Hivi kwani ni lazima kila nyumba inayotazama barabara, iwe na fremu ya duka?

Hivi kwani ni lazima kila nyumba inayotazama barabara, iwe na fremu ya duka?

Ila uzuri wakitoka madarakani wanakumbana na uhalisia kama biashara uliizoesha kukua kwa pesa za ufisadi na rushwa siku zikikata unabaki na majengo tu, na wengi imewakuta hii.
Wana Mali nyingi sana
 
Mpaka kanisa katoliki kwa sasa linajenga fremu ujue nyumbani kumenoga!!
 
Wewe mwenye maono na akili si ufungue hivyo viwanda ujikite kwenye huo uzalishaji? Wenzio wameona fursa kwenye fremu na uchuuzi badala ya kupiga kelele funguo wewe hicho kiwanda uwauzie bidhaa hao wachuuzi waache kwenda China.
Ni kawaida wazalishaji kuwa wachache na wachuuzi kuwa wengi,wewe kuwa mmoja kati ya hao wachache badala ya kuponda na kulalamikia njia za watu kujiingizia kipato.
 
Nimepita Songea mjini siku za karibuni Aisee nyumba zote zimegeuzwa fremu za biashara,hadi kituo kikuu cha police kumejengwa fremu za biashara kuzunguka eneo lote la kituo
 
Ni kama fasheni Tu, Mimi nikiwa na weka fensi Wife alinipigia simu Mume wangu usisahau kuniwekea fremu hapo. Nikamwambia Nyumba yangu sitaki kujenga kama uswazi hapa hakuna potential ya biashara. Akasema we niwekee Tu Mimi hivyo hivyo😂😂
Kwa kuwa Mke wangu Nampenda na kuweka mlangoni frem kwenye fensi ninayojenga hainichukuia gharama nikamwekea. Huu ni mwaka wa 6 hajaweka chochote
Wanawake wana nguvu sana
 
Tumekuwa taifa la wachuuzi na watu waliokosa ubunifu

Tunaona nyumba nyingi zinazojengwa pembezoni mwa barabara zikibuniwa na fremu za maduka, hata kama wenye nyumba hawana mpango wa kufanya biashara.

Je, hii ni kutokana na mahitaji ya biashara, kuongeza thamani ya nyumba, au ni mtindo tu wa ujenzi unaoendelea kuzoeleka?
Moja ya tatizo kubwa la watanzania ni kutokuwa na idea za biashara na badala yake tunapenda kuwaiga wenzetu walioanzisha kitu na kupunguziana riski tu. Kila mtu anajenga fremu za duka kwa sababu tu wengine wamejenga fremu na anaon nae atapata visenti. Hawaji na idea zao. Hivi leo hapo unapoishi wewe anzisha tu kuuza mlangoni kwako kashata na kahawa, kesho yake majirani wako kumi nao wataanza kufanya biashara hiyo hiyo.
 
Tanzania wauzaji ni wengi kuliko wanunuzi
 
Back
Top Bottom