Kuna habari ya nabii mmoja anaitwa Eliya, basi siku moja akamwambia Mungu kuwa amebaki peke yake tu na adui zake wanatafuta kumuua. Mungu akamwambia ninao manabii wengine 700 ambao hawaja abudu kwa miungu.
Ndivyo watu wengi huwa tunachukulia mambo, kwamba maadamu jambo la kuchepuka linatangazwa sana , linaonekana kama sifa nzuri, limepewa jina zurizuri, kwamba watu wenngi sana au wote watakuwa wako hivyo. LAKINI mara nyingi sana watu wengi hawako hivyo.
Nina miaka 10+ kwenye ndoa, sijawahi kuchepuka, sina hata hilo wazo, ni msimamo nilishaweka. Na kwa sababu hiyo nimejifunza kujiepusha na mazingira hatarishi. Utani utani wa kimapenzi, mizaha mizaha ya kimapenzi, chating zisizo na maana, mazoea mazoea n.k , vitu kama hivi sitoi nafasi kabisa.
Kwenye ndoa yetu, simu zetu ni kitu cha pamoja wote wawili.
Tusiite kuchepuka, tuite tu kuzini, kufanya uasherati, uhuni, ukahaba n.k
Madhara kwenye jamii ni makubwa, tukemee kabisa hiki kitendo kiovu, kichafu, kisichofaa kabisa.