Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Hivi kuna uhusiano wa kwenda Ulaya na kufeli maisha?

Sasa Joannah kipi kimebadilika kutoka miaka hio ya 90 huko Europe na sasa watu hawa win tena wakienda?

Mimi naona uko peke yako unayeona ulaya ni pa kawaida, itisha hapo mkutano wa wanaotaka kwenda ulaya uone watakavyojaa maelfu!

Kisha usitudanganye watu wako better huko Tanzania, wakati familia nyingi hazipati milo mitatu and majority lives under 2 dollars per day...

Mwisho km wewe uko Dar usitufokee, jenga kwenu Chitoholi ,lol, ..sio wote wanokuja Dar,wanarudi vijijini wakiwa successful,the same as ulaya...kila mtu apambane na hali yake popote alipo!..lol
Ukisoma Uzi mwanzo mpaka mwisho utapata jibu kwamba siko peke yangu mwenye huo mtazamo....Kubishana na wewe wakati ukweli uko wazi Ni kuchosha akili yangu..Kama wewe ni mmoja Kati ya wale wachache wanao tusua hongera,Ila Kama na wewe ni mmoja katika lile kundi la looser pole dada,,,take your time jipange
 
Asante.ni kweli usemayo
Ukiwa ulaya kutoboa africa ni rahisi saana ila ukiwa ulaya ni vigumu saana
Pili na vijana wengi wa africa wana fanya wakifika ulaya wana badirisha lifestyle yao wanatumikisha pesa vibaya saana
Ndo maana wengi wao wanaishia kuwa maskini lakini kwa wale wenye akili kutobowa ulaya ni kitu raisi saana tena saana zaidi ya saana
 
Kwa kweli nashangaa kejeli na chuki zilizopo humu dhidi ya watu waliopo nje.

Mimi naamini penye - (negative) Pana + (positive) pia. Penye waliofeli Kuna waliofaulu pia. Bahati mbaya failure ndiyo inaonekana na kupigiwa kelele zaidi. Ni husda. Ni kwa sababu hatupendi kuzidiwa.....

Binafsi nawafahamu watu 3 waliohamia Dsm miaka 20+ wakaja kurudi Kijijini kukata miti ya familia kuchoma mkaa. Mmoja wao kaondoka kabla sijaanza darasa la 1 karudi nikiwa nimehitimu shahada. Wakati huohuo Kuna wengi tu wametusua life humuhumu Dsm. Kuna Mama yupo zake USA kila Mara anaporomosha nyumba za kupangisha hapahapa bongo. Kufeli ama kufaulu kupo popote iwe ndani na hata nje ya nchi, it's all about our mind, and mind your own business.
Elewa kinachoongelewa....watu wamekili Kuna wanaotusua maisha na Kuna wengi wanaofeli....na wadau wengi wametoa na Sababu za hao watu kufeli...pitia vizuri uzi Kabla hujalalamika
 
Mambo yanaenda fresh tu. Nashangaa bi dada anavyoponda diaspora wakati huku kunazidi kutam tu.
Ngoja nimualike aje atoe ukurutu kichwani kwanza.😁😁
😂😂😂😂😂Pakufikia pazurii papo lakn?sio nije kufikia magetoni huko kwenye mablock mmebanana hamna hata pakulala....sipendagi ujinga
 
Wasalaam wanajamvi.

Jamani kuna jambo linanifikirisha kwa muda sasa, hivi kuna uhusiano wowote kwa vijana wa makamo wanaorudi toka ughaibuni na kufeli maisha? Nimekutana na case Kama tatu hivi ambazo zimenivuruga kichwa. Nitazielezea kiufupi.

1. Katika hekaheka za humu duniani nilikaribishwa kwenye house party moja maeneo ya Salasala, ilisheheni mbwembwe za kila aina, nilikuwa na wadada warembo na wakaka wamotoo, kila mtu alijifanyia ni mmarekani, Siku hiyo nilijiona nimeokota dodo chini ya mchongoma kwani Kuna jamaa very presentable aliyetambulishwa Kama ndio fresh karudi zake kutoka ughaibuni alitokea kunitunuku. Hapo ndio ulikuwa mwanzo wa penzi tamu nikiwa na matarajio kibao.

Picha linaanzia huyu Bwana hana hata nyumba, kapewa nyumba na wazazi wake maeneo ya Tangi bovu ndio anaishi hapo, huyu Bwana sifa ya umalaya hakubarikiwa, yeye ni mlevi hujapata ona, akiamka asubuhi anaoga, anawasha zake muziki anaanza kunywa whiskey jamani ni asubuhi ya saa tatu, hiyo Ni mpera mpera mpaka atavyolala Sasa sita. Alikuwa anapenda kupika mwenyewe, anapika anakula kidogooo vyote najilia mie yeye anatwanga mipombe yake.. Baada ya miezi kadhaa nikaanza muuliza ana mpango gani wa maisha? Kazi au biashara hana jibu sahihi.. Nina search zoom namuonyesha nafasi za kazi jibu lake sawa nita apply, miezi inayoyoma yule bwana hastuki wala nini. Imagine mtu ana 41 anapewa pocket money na mama..

Nikaanza lalamika kwa ndugu zake wa karibu, mtoto wa baba yake mdogo akaniita faragha "Kama kweli una ndoto na maisha yako hapo unapoteza muda wako buree huyo hajarudi na kitu chochote zaidi ya begi lake na picha za kwenye barafu, huko Germany hajasoma chochote na wala huku nyumbani hajainvest kitu chochote kufupi Ni kwamba"Kaenda KUZURURA miaka Saba halafu karudi hoi.. Nikachoka na penzi likafa.. Ila penzi lake lilikuwa tamu sana hana kero, muelewa, romantic kwa kweli abarikiwe Sana na atolewe tozo kwenye kila muamala ataofanya.

2. Huyu ni kaka wa best friend wangu, siku anaondoka hadi airport tumemsindikiza akielekea UK akiahidi ahadi kedekede lazima apambane atoke kimaisha kwamba nafasi aliyoipata hawezi chezea. Jamani kaenda huko miaka sita baadae hata nauli ya kurudi ilibidi atumiwe, karudi hana hata mia yupo tu amekuwa mwamba wa kupiga virungu.

3. Huyu wa tatu nahisi ndio kamaliza Ulaya yoteee kikubwa anachomiliki Ni saa aina Seiko anadai Ni original alinunua Milan, simu yake ya smartphone, kiingereza kilichonyooka na album yake ya Google photos ikiwa imesheheni picha pambe kabisa zenye mandhali ya kuvutia sana. Nae kwa virungu na uchawa hajambo.

Sasa Hawa Ni mfano tu wa wengi wanaokwenda huko ughaibuni na kurudi tee. Hebu tuwaulize nyie mnaojiita Diaspora huko huwa mnafanya nini? Wenzenu huku nyumbani Mambo yetu ni bambam tumeoana, tuna watoto, tunaishi vizuri. Sasa huko jamani mbona Kama mnapoteza muda Ila mkitupia picha mnatuvimbia kwelikweli ilihali si uhalisia.

My Take Kama huko Mambo meusi rudini nyumbani tujenge nchi. Nyie vijana wenye ndoto za kwenda kusaka tonge huko ughaibuni nawashauri mpambane tu hapa nyumbani mtatoboa unless mkachukue elimu mrudi.
Mbona kama haipenyi akilini, nchi za wenzetu kwa nijuavyo mimi kazi zipo nyingi na pay ni uhakika.
Imagine rate ya chini ni usd14 per hour, afu huyu mtu afanye kazi miaka sita aiseee naweza sema ukirudi masikini wewe utakuwa mtoto wa mama uliendekeza starehe na ulimbukeni wa kishamba kabisa ila kwa mtu aliepitia msoto sidhani kama hii inawezekana.
 
🤣🤣🤣🤣🤣Dear X....fanya kazi acha kumbwela
Daaaaah nimebaki kusikitika tu...kuna jamaa nlikutana nae mbele mbele hhhuko tulikuwa tunabadilisha ndege likuwa anaenda US alivyorud mambo anayofanya naona aibu mimi..Yan kababisha nisiwe naenda mayfair yan anaapiga virungu askari wa jiwe wanasubir...Mayfair ndio kituo yake ya kaziii...
 
Sema wewe Kaka umeyaona,Kuna wengine wapo humu wananigombeza eti Sina exposure,eti Mimi Ni wamashambani....lkn Mambo wanayofanya baadhi yao wakirudi ndio haya
 
Sema wewe Kaka umeyaona,Kuna wengine wapo humu wananigombeza eti Sina exposure,eti Mimi Ni wamashambani....lkn Mambo wanayofanya baadhi yao wakirudi ndio haya
Yan mwanaume anaamka anaenda kujitega mayfair ukitokea anakujua kazi unayo, na anajuana na watu wakuu wakuu, siku nkamwona anampiga kirungu nape mh, mwanaume anaish kwa virungu na amekaa sana US, tabia mbaya kbsa
 
Ukisoma Uzi mwanzo mpaka mwisho utapata jibu kwamba siko peke yangu mwenye huo mtazamo....Kubishana na wewe wakati ukweli uko wazi Ni kuchosha akili yangu..Kama wewe ni mmoja Kati ya wale wachache wanao tusua hongera,Ila Kama na wewe ni mmoja katika lile kundi la looser pole dada,,,take your time jipange
Dada endelea na mission yako kutaka kuonyesha mbele hakufai, nimekupa facts ungenijibu kwa facts sio kumbwela mbwela,bye
 
Daaaaah nimebaki kusikitika tu...kuna jamaa nlikutana nae mbele mbele hhhuko tulikuwa tunabadilisha ndege likuwa anaenda US alivyorud mambo anayofanya naona aibu mimi..Yan kababisha nisiwe naenda mayfair yan anaapiga virungu askari wa jiwe wanasubir...Mayfair ndio kituo yake ya kaziii...
Rebeca 83 Kabla hujaondoka pita hapa
 
Yan mwanaume anaamka anaenda kujitega mayfair ukitokea anakujua kazi unayo, na anajuana na watu wakuu wakuu, siku nkamwona anampiga kirungu nape mh, mwanaume anaish kwa virungu na amekaa sana US, tabia mbaya kbsa
Imagine haogopi hata mheshimiwa!huyo Ni nguli kabisa
 
Na Wanawake wanao olewa na Wazungu na kupelekwa kuishi Ulaya jee? Hawa ni wengi sana ukilinganisha na Wanaume ambao mara nyingi wakienda Ulaya ni kwa efforts zao binafsi.
 
Back
Top Bottom