Melki Wamatukio
JF-Expert Member
- May 3, 2022
- 6,367
- 11,604
Ila cha kwanza nipende kumshukuru Mungu kwa kunitwisha utu uzima. Mimi wa zamani humu ndani nilikuwa namiliki ma-Range, nyumba kali Sinza, Car Wash moja matata pale Madale bila kusahau mke mzuri tu, housegirl na mtoto mmoja wa kiume aitwaye RomyJohnson.
Nilikuwa na nafasi kubwa sana pale Wilaya Ilala bila kusahau kitambi cha kufutia smartphone. Cha kusikitisha hayo yote yalikuwa ni ya kufikirika. Kuna baadhi ya watu walinirejea piemuni na kuniuliza kulikoni mkuu unaulizia tena biashara ya mtaji wa laki moja ilihali ulinishauri nisinunue gari aina ya Avoki kwa kuwa zinakunywa sana mafuta?
Nilivyokuwa ninapita kwenye nyuzi za marijendari waliokuwa wanasimulia namna walivyoichapa kwa kibunda cha Tsh. 500,000 nilikuwa naguna na kujua huenda nu wale wale wenzangu na mie wakiishi maisha ya kioo, lakini kumbe sio sawa, leo ndo nimeamini kuwa kuna watu iko na pesa, yaani mtu anampatia binti wa kyuo kyikuu X laki saba keshi mbele ya macho yangu halafu anamwambia akatumie kwa chakula halafu wataonana wiki ijayo amuongeze, dah! kuna watu wana hela aisee!
Kipindi kile nashauriwa kujiunga na mafunzo ya Uafisa Usafirishaji nilikuwa nakaza fuvu eti naogopa kutokusikia la mkuu nisije kuvunjika guu, jirani yangu anakuja na kibunda cha laki kutoka Bolt per day na hana hata cheti cha darasa la saba. Kweli haya maisha ni fumbo
Wacha ningojee pale nitakapozaliwa upya tena...