chamaclotus
JF-Expert Member
- Apr 19, 2019
- 1,079
- 2,273
Habari za mchana ndugu zangu,
Hawa polisi mbona wanatunyanyasa na hawakemewi na serikali. Juzi pale mataa ya ubungo walimkamata jamaa kwa kupaki bajaji sehemu isiyoruhusiwa, kwa kuwa walikuwa wamevaa kiraia jamaa aliwaomba kitambulisho maana walitaka wampeleke kituoni. Cha ajabu polisi mmoja alimkaba jamaa wa bajaji Koo mpaka jamaa akaanza kulia kama mtoto huku polisi wengine wakimshika Tanganyika jeki na kumlazimisha aingie kwenye bajaji waende kituoni, ilikuwa kama vita. Ushauri wangu kwa mamlaka husika Ni kujaribu kutoa elimu kwa hawa polisi namna ya ukamataji raia.