Eh WOS! Si unajua wakati mwingine inabidi ku-compare menu ya 'home' na ya 'jirani.' Sasa unakuta maharage ya home yapoyapo tu, yameungwa kwa vitunguu na mafuta basi. Lakini maharage ya kwa jirani yananukia nazi, iliki, na pilipili mbuzi. Sasa hebu niambie, mtoto akipiga ana-ana-do lazima mkono uangukie kwa jirani. LOL
Next time ukialikwa kwenye harusi, nenda na khanga, halafu jaribu kwenda kumvisha bibi harusi (wakati wa kutoa zawadi). Wallahi hautaweza kumfikia bibi harusi. Utaona jinsi utakavyopigwa bonge la stop na 'shangazi-mpenda-shari.' Na ukifanikiwa kumvalisha, hiyo khanga itavulia in a blink of an eye. hautajua hata nani kaivua, kwa jinsi itavyovuliwa haraka.
Kwa nini usijaribu?...halafu uje utupe feedback
Hivi jicho baya nayo ni sehemu ya imani za kishirikina? Na kuna ile ya 'mdomo mbaya' pia.