Hivi kuna wanaoamini mapenzi ya kweli kama mimi?

Hivi kuna wanaoamini mapenzi ya kweli kama mimi?

Mapenzi ya kweli yapo na ni matamu sana , ni namna ya kumpata huyo mwenzi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Sijawahi kukutana nayo , siamini sana kama yapo!
Ni bahati tu kukutana na mume au mke wa kufanana naye mkawa na "love chemistry", pia kuondoa imani moyo ya kuamini kwamba mapenzi ya kweli hayapo wakati si kweli .

Mapenzi ya kweli yapo , mume mwema yupo na mke mwema yupo kabisa na tupo nao mitaani, kwenye mitandao, mfano jamiiforum, Facebook n.k., makazini, kila mahali, swali ni utamjuaje, ukimjua kumpata ni rahisi sana.
Na ni vizuri sana wakati mwingine kujichanganya kuwepo kwenye matamasha, kwenye ibada, huko pia unaweza kutana na mume wako au mke wako mwema.

Kuna watu wengi wapo wanajiheshimu sana pia wakisubiria wenzi wema wa maisha yao .
Pia usiwe muoga kumwambia mtu ukweli wako juu yake kama ndiye unaye shuhudiwa kuwa ndiye mke wako au mume wako.

Woga huwa unatufanya watu wengi tupishanishwe na yule ambaye MUNGU amekusudia kuwa naye kwenye mahusiano ya kindoa.

Kwenye kitabu cha Isaya 34:16- imeandikwa hivi ," Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome, hapana katika hao wote atakayekosa kuwepo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake, kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.
Maana yake ndiyo kama nilivyoeleza hapo juu, umuhimu wa kutoka na kujichanganya kwenye ibada, mikusanyiko na matamasha , mfano ya injili nk.
 
Licha ya kwamba marafiki zangu wengi Ni dungadunga na madungwadungwa,mm sijaathiriwa na hiyo tabia, bado nimetulia zangu nikiwa single nikitafuta anayeendana na Mimi; mwenye mapenzi ya kweli na uaminifu kwenye mahusiano.

Kwa bahati mbaya madem waaminifu kuwapata ni vigum, hata ukiwapata hawakuamini kirahisi.

Bado naamini ni swala la muda tu nitakuja kumpata. Amen.

Hivi kuna watu humu JF mna mindset kama yangu maana tamaa ya ngono na pesa imeharibu mahusiano ya siku hizi.

naamini hii kitu 100%
 
Kwa dunia ya sasa mapenzi ya kweli yanapatikana endapo mwanaume utakuwa na sifa zifuatazo

1.Una Kazi inayokuingizia kipato

2.Una biashara inayoeleweka

3.Unamiliki assets zinazoeleweka

4.Una hela ya kubadilisha mboga

Kama huna sifa moja wapo hapo juu mapenzi ya kweli utayapata mwanamke anajiuza ambae anatumia papuchi yake ipigwe na wanaume wengine kukulisha ww mwanaume wake na familia
sio kweli
 
Kwa dunia ya sasa mapenzi ya kweli yanapatikana endapo mwanaume utakuwa na sifa zifuatazo

1.Una Kazi inayokuingizia kipato

2.Una biashara inayoeleweka

3.Unamiliki assets zinazoeleweka

4.Una hela ya kubadilisha mboga

Kama huna sifa moja wapo hapo juu mapenzi ya kweli utayapata mwanamke anajiuza ambae anatumia papuchi yake ipigwe na wanaume wengine kukulisha ww mwanaume wake na familia
Bill gate anavyote hivyo na ameachwa mkuu....hayo madudu hayana formula chief.
 
Naamini mapenzi ya kweli yapo. Yapo kabisa yapo.

Tatizo linakuja mmojawapo anapokua na ubinafsi, ama kuona mapenzi ni hisani. Yaani ni kama anafanya msaada ama faviur kuwa na wewe. Na wakati mwingine kuviziana makosa. Yaan mtu anakua amekaa kivita muda wote. Mtu anakua kwenye mahusiano kwa kujihami. Si sawa kabisa. Mtu anapaswa kuachilia moyo wake. Mapenzi si huruma wala hisani.

I love you my eternal partner. All will be well[emoji120][emoji120]
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
NIKIRI UKWELI. NATURALLY NILIZALIWA KUPENDA, YAANI NILIANZA KUPENDA (Upendo wa kawaida) NIKIWA MDOGO SANA. kuna mgeni alikuja kututembelea akaja na binti yake, aisee nilimpenda sana ndani ya masaa tu.

ila walimwengu wameuspoil moyo wangu

Sent from my Infinix X572 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom