Nina mashaka kidogo kama kweli uchawi ni tawi la sayansi.
Well, naweza kuwa nimekosea kuhusisha uchawi kama sehemu ya sayansi. Pengine labda wachangiaji wengine wanaweza kusaidia kuelea hasa uchawi ni nini.
Je kuna uwezekano wa kumroga mtu asiyeamini ushirikina na mtu huyo akadhurika? Kwa mfano mtoto mchanga.
Kiujumla, siamini kuwa mtu
asiyeendekeza uchawi anaweza kurogeka. Sasa, mtu
asiyeamini uchawi hawezi kuwa anaendekeza uchawi. Kwa hiyo jibu langu ni kama la sentensi ya kwanza.
Kwa mtazamo wangu, imani ya mtoto mchanga inaangukia kwa wazazi wake moja kwa moja. Hivyo basi, kama wazazi wanaendekeza imani za kichawi, basi mtoto anaweza kudhurika.
Lakini kama kweli uchawi upo (mtu anaweza kukuroga ufe ukafa) then huoni pengine watu wanayo sababu ya kuchukua tahadhari. Kwa mfano kama uaamini kuna wizi/ujambazi ni lazima utafunga milango, utaweka walinzi nk. Isnt this automatic?
Tofauti na ujambazi, uchawi unategemea sana 'ushiriki wa imani hiyo.' Kwa hiyo, bado nasisitiza kuwa mtu ambaye hashiriki kwenye imani hizi hawezi dhurika na matendo ya kichawi. Kwa mara nyingine tena, huu ni mtazamo wangu.
Je kuna ushirikina makanisani/misikitini nk?
Ushirikina unahusisha watu. Mashehe na wachungaji ni watu. Sasa kama msikitini na makanisani kuna ushirikina, basi wahusika wa hayo 'majumba' ni washirikina.
Wachungaji wanaokemea mapepo nao ni washirikina? Mtu hawezi kuzaa, wanasema mapepo! Anaumwa malaria wanasema mapepo!
Tricky!
Sidhani kama mapepo yanatokana na uchawi. Katika miongozo ya kidini, mapepo ni aina ya viumbe ambavyo vinauwezo wa kuishi ndani ya mtu. Mapepo wako kwenye kundi la mashetani na majini (kama sio kitu hicho hicho). Uchawi ni imani ambayo inafanya mambo kwa kutumia nguvu za giza. (hapa naweza kuwa nimejichanganya mwenyewe....!!)
Sasa basi, mchungaji anayekemea mapepo si mshirikina. Lakini mchungaji anayeamini kuwa kuna watu walikufa na wakazikwa, halafu ( anaendelea kuamini) kumbe walichukuliwa kichawi na kufanywa misikule, basi huyo ni mshirikina.
Binafsi napata shida kuamini kwamba uchawi upo.
Well, ni imani kama imani nyingine. Wewe huamini kuna uchawi. Kuna watu wengine hawaamini kuna Mungu. Ni imani tu.