Chukua hata watoto yatima, wako kwenye vituo mbalimbali, wanatamani sana wazazi na kukaa nyumbani, sio kwenye vituo hivyo, wanatamani sana kuita Baba,Mama, Dada, Kaka, Shangazi n.k, mbona kuna watu wanafanya hivyo, hasa Ulaya, walee kama sehemu ya familia yako kabisa, uwatambulishe kwa ndugu zako, upiganie, uhakikishe, watoto hao na ndugu zako, wanapendana, kujaliana, kuheshimiana na kuthaminiana vizuri, wasomeshe vizuri, wape pia sehemu ya mali yako itakayowafaa maishani, watakutunza mno, we wasomeshe na kuwalea vizuri, hutapata shida uzeeni, watakutunza, usiwe na shaka, wapo watu waliotunzwa na familia za watu wengine, wanazijali sana hizo familia na kuwasomesha watoto au wajukuu wa hizo familia na wanaishi kama ndugu wa damu kabisa, kiasi mtu asiyewajua hataweza kujua kama si ndugu, mpaka mbea amwambie, undugu kufaana, sio kufanana, na akufaaye kwa dhiki ndiye rafiki wa kweli, mfaaye, mjali na yeye atakufaa na kukujali uzeeni kama mzazi wake wa kumzaa, Mungu atakuongoza.