Hivi kuna wanachama wa JF wanaoishi vijijini?

Mimi nipo kijijini ila panaitwa ulaya ni kilosa mkoani morogoro. Mimi ndo mjanja wao huku. Nikienda dar nafikiaga kwa shemeji yangu nalala sebuleni kwenye makochi,naangalia TV usiku kucha.
Ulaya na tindiga tuko karibu,asee tukutane Uwanja wa Azimio ,Mavuno cup
 
Ulaya na tindiga tuko karibu,asee tukutane Uwanja wa Azimio ,Mavuno cup
Haaa haaa haaa dah kweli we wa kilosa mwenzangu. Uje mpaka njiapanda ya tende utanikuta mkuu niende nikakupe maziwa mtindi hapo magomeni.
 
Jina nalotumia JF linasadifu nilipo acha mtandao wa shida hapa kuna wakati napata tabu sana
 
Nipo TUBUGWE - KONGWA, na Last Friday tulikuwa na Mh. Mbunge wetu Ktk uwanja wa Mpira TUBUGWE, alikuja kutoa zawadi kwa washindi! Katika mashindano yake aliyoyaanzisha yeye mwenyewe!

Tangu nusu ya pili ya mwaka 2018 anazunguuka sana vijiji vyetu. Huku wanasema atakuja sana kipindi hiki mpk 2020!

Pia amesema atatuwekea lami barabara ya MLALI - TUBUGWE! Kiukweli sisi watu wa Kongwa tuna bahati Sana!

From nowhere, Jumatatu ilopita wakaja ma VX ya waziri wa nishati, akatukusanya, akahutubia! Akasema "naamuru TANESCO msiondoke site (Tambi - Kijiji jirani) mpk umeme uwake! Cha ajabu hakukuwa na nguzo wa shimo!

Nikawa nasubiria kuona " wireless electric power!" Hamna Kitu na washaondoka!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…