Hivi kwa umri wa miaka 41 niliofikisha naweza kutoboa maisha au ndio basi tena?

Hivi kwa umri wa miaka 41 niliofikisha naweza kutoboa maisha au ndio basi tena?

Wana JF hivi kuna uwezekano wa kufanikiwa kiuchumi unapokuwa na umri wa kuanzia 41?

Mpaka sasa nina mke na watoto watatu. Sina shughuli rasmi, nabangaiza tu.

Naanza kuona kama ndoto yangu ya kuwa na mafanikio kiuchumi inafifia.

Swali langu ni kwenu ninyi Wana JF. Hivi kuna possibility ya kutoboa kwa umri huo? Au ndio nishazeeka Tena!

tatizo lako humuamini mungu unaamini kitoboa ni umri
 
Vijana jitahidini msizae watoto wengi kabla hamjatoboa, mtapata tabu sana. Kama unapenda sana watoto na mambo bado hayajakaa vizuri jitihadi usizidishe wawili.
Ni ukweli kabisa, chukulia mtu bado huna chanzo cha kipato cha uhakika, muda huo tayari una watoto wanne, basi upo uwezekano mkubwa wa kubaki kwenye cycle ileile ya chini.

Simply because children at their childhood are liabilities, but if you parent them well they will become assets as you grow older, but how can you parent them well while you are still in economic hardship
 
Wakati wa Mungu hauna kikomo, Hata hii leo unapouliza swali hili huenda usimalize hata mwezi ukafikia mafanikio usiyoyatarajia.
Kikubwa shukuru tu kwa hicho ulichojaaliwa. Huenda ungepewa kikubwa kabla ya leo tungekuwa tushakusahau tayari.
 
Aisee maswali gani hayo mango? Life begins at 40...ndo kwanza ngoma imeanza. Kikubwa uwe na mipango
 
Back
Top Bottom