Hivi kwa nini tunaendekeza sana imani za kishirikina?

 

QM,
Hunitakii mema naona!Kisa cha kuitwa mchawi kwenye harusi za watu?? kisa nije kuwapa ushuhuda hapa JF!
Utanisamehe maana mtihani huo wala sijaribu.
 
...Je Limbwata?

hujawahi kuona mume anafanyiwa kila kisa na mkewe yeye yupo yupo tu?

Nitakupa mfano mwingine; nilipokuwa Boarding school, na wenzangu tulikuwa tunatoroka kwenda uswahilini kula kwa mama ntilie... cha ajabu umati wa watu ulikuwa unang'ang'ania kula kwa kina mama fulani fulani tu, hata kama ni makoko,... wale mama ntilie wengine aaahh... masufuria yao hayaguswi japo wali tele, bei moja, portion sawa, ladha ya wali wa nazi na maharagwe ya nazi bomba...

mpaka leo najiuliza imekaaje ile!
 
hapo kweli umenenea kwasababu hili swala la imani za kishirikina linazidi kushamiriri sana na watu wanashindwa kuamini muumba wao, na hili jambo linazidi kudidimiza watu sana. mimi naona elimu itolewe watu wahamasishe wamuamini mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…