Hivi kuna watu sijui wanawachukuliaje watu wengine

Hivi kuna watu sijui wanawachukuliaje watu wengine

Hapo kipengele unacho wewe mkuu, jenga maghorofa 2, tafuta akiba ya milioni 900, ishi vizuri, simu zitaita hadi utakuja hapa na uzi wa kulalamika.
 
We nani kakwambia simu yako ni ya muhimu sana kwamba lazima upokelewe?
Kuchangia harusi siyo deni usichange kwa lengo la wewe uje uchangiwe kama huna acha ila kunichangia siyo kigezo cha mimi kukuchangia pia.
Wee kobaz acha roho mbaya.
 
Kwanini upige simu mara 3? Ukiona bado unajiliza liza watu hawapokei simu ujue una safari ndefu sana, mtu hajapokea achana naye fanya mambo mengine.. na wewe ukipigiwa wala sio lazima kupokea.

Alafu hapo kwenye tajiri umechomekea tu, wewe bado ni kapuku tena mpka namna yako ya kufikiri!
 
Wachangiaji wengi wanamwambia mleta mada atafute hela ili athaminiwe,

Ni kweli hela huleta heshima kwa Dunia ya sasa but heshima hiyo ni fake,shallow respect that vanishes when money dissapear,

Pesa mara nyingi hununua heshima ya juu juu,umakini na ushawishi na kuwafanya watu wakuone kama vile ni mtu special kutokana na rasilimali zako badala ya tabia yako,

Inasikitisha kuona Binadamu tumeipa mamlaka,Nguvu hela itutawale mpaka kwenye utu wetu!

Heshima ya kweli na ya kudumu inatokana na unyenyekevu,uadilifu na jinsi unavyowatendea wengine,
True respect is earned through actions,generosity and humility not just by having Bank balance,

Binadamu tusipoteze utu wetu sababu tu ya material possession,tutapoteza maana halisi ya maisha.
 
Usilaumu watu kushindwa kupokea simu zako hujui wapo mazingira gani na wanafanya nn au wanapitia nini
Pia simu niyakwake anamaamuzi yake juu ya simu yake
 
Yaani kwa mfano unachat na mtu halafu una cha kumwambia lakini unaona ni bora kumpigia kuliko kuandika meseji.

Mlikuwa mnachati hata sekunde 30 hazijapita unampigia simu.

Simu Nita weee lakini wapi, haipokelewi.

Sasa hapo maswali lukuki yanaanza kukaa kichwani……

Kwa mfano, ‘huyu fala si tulikuwa tanachaji sekunde kadhaa tu zilizopita halafu nampigia ila hapokei.

Cha ajabu, simu ikishakata, huyo fala anakutumia meseji halafu anajikausha kama vile hukumpigia simu 😉.

🖕🖕
Hahahhahaah. Dah. Basi sirudii tena umeamua kunishtaki kwa mods.
 
Mimi napokea simu ya aina zote, kikubwa njoo na heshima yako tuu,

Ni shida nayoweza kukusaidia nitakujibu, siwezi nitakujibu

Ila siwezi kukataa kupokea simu inapoingia

Pesa inakupa heshima Ila heshima yake kwa utu uzima wangu nimekuja kugundua ni heshima ya unafiki, ikose hiyo pesa kama watu au hao waliokuwa wanakuheshima km watakuheshimu,

Nimekuja kuhitimisha tunakuwa km miti kando ya mito itaelkza mizizi yake kwenye chanzo Cha maji ili ifyonze maji vzr, mto ukikauka na mti hudhoofika, ndivyo binadamu tulivyo tunajisogeza penye fursa hata kwa unafiki tuu mzee
 
Baba yangu alikuwa akifika NBC bank anapelekwa kwa Meneja moja kwa moja hata kwenye line hakai. Nilimuuliza kwanini yeye hakai kwenye foleni ya kwa Teller alinijibu pesa ndio heshima.

Wale wazee niliokuwa mdogo nawapa salamu ya unyenyekevu kwa utuuzima wao. Sasa nikiwasalimu wao ndio wanani nyanyapaa. Mleta mada ikumbuke kauli ya baba yangu hapo juu, Ukiona hutafutwi huna cha kusababisha ukatafutwa(hela)
Heshima kwa sababu ya pesa si heshima halisi!!
 
Back
Top Bottom