 9 za ukweli mkoa fulani hapa nchini.

Kwa hiyo wengi hawafanikiwi ksbb hawajitambui,wanaendekeza starehe.
ASANTE umenena Vyema.
 
Back
Top Bottom