Sijawahi kukutana nayo , siamini sana kama yapo!
Ni bahati tu kukutana na mume au mke wa kufanana naye mkawa na "love chemistry", pia kuondoa imani moyo ya kuamini kwamba mapenzi ya kweli hayapo wakati si kweli .
Mapenzi ya kweli yapo , mume mwema yupo na mke mwema yupo kabisa na tupo nao mitaani, kwenye mitandao, mfano jamiiforum, Facebook n.k., makazini, kila mahali, swali ni utamjuaje, ukimjua kumpata ni rahisi sana.
Na ni vizuri sana wakati mwingine kujichanganya kuwepo kwenye matamasha, kwenye ibada, huko pia unaweza kutana na mume wako au mke wako mwema.
Kuna watu wengi wapo wanajiheshimu sana pia wakisubiria wenzi wema wa maisha yao .
Pia usiwe muoga kumwambia mtu ukweli wako juu yake kama ndiye unaye shuhudiwa kuwa ndiye mke wako au mume wako.
Woga huwa unatufanya watu wengi tupishanishwe na yule ambaye MUNGU amekusudia kuwa naye kwenye mahusiano ya kindoa.
Kwenye kitabu cha Isaya 34:16- imeandikwa hivi ," Tafuteni katika kitabu cha BWANA mkasome, hapana katika hao wote atakayekosa kuwepo, hapana mmoja atakayemkosa mwenzake, kwa maana kinywa changu kimeamuru, na roho yake imewakusanya.
Maana yake ndiyo kama nilivyoeleza hapo juu, umuhimu wa kutoka na kujichanganya kwenye ibada, mikusanyiko na matamasha , mfano ya injili nk.