Hivi kwani Mungu anajibu maombi mabaya?

Hivi kwani Mungu anajibu maombi mabaya?

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,749
Reaction score
62,766
Wakuu habari za kuamka....

Mwenzenu najiskia vibaya sana sana sana yaani vibaya mnooo.. Natamani hata nisingekua nimeshika simu leo,. Kuna mtu kaweka status "Forever in our hearts" kampost mtu ambaye alifariki 2012 hadi nilishamsahau,. Nilikua mtoto lakini huyu mtu kila siku nilikua namuombea kwa Mungu afe,.

Ilikua hivi,. Nakumbuka Kabla ya likizo ya pasaka nlikua darasa la nne by then.. Tulikua tunafanya mitihani ya Joint shule nyingi nyingi na wale wanaokuwa topten mnaitwa mnapewa zawadi mnashangiliwa na kombe mnapewa kurudi nalo shuleni

Hiyo siku na mimi nilipass nikawa nominated kati ya ambao wataenda kuchukua zawadi,. Mda tunajiandaa tukaanza kujisafisha yaani kama kufuta viatu, kujiweka tu vizuri, nikatafuta lesso yangu nifutie viatu sikuiona.. Huyu binti ambae ni marehemu Alitoa lesso watu wote wakawa wamefutia viatu mimi nlikua wa mwisho ikafika zamu yangu huku najifuta nikaangalia vizuri nikaijua ni lesso yangu ambayo nlikua naitafuta, nikamwambia hii mbona lesso yangu nlikua naitafuta umeipata wapi? Si akakasirika akaninyang' anya nikamwambia basi nikupa iwe yako niachie tu nimalizie kufutia maana ndio nlikua nimeitwa niende mbele Akagoma .

Imagine nimeenda Mbele yatu wengi wanafunzi wa karibia shule 10 na walimu ,kiatu kimoja kisafi kingine kina Vumbi halafu yeye na rafiki zake walikua wananicheka 😭😭😭,. Ile siku hata sikuifurahia nilivyotoka tu nikapiga picha (na kiatu changu kimoja kina vumbi mwenyewe) nikarudi zangu nyumbani hata sikuongea na mtu...

To be honest tangu sikuile nilikua namchukia , mda wa kusali sala za jioni au asubuhi au kanisani nlikua namwambia Mungu kwanini watu wenye Roho mbaya unawaacha waishi,. Nlikua namwomba Mungu kila siku yule binti afe,. nilikua simpendi yaani kila siku nlikua namwambia Mungu huyu mtu asipokufa mimi nitaacha kusali maana ni anaroho mbaya kwanini asife tu?

Wakati tunakaribia kufunga shule December alianzaga kuumwa akawa na vidonda vidonda,nywele zake zilikua zinayonyoka Alikua anababuka midomo, Mara shuleni haji,. kwa wiki anaweza aje siku moja na akifika basi kuna mda anaanza kuumwa mara anatapika mzazi wake anakuja kumchukua, tulikua tunaambiwa Fulani anaumwa mkipata nafasi mkamwone me sikwenda hata siku moja, Kwanza nlikua nafurahi rohoni namwambia Mungu saizi ndio muda wake huu wa kufa, Wakati tupo darasa la tano alifariki nikawa najiskia amani kwanza hadi nilishamsahau... Tulikujaga tu kujua baadae kumbe alikua ni HIV POSITIVE tangu alivyozaliwa,.

Hapa nimekaa najiskia tu huzuni maybe hatakama alikua HIV positive pangine angeishi mda mrefu ila maombi yangu yalikuwa yanapigilia misumari mpaka akafa mwee!!,. Nimetoka kumwambia Mungu kama maombi yangu yalihusika anisamehe maana sikua najua nafanya nini kwa kipindi kile ni utoto tu😒🙏🙏

Ila sidhani kama maombi mabaya huwa yanaskilizwa🤔🤔
 
FB_IMG_1748852351669.jpg
 
Hakuna kinachojibiwa na mungu, ni illusion tu na myths. Kifo ni natural event, uombe usiombe kifo kipo pale pale. Miaka 90 ijayo asilimia 99.9 ya watakao soma maoni haya leo, hawatokuwepo tena kwenye uso wa ulimwengu.

Siku uliyo zaliwa ndio siku uliyoanza kufa.
 
Maisha yana siri kubwa sana hasa unapotamka kitu kwa uchungu... Kuna jamaangu nilizozana nae kipindi fulani nilifilisika nikamuuzia friji akanizulumu chenchi kidogo tu kwenye ile hela aliyotakiwa kunipa, sasa kwa hali ngumu niliyokua nayo nikajikuta nimemtamkia maneno fulani kwa uchungu kitu ambacho naona kimetokea kama nilivyomwambia.

Friji niliuza ili niweze kumhudumia mke wangu aliyeenda kujifungua.
Yule jamaa nae alikuja kufilisika na kanasa kwenye mtego kama wangu hadi namkwepa asije kusema mimi mchawi
 
Wakuu habari za kuamka....

Mwenzenu najiskia vibaya sana sana sana yaani vibaya mnooo.. Natamani hata nisingekua nimeshika simu leo,. Kuna mtu kaweka status "Forever in our hearts" kampost mtu ambaye alifariki 2012 hadi nilishamsahau,. Nilikua mtoto lakini huyu mtu kila siku nilikua namuombea kwa Mungu afe,.

Ilikua hivi,. Nakumbuka 2011 Kabla ya likizo ya pasaka nlikua darasa la nne by then.. Tulikua tunafanya mitihani ya Joint shule nyingi nyingi na wale wanaokuwa topten mnaitwa mnapewa zawadi mnashangiliwa na kombe mnapewa kurudi nalo shuleni,.
Hiyo siku na mimi nilipass nikawa nominated kati ya ambao wataenda kuchukua zawadi,. Mda tunajiandaa tukaanza kujisafisha yaani kama kufuta viatu, kujiweka tu vizuri, nikatafuta lesso yangu nifutie viatu sikuiona.. Huyu binti ambae ni marehemu Alitoa lesso watu wote wakawa wamefutia viatu mimi nlikua wa mwisho ikafika zamu yangu huku najifuta nikaangalia vizuri nikaijua ni lesso yangu ambayo nlikua naitafuta, nikamwambia hii mbona lesso yangu nlikua naitafuta umeipata wapi?? Si akakasirika akaninyang' anya nikamwambia basi nikupa iwe yako niachie tu nimalizie kufutia maana ndio nlikua nimeitwa niende mbele Akagoma . Imagine nimeenda Mbele yatu wengi wanafunzi wa karibia shule 10 na walimu ,kiatu kimoja kisafi kingine kina Vumbi halafu yeye na rafiki zake walikua wananicheka 😭😭😭,. Ile siku hata sikuifurahia nilivyotoka tu nikapiga picha (na kiatu changu kimoja kina vumbi mwenyewe) nikarudi zangu nyumbani hata sikuongea na mtu...

To be honest tangu sikuile nilikua namchukia , mda wa kusali sala za jioni au asubuhi au kanisani nlikua namwambia Mungu kwanini watu wenye Roho mbaya unawaacha waishi,. Nlikua namwomba Mungu kila siku yule binti afe,. nilikua simpendi yaani kila siku nlikua namwambia Mungu huyu mtu asipokufa mimi nitaacha kusali maana ni anaroho mbaya kwanini asife tu??..

Wakati tunakaribia kufunga shule December alianzaga kuumwa akawa na vidonda vidonda,nywele zake zilikua zinayonyoka Alikua anababuka midomo,. Mara shuleni haji,. kwa wiki anaweza aje siku moja na akifika basi kuna mda anaanza kuumwa mara anatapika mzazi wake anakuja kumchukua.. tulikua tunaambiwa Fulani anaumwa mkipata nafasi mkamwone me sikwenda hata siku moja, Kwanza nlikua nafurahi rohoni namwambia Mungu saizi ndio mda wake huu wa kufa,. 2012 wakati tupo darasa la tano alifariki nikawa najiskia amani kwanza hadi nilishamsahau... Tulikujaga tu kujua baadae kumbe alikua ni HIV POSITIVE tangu alivyozaliwa,.


Hapa nimekaa najiskia tu huzuni maybe hatakama alikua HIV positive pangine angeishi mda mrefu ila maombi yangu yalikuwa yanapigilia misumari mpaka akafa mwee!!,. Nimetoka kumwambia Mungu kama maombi yangu yalihusika anisamehe maana sikua najua nafanya nini kwa kipindi kile ni utoto tu😒🙏🙏

Ila sidhani kama maombi mabaya huwa yanaskilizwa🤔🤔
20250428_105233.jpg

Relax.
Mungu hawezi kujibu maombi yaliyo kinyume na maelekezo yake. Mungu ni pendo. Ametuagiza tuwaombee hata wanaotuudhi. Na anatuambia kuwa si kazi yetu sisi kulipa kisasi kwa anayetukosea. Kazi ya kulipa kiasi kwa ajili yetu ni kazi ya Mungu mwenyewe. Yeye ndiye anajua atakulipia kiasasi kwa njia gani na kwa wakati gani?

Mathayo 5:44
Lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,

But I say unto you, Love your enemies, bless them that curse you, do good to them that hate you, and pray for them which despitefully use you, and persecute you;

Warumi 12:19
Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
Dearly beloved, avenge not yourselves, but rather give place unto wrath: for it is written, Vengeance is mine; I will repay, saith the Lord.
 
Kama una amini kuwa Mungu aliumba Dunia kwa kutamka tu na ikawa,hata wewe unaweza kutamka ikawa kwakuwa tumeumbwa kwa mfano wa Mungu,unachokuwa unakisema kinadakwa kwenye ulimwengu wa roho,hapa ni either evil or holy,then kile kitu kinafanyika as you wish...
 
Sijasoma post yote nimeishia hapo uliposema ulimuombea mtu afe.

Huwezi kumuombea mtu afe na akafa,ingekuwa hivyo hata wewe ungeshakufa maana siyo wote unaoona wanakuchekea wanakupenda au wanakutakia heri,tunakufa kwa sababu tunakuwa tumeshamaliza yaliyotuleta duniani.
 
Wakuu habari za kuamka....

Mwenzenu najiskia vibaya sana sana sana yaani vibaya mnooo.. Natamani hata nisingekua nimeshika simu leo,. Kuna mtu kaweka status "Forever in our hearts" kampost mtu ambaye alifariki 2012 hadi nilishamsahau,. Nilikua mtoto lakini huyu mtu kila siku nilikua namuombea kwa Mungu afe,.

Ilikua hivi,. Nakumbuka 2011 Kabla ya likizo ya pasaka nlikua darasa la nne by then.. Tulikua tunafanya mitihani ya Joint shule nyingi nyingi na wale wanaokuwa topten mnaitwa mnapewa zawadi mnashangiliwa na kombe mnapewa kurudi nalo shuleni,.
Hiyo siku na mimi nilipass nikawa nominated kati ya ambao wataenda kuchukua zawadi,. Mda tunajiandaa tukaanza kujisafisha yaani kama kufuta viatu, kujiweka tu vizuri, nikatafuta lesso yangu nifutie viatu sikuiona.. Huyu binti ambae ni marehemu Alitoa lesso watu wote wakawa wamefutia viatu mimi nlikua wa mwisho ikafika zamu yangu huku najifuta nikaangalia vizuri nikaijua ni lesso yangu ambayo nlikua naitafuta, nikamwambia hii mbona lesso yangu nlikua naitafuta umeipata wapi?? Si akakasirika akaninyang' anya nikamwambia basi nikupa iwe yako niachie tu nimalizie kufutia maana ndio nlikua nimeitwa niende mbele Akagoma . Imagine nimeenda Mbele yatu wengi wanafunzi wa karibia shule 10 na walimu ,kiatu kimoja kisafi kingine kina Vumbi halafu yeye na rafiki zake walikua wananicheka 😭😭😭,. Ile siku hata sikuifurahia nilivyotoka tu nikapiga picha (na kiatu changu kimoja kina vumbi mwenyewe) nikarudi zangu nyumbani hata sikuongea na mtu...

To be honest tangu sikuile nilikua namchukia , mda wa kusali sala za jioni au asubuhi au kanisani nlikua namwambia Mungu kwanini watu wenye Roho mbaya unawaacha waishi,. Nlikua namwomba Mungu kila siku yule binti afe,. nilikua simpendi yaani kila siku nlikua namwambia Mungu huyu mtu asipokufa mimi nitaacha kusali maana ni anaroho mbaya kwanini asife tu??..

Wakati tunakaribia kufunga shule December alianzaga kuumwa akawa na vidonda vidonda,nywele zake zilikua zinayonyoka Alikua anababuka midomo,. Mara shuleni haji,. kwa wiki anaweza aje siku moja na akifika basi kuna mda anaanza kuumwa mara anatapika mzazi wake anakuja kumchukua.. tulikua tunaambiwa Fulani anaumwa mkipata nafasi mkamwone me sikwenda hata siku moja, Kwanza nlikua nafurahi rohoni namwambia Mungu saizi ndio mda wake huu wa kufa,. 2012 wakati tupo darasa la tano alifariki nikawa najiskia amani kwanza hadi nilishamsahau... Tulikujaga tu kujua baadae kumbe alikua ni HIV POSITIVE tangu alivyozaliwa,.


Hapa nimekaa najiskia tu huzuni maybe hatakama alikua HIV positive pangine angeishi mda mrefu ila maombi yangu yalikuwa yanapigilia misumari mpaka akafa mwee!!,. Nimetoka kumwambia Mungu kama maombi yangu yalihusika anisamehe maana sikua najua nafanya nini kwa kipindi kile ni utoto tu😒🙏🙏

Ila sidhani kama maombi mabaya huwa yanaskilizwa🤔🤔
Dah!...haya maombi ya aina hii yaelekeze kwa wale 'watekaji' Ili raia wapumue.
 
Back
Top Bottom