Hivi kuwa single mama ni ulemavu au kosa?

Hivi kuwa single mama ni ulemavu au kosa?

Naongezea na wale strong women na super woman.
Amepata elimu, kapata kazi na biashara kafungua basi yeye Ni strong woman,sasa who is weak woman?

Huku kwenye vicoba,makundi kibao strong woman,wake Za matajiri na wale wakudunduliza kweli jamani kuna maendeleo Hapo???

Jifunzeni kwa wanaume, huwezi kusikia mwanaume analeta tambo za kijinga mbele ya wanaume wenzake tena kwenye mambo ya msingi..km tunajadiliana ishu ya maendeleo tuweka utani pembeni,vyeo pembeni,sifa pembeni.Na kweli tunajadili ishu kwa kuheshimiana sio kwa status zetu..
 
Yaan huu Uzi ukiufikria sana mtu unashindwa hata kutoa comment.Ila Mimi Kwa mawazo yangu naona irrational beliefs ndo inayosababisha kuwepo Na hawa single yaan mtu akiona ana miaka 25+ anajiona hana thaman ya kuolewa hivyo Bora akatafute mtu azae tuu ili aweze kulea watoto.. wenyewe wanasema umri umeenda
 
kukamata fursa.Ukiona kuna tamasha la single mothers jua kuna mtu anaingiza mkwanja.Matatizo ya watu ndo fursa yako ya kuingiza mkwanja.Single mothers wapo desparate,ni kweli kulea mtoto/watoto peke yako siyo kazi rahisi kwa kweli.
 
Nakuunga mkononkwa kiasi kikubwa mimi pia huwa inanikera hasa ukizingatia wanaume wengi humu wanatoka na hao singo maza ila akifika jf anaponda si ajabu mama yake au dada yake au shangazi yake ni singo maza

Na mimi natoka sana na hao singi maza na ukiangalia ukweli sisi wanaume ndio tuozalisha hao singo mazas
 
Hakuna kitu kama "single mother". Hakuna mtoto asiye na baba.

Kujiita "single mother" ni kujipachika jina la kuhurumiwa. Unacheza na akili za watu.
Duuh maneno mazito kabisa kuwahi kuyasikia kutoka Kwa mwanamke ningekua nauwezo ningetoa posa kabisa
 
Hujaelewa context ya hilo jina!

Wewe sio native English speaker,natives wenye lugha yao ndio wametoa hilo jina!

Sijui wewe unawabishia wenye lugha yao meaning na context yao wewe kama nani hasa?

Wewe sio native English speaker,sio English language scholar,sio yeyote hapo,ila unawabishia matumizi yao kwa maana yao waliyojiwekea wao,sijui haya mapafu unatolea wapi?
Nnaota ki English wacha kukielewa. Hilo si jina, ni sifa. Sifa mbaya ki maadili. Siioni sababu ya mtu kujisifu kuwa eti ni "single mother". Mtoto yupi asiye na baba?
 
Na wasipoolewa mpaka 25+ mnasema wamezeeka hamuwaoi
Ni ujinga kuzaa na mwanaume ambaye sio mume wako...ni sawa na kubet kwa pesa ya chakula, ikiliwa umelala njaa.
 
single mother vumilieni tu mbona sisi wenye vibamia kila kona tunakutana na mabango ya kuongeza uume lakini hatutetereki?
 
Na wasipoolewa mpaka 25+ mnasema wamezeeka hamuwaoi
Sio kweli, mbona wanawake kibao wanaolewa kwenye 30's!! Besides, kwani kuolewa ni lazima? Kuna watu wameolewa halafu ndoa imevunjika baada ya mwaka, tayari hapo kuna single mother....wanawake wana nafasi kubwa kuamua hatma zao, hasa kama watatuliza akili kujua yupi mwanaume sahihi kwake
 
Nnaota ki English wacha kukielewa. Hilo si jina, ni sifa. Sifa mbaya ki maadili. Siioni sababu ya mtu kujisifu kuwa eti ni "single mother". Mtoto yupi asiye na baba?

Ni sifa ndio,nimetaja neno 'jina" metaphorically!

Single mama gani kajisifu?

Kwanini response yako imekua reactionary sana kwao?

Watoto wote wana baba biologically ila socially sio wote!

Na hili unalijua!

Inaonesha una maadili sana mpaka unapata mamlaka ya kuhukumu wanadamu wengine.

Thats cute really!
 
Ikiwa wana baba zao "biologically" huo u "single" unatoka wapi? Hiyo ni "terminology" iliyotumiwa ili kuletwe huruma fulani. Nchi za nje (ambako nimeishi kwa muda mrefu kuliko Tanzania) wengi wametumia sifa hiyo kupata huruma ya "social benefits". Lakini ukweli ni kuwa wengi pia wamekuwa wakii "abuse" system ya "social benefits" kwa kutumia sifa hiyo.

Ki uhalisia ni sifa za kuiba ambazo hazina maadili kabisa ndiyo maana sikubaliani nayo. Kimalezi niliyokulia, kuwa "single mother" mwenye kuishi kivyako ni kuwa mama mzaa kiharamu.

Jamii niliyokulia, mtoto asiye na baba ni yatima na yatima si wa kulelewa na "single mother". Kwanza ni jukumu la ndugu wa karibu kumuhifadhi mtoto na mama aliyefiwa na mumewe ili mtoto/watoto walelewe kama vile hawajaondokewa baba mzazi na hali kadhalika kwa aliye achana na mumewe.

Ni upuuzi kujisifu u "single mother".
 
Huu ni ukweli mchungu...
Habari zenu,sihitaji kashfa wala matusi hapa maana kuna watakatifu humu koo zao hazina singo mama wala walioachana..

Jf wanapita watu wengi mnoo!!!waliojiunga na wasiojiunga naomba kuuliza hivi singo mama siku hizi imekua ulemavu,kosa,dhambi au fursa!

Mimi sielewi maana naona Mara makongamano ya masingo maza,Mara sijui tamasha La singo mama,uwaunge mkono sijui uwachangie...jamani!!!

Hivi wanawake kwa nini tunapenda kujiona sisi ni waathirika wa kila jambo ambalo jamii inaliangali ktk mrengo tofauti...?

Mbona hakuna hayo mambo kwa wababa wanaolea watoto wenyewe?au wao hawakutani na changamoto za kimalezi?

Mimi binafsi sipendi na nachukia hii kitu (mniwie radhi kwa nitakaowakwaza)ila naona kama vile kujidhalilisha flani hivi...au ndo kutojiamini kama tunaweza!kwa staili hii tunataka usawa na wanaume...haitokaa itokee mpk Yesu arudi...!!!

Kama uliweza kubeba mimba,ikataliwe isikataliwe ukajifungua watoto au mtoto wako mwenyewe kwa nini usikomae mbona vijijini huko watu wanatelekezwa na wanalea watoto wao bila misaada?

Kama umetengana na mmeo au mmeachana kama unahisi huwezi kuwahudumia watoto si uwapeleke kwa baba yao?kama hutaki kaa nao Leo mwenyewe!!!

Yaani sasa hivi huku mijini masingo mama naona wanafanywa mitaji na watu wachache kujiingizia kipato na wenyewe wanaona kama wanapendwa kumbe hawajui ukiona umeitiwa fursa basi jua wewe ndo fursa yenyewe!!!

Wapo wanawake wengi wanalea watoto wao tena kwa shida na hawapigi kelele kimya kimya mpk wanakua!

Wamama wenzangu hii mitandao isifanye tujidhalilishe jamani...hebu tupambane kivingine sio mpk matangazo..maana huko kwenye mitandao siku hizi sijui wameonelea biashara ya Kuwakusanya singo mamaz inalipa kila mtu anaibuka na hoja zake!!

Tuinuke tupambane tusipende kujiweka nyuma!!!
 
Hongera kwa thread nzuri sana.

Hakika unajielewa. 1 woman in 50 MMU.
 
Ni sifa ndio,nimetaja neno 'jina" metaphorically!

Single mama gani kajisifu?

Kwanini response yako imekua reactionary sana kwao?

Watoto wote wana baba biologically ila socially sio wote!

Na hili unalijua!

Inaonesha una maadili sana mpaka unapata mamlaka ya kuhukumu wanadamu wengine.

Thats cute really!

KUMBE HUYU NDIYO WEWE?
1081876
 
Ni ujinga mwaya ukijiamini ukaondoa inferiority complex utafanikiwa mpka baba ashangae
Kwanza wanaume weng hawapend kuona mwanamke anafanikiwa kabsaa
 
Back
Top Bottom