Hivi kuwa Mlinzi wa Viongozi ni kibali cha kutishia watu kuwaua tu?! Inakera sana!

Hivi kuwa Mlinzi wa Viongozi ni kibali cha kutishia watu kuwaua tu?! Inakera sana!

jitombashisho

JF-Expert Member
Joined
Jun 11, 2020
Posts
667
Reaction score
2,245
Yaani hii tabia ya vijana hasa wenye umri mdogo walinzi wa viongozi ya kutishia kuwapiga watu na risasi si ya haki kabisa.

Mchana huu hapa maeneo ya Ihumwa Dodoma karibu na makazi ya mkubwa mmoja mstaafu bwana mdogo mmoja akiwa na ndani ya v8 nyeusi yenye vioo vya giza amemtishia msukuma toroli kumpiga na bastora kisa tu amegoma kumpisha kwenye njia ya mchepuko.

Maskini kijana wa watu akiwa na lumbesa la mawe ndani ya mkokoteni ilimuwia vigumu kupisha gari lile la kifahari na busara kidogo tu ilihitajika kwa dereva wa v8 angesubiri yule kijana apite na ndiposa pia naye akate kona.

Kwakweli leo ndiyo nimekerwa mno na vitisho vya namna ile!
 
Wengi ni vilaza wamewekwa bila utaratibu....wengi walifeli shuleni
Nchi ina mfumo wa hovyo sana sisi tumesema kwenye utawala wa mkapa, kikwete na sasa magufuli tuna mfumo wa hovyo mno na hatufanyi vetting ya kutosha sasa idara imevamiwa na wahuni wa ccm na pia wazee wamewekwa bench, nchi ipo hoi sana.
 
Maskini kijana wa watu akiwa na lumbesa la mawe ndani ya mkokoteni .........

Si angemuweka tu hayo mawe ya kichwa au unapasua vioo tu, hao jamaa wanakera sana wakikaa kwenye magari yao hayo wanaona wamemaliza kila kitu shwain!

Let's meet at the top, cheers 🥂
 
Nchi ina mfumo wa hovyo sana sisi tumesema kwenye utawala wa mkapa, kikwete na sasa magufuli tuna mfumo wa hovyo mno na hatufanyi vetting ya kutosha sasa idara imevamiwa na wahuni wa ccm na pia wazee wamewekwa bench, nchi ipo hoi sana.
Hama nchi mkuu usije kufa na stress bure!!
 
Back
Top Bottom