Hivi kuna wanandoa ambao hawachepuki kabisa?

Naona umeona umchane!
Dawa ya uzinzi ni kuikimbia na kuhakikisha akili yako haielekei huko kwani tatizo huanzia kwenye mawazo na ikikaa hadi kufikia moyoni ni vigumu sana kuishinda dhambi hiyo ya uzinzi. Haijalishi umeokoka ama hujaokoka. Ndio maana kuna walokole wameanguka kwenye dhambi hii na kuna ambao si mtu wa dini lakini kwa kuwa amedhibiti akili yake hafanyi dhambi hii. YESU alipomwokoa mama mmoja ambaye alikuwa apigwe mawe kuuawa kwa sababu ya uzinzi, alimwambia aende na asifanye tena dhambi - hakutoa pepo. Hivyo ni uamuzi wa mtu binafsi kuacha uzinzi, usisingizie mtu. Dhibiti mawazo yako.
 
Wapo walio waaminifu na ndoa zao, lkn kwa kuwa kuchepuka kunapigiwa debe bas hii inapelekea waaminifu ktka ndoa zao kutokuonekana kwny jamii.

Lkn waaminifu wapo.
 
Kuna habari ya nabii mmoja anaitwa Eliya, basi siku moja akamwambia Mungu kuwa amebaki peke yake tu na adui zake wanatafuta kumuua. Mungu akamwambia ninao manabii wengine 700 ambao hawaja abudu kwa miungu.

Ndivyo watu wengi huwa tunachukulia mambo, kwamba maadamu jambo la kuchepuka linatangazwa sana , linaonekana kama sifa nzuri, limepewa jina zurizuri, kwamba watu wenngi sana au wote watakuwa wako hivyo. LAKINI mara nyingi sana watu wengi hawako hivyo.

Nina miaka 10+ kwenye ndoa, sijawahi kuchepuka, sina hata hilo wazo, ni msimamo nilishaweka. Na kwa sababu hiyo nimejifunza kujiepusha na mazingira hatarishi. Utani utani wa kimapenzi, mizaha mizaha ya kimapenzi, chating zisizo na maana, mazoea mazoea n.k , vitu kama hivi sitoi nafasi kabisa.

Kwenye ndoa yetu, simu zetu ni kitu cha pamoja wote wawili.

Tusiite kuchepuka, tuite tu kuzini, kufanya uasherati, uhuni, ukahaba n.k
Madhara kwenye jamii ni makubwa, tukemee kabisa hiki kitendo kiovu, kichafu, kisichofaa kabisa.
 
Mungu wetu wa Mbinguni akubariki
Umetukumbusha swala la Msingi sana
Aaminiye na kubatizwa ataokoka asieamini amekwisha kuhukumiwa
 
Umenena sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…