Nakumbuka nikiwa mtoto, mtaani kwetu kulikuwa na mzee mmoja na mkewe ambaye walisemekana kuwa ni wachawi. Basi sisi watoto (na baadhi ya wakubwa) tulikuwa tunawanazomea kila wakipita. Tulikuwa hatuwaogopi wala kuwatetemekea. Na hakukuwa na mtu yeyote aliyewahi kudhurika na 'mashambulizi' yao (kama yalikuwepo)
Sijaelewa vizuri, wewe ulikiona kitendo cha kuwazomea wazee wa watu ni kitu kizuri au kibaya?
Sijaelewa vizuri, wewe ulikiona kitendo cha kuwazomea wazee wa watu ni kitu kizuri au kibaya?
Sometimes mambo mengine ni kukosa akili tuu.
Wee unaenda kwa mganga eti upandishwe cheo while ndo mtu mvivu na mwenye majungu ofisini.
Ila sometimes hawa waganga aminia kama ile ya kumwona mwizi wako kwenye kioo imetulia na haina tofauti na kamera za bank-big up ila masharti yapungue.
Ntashukuru kama suala la kuruka na ungo litakuwa commercialised hasa ktk ulimwengu huu ambapo mafuta yanasumbua and time is of essense
Washirikina ni wagonjwa....(adui wa tatu)..wana ugonjwa kushindwa kufikiri ( over and above ujinga)
...
Ukiachilia mbali anecdotes za ushirikina ( k.m. kamera za kuonyesha mbaya wako n.k) ni wapi tumeona kwa mfano ushahidi wa jambo zuri lililofanywa na wachawi?
Kama kuna mwenye mifano hai hapa JF atuonyeshe.
1) Siku hizi watoto kula kwa jirani ni mwiko. Kisa? Eti huwezi jua jirani ameweka nini kwenye chakula.
2) Siku hizi ni mwiko kwa mtu yoyote (isipokuwa ndugu wa karibu sana) kumfunga khanga kiunoni bibi harusi. Kisa? Eti kuna hofu kuwa wengine wanakuja na kanga zilizowekwa mambo ya kufunga kizazi.
3) Siku hizi mwanamke akiwa mjamzito, anahakikisha ananunua khanga mpya kabisa, na kuacha kuzivaa zile za zamani. Kisa? Eti kunaweza kuna na khanga zilizofanyiwa mambo kutaka kumdhuru mtoto ingali bado tumboni.
4) Siku hizi wafiwa wanahakikisha kwenye shughuli za uoshaji wa mwili wa marehemu ni lazima kuwe na mtu ambaye kazi yake ni kuhakikisha hakuna mwoshaji yoyote anayenyofoa kiungo cha marehemu. Kisa? Eti watu huwa wanatabia ya kunyofoa viungo vya marehemu na kupeleka wa wanganga wao au hata kwenda kuviuza.
Tukiangalia hizi scenario nne – ni hipi kati ya hizi ambayo wanajamii wanahaki ya kuhofia? Na kwa nini?
1) Siku hizi watoto kula kwa jirani ni mwiko. Kisa? Eti huwezi jua jirani ameweka nini kwenye chakula.
2) Siku hizi ni mwiko kwa mtu yoyote (isipokuwa ndugu wa karibu sana) kumfunga khanga kiunoni bibi harusi. Kisa? Eti kuna hofu kuwa wengine wanakuja na kanga zilizowekwa ‘mambo' ya kufunga kizazi.
3) Siku hizi mwanamke akiwa mjamzito, anahakikisha ananunua khanga mpya kabisa, na kuacha kuzivaa zile za zamani. Kisa? Eti kunaweza kuna na khanga zilizofanyiwa ‘mambo' kutaka kumdhuru mtoto ingali bado tumboni.
4) Siku hizi wafiwa wanahakikisha kwenye shughuli za uoshaji wa mwili wa marehemu ni lazima kuwe na mtu ambaye kazi yake ni kuhakikisha hakuna mwoshaji yoyote anayenyofoa kiungo cha marehemu. Kisa? Eti watu huwa wanatabia ya kunyofoa viungo vya marehemu na kupeleka wa wanganga wao au hata kwenda kuviuza.
Mbu...ebwanaaa eeeh! QM mbona yote yanatisha haya, huenda kuna kaukweli hapa, hata kama mtu huna imani ya ushirikina, unakuta jimama linang'ang'ana kumfunga kanga mamsapu, tena yenye maneno "kufuli langu", hata mimi nitarusha ngumi!
Shukran kwa kunifungua macho, duh!
Woman of Substance sijui ata comment lipi juu ya hayo manne, maana yanawagusa moja kwa moja wanawake...
Kula kwa jirani, kwanini mtoto ukale kwa jirani? kwenu hamna chakula?
Mbu
ukiacha hilo la kwanza la kula kwa jirani ambalo siyo la siku hizi tu bali lilikuwepo tangia zamani, hayo mengine wala sina la kusema maana binafsi sijaskia.
Umesahau pia kuna zongo - jicho baya, yaani mtu anaweza kumwangalia mwanao akapata maradhi! Hili pia sijui asili yake lakini watu wengi hasa wa pwani utawasikia wakizungumzia hiki kitu.
Kuna kupigwa kipapai - sijui ndo kutupiwa majini/mashetani... alimradi utitiri wa imani za kishirikina.Lakini kama nilivyochangia mwanzo - ujinga, umaskini na maradhi ya kushindwa kufikiri na kutumia akili na pia hali ya kukumbatia imani na tamaduni zisizo na maana!
Mimi naomba kuuliza yafuatayo:
1. Je ushirikina/uchawi upo? (i.e. Ni kweli kwa mfano mtu anaweza akoroga ufe na ukafa?). Mwenye experience atupatie.
2. Je ushirikina na uchawi ni kitu kimoja? Mchawi ni nani na Mshirikina ni nani?
Si unaona hata viongozi wetu haweshi kuvaa mapete na macheni ya ajabu-ajabu. Ushirikina mtupu!
3. Mazingaombwe ni tofauti na uchawi/ushirikina?
Mbu
ukiacha hilo la kwanza la kula kwa jirani ambalo siyo la siku hizi tu bali lilikuwepo tangia zamani, hayo mengine wala sina la kusema maana binafsi sijaskia.
Kula kwa jirani, kwanini mtoto ukale kwa jirani? kwenu hamna chakula?
Eh WOS! Si unajua wakati mwingine inabidi ku-compare menu ya 'home' na ya 'jirani.' Sasa unakuta maharage ya home yapoyapo tu, yameungwa kwa vitunguu na mafuta basi. Lakini maharage ya kwa jirani yananukia nazi, iliki, na pilipili mbuzi. Sasa hebu niambie, mtoto akipiga ana-ana-do lazima mkono uangukie kwa jirani. LOL
...ha ha ha... haki ya mungu hata mie chakula cha jirani kilikuwa kinanitoa mate kila siku ...sijui ilikuwa ni utoto? lakini hata wazungu wana msemo "the grass looks greener on the other side!"
...tukirudi kwenye sayansi ya mwafrika; ...na ile ya wale watoto wanaovimba vitumbo halafu unaambiwa "kalambishwa", au "kabemendwa" nayo imekaaje?
Uchawi upo. Uchawi ni tawi la sayansi.
Kuamini uchawi upo na kuendekeza uchawi ni vitu viwili tofauti. Binafsi ninaamini uchawi upo, lakini siuendekezi wala kuogopa. Ninaamini kuwa anayekumbwa na dharuba la kichawi ni lazima na yeye awe anajihusisha na imani hizo kwa njia moja au nyingine. Ninaamini kuwa ukikaa mbali na imani hizi, basi hautadhurika....hata kama ukashindiwe makaburini mwaka mzima.
Nina mashaka kidogo kama kweli uchawi ni tawi la sayansi.
Je kuna uwezekano wa kumroga mtu asiyeamini ushirikina na mtu huyo akadhurika? Kwa mfano mtoto mchanga.
Lakini kama kweli uchawi upo (mtu anaweza kukuroga ufe ukafa) then huoni pengine watu wanayo sababu ya kuchukua tahadhari. Kwa mfano kama uaamini kuna wizi/ujambazi ni lazima utafunga milango, utaweka walinzi nk. Isnt this automatic?
Je kuna ushirikina makanisani/misikitini nk?
Wachungaji wanaokemea mapepo nao ni washirikina? Mtu hawezi kuzaa, wanasema mapepo! Anaumwa malaria wanasema mapepo!
Binafsi napata shida kuamini kwamba uchawi upo.