Uchaguzi 2020 Hivi kwanini baadhi ya watu wanataka Aidah Khenan wa CHADEMA ajiuzulu Ubunge alioshinda?

Uchaguzi 2020 Hivi kwanini baadhi ya watu wanataka Aidah Khenan wa CHADEMA ajiuzulu Ubunge alioshinda?

Hivi unawezaje kuweka chama mbele dhidi ya wananchi wako!?

Kosa lenu CHADEMA ndio hilo na adhabu yake tumewapa kwenye uchaguzi huu.

Mmekuwa na kawaida ya kuheshimu chama kuliko wapiga kura wenu....Sasa safari hii sisi Watanzania tumewapa dozi ambayo imewazika kabisaaaa. Hatutaki wahuni kwenye Bunge letu!

Kaeni kwenye lichama lenu na muendelee kumtukuza yule mzee wa Faru Joni tuonane mtafika wapi kisiasa.

Huyo dada kwa hekima anapaswa kuheshimu wapiga kura wake kisha ndio chama kinafuata. Wapiga kura ndio kila kitu kwenye siasa. CCM wanalijua hilo CLEARLY.
Hiyo ni katiba mkuu sio CHADEMA. Na ndio maana kina Mnyika walipigania wagombea binafsi ili hta mbunge akivuliwa uanachama aendelee kuwa mbunge na hta akikosa chama bado ana fursa ya kugombea ubunge.

CCM walikataa wagombea binafsi maana waliogopa watu wakikatwa watagombea na kugawa kura.

Sasa unapolaumu CHADEMA nakushangaa sana pengine hufuatilii siasa wala katiba.

NB: Wapiga kura hawakudhamini ila chama kina kudhamini sasa yye akiwasikiliza wananchi alafu akavuliwa ubunge na Mbowe ndio utaelewa nani ni nani kwenye kumuweka bungeni.
 
Unamaanisha auache mshahara wa kibunge utamapa ugali wewe kiazi kweli[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kama katumwa na wananchi bhas ajiuzulu maana atawakosesha hao wananchi maendeleo in Meko's voice

Afanye fair play kwa chama na kwa wananchi
 
Hajatumwa na wenzake Diba ametumwa na wananchi. Akijiuzulu atakua amevunja mkataba na hatawatendea haki aliowaahidi kuwatumikia miaka5
Wananchi Kama anawapenda ajiuzulu maana hakuna maendeleo kwa wananchi wenye mbunge wa upinzani in Meko's voice

ajiuzulu tu hawaachie watu wapate maendeleo aisiwe kizuizi Cha maendeleo
 
Sheria ya kupata viti maalum unaijua? Lengo ilikuwa kuwe na ccm tu. Wamefanikiwa kelele za nn? Chadema watafute biashara nyingine maisha yasonge. Siyo lazima cdm wawepo bungeni. Narudia siyo lazima. Ccm wanatosha peke yao
Sheria ya viti maalum ikoje ?Tokea jana natamani kufahamu. Ikute CCM walifanya mahesabu ili Lissu apate kura ambazo chama chake hakitaweza kupata wabunge viti maalum.
 
Hata akimfuta, Spika na Tume ya Uchaguzi watakataa kutambua kuwa amefutwa. Kama amewekwa kama boya, hamna namna watakubali akose ubunge.

Amandla...
Mm nazani hii itakua nzuri kwake

Mbowe afanye Kama anamfuta ili Spika tulia akatae barua, Aidan aendelee kula mema ya wabunge. Bila kujulikana analia kutokea chama gani.

Lakin tayar chadema washajivua lawama/dhambi yakushiriki vikao vya CCM (vya ndio mzee).

Pia kizingizio Cha serikali etii wameshindwa kuleta maendeleo sababu ya upinzani vikosekane

Sina Shaka na wabunge wa kafu maana kitandan akizai haramu
 
Sheria ya viti maalum ikoje ?Tokea jana natamani kufahamu. Ikute CCM walifanya mahesabu ili Lissu apate kura ambazo chama chake hakitaweza kupata wabunge viti maalum.
Inataka uwe na at least 5% ya kura za wabunge.
 
Kasema mwenyewe kuwa hataki kwenda bungeni na hadi sasa viongozi wake hawajasema lolote. Kumbuka huyu alikuwa mbunge wa viti maalum chadema bunge lililopita. Anajua anachokisimamia. Hawezi kwenda bungeni ili ccm wapate mtu wa kumdhihaki
Mkuu umepata update baada ya kikao cha chama leo?
 
Mbunge anadhaminiwa na chama sio wananchi. Hta bungeni mnakaa kwa mfumo wa kichama, same to kamati. Na ndio maana Leo Mbowe akimfuta uanachama huyo dada ndio ubunge wake unafia hapi hapo.
Sio kwa spika wetu mwaminifu Ndungai huyo Dada akiamua kuwa mbunge atakaa bungeni kama walivyokaa kina Mwambe,silinde .Wananchi awawezi kukosa uwakilishi kisa wahuni wachache wamekaa kujadiliana kumfutia uanachama mbunge
 
Mi nawaza tuu hivi akiamua kijiuhudhuru, au sijuh kufanya maamuzi gani ni Sawa ila swali

Atakuwa ame watendea Haki watu wake walio kubali kupanga folen kuchagua yeye???

Yeye awaze kuusu chama chake Je walio piga kula ni watu WA chama chake tuuu???

Kumbuka watu wame mwamin ndio maana wame fanya maamuhayo kwake Sasa akiamua kuwa tupa huo ndio ushenz utakao fanya watu wasije kuthubutu Tena kufanya maamuzi kama hayo kwakuwa wanajua tukimchagua wenziwe wakikosa ataujiudhuru
Anatakiwa asimamie idhini ya wananchi na siyo wivu wa viongozi wenzake wa chama.
 
Haileweki mpaka sasa kwa nini CCM wameamua kutoiba kura huko Nkasi.
Hilo ni jambo lingine na tayari matokeo tunayo kua Bi Aidah ni mshinde, ni halali kama chama kukomaa mama wa watu asiende bungeni wakati ticket kaipatia kwenye kura?
 
Sio kwa spika wetu mwaminifu Ndungai huyo Dada akiamua kuwa mbunge atakaa bungeni kama walivyokaa kina Mwambe,silinde .Wananchi awawezi kukosa uwakilishi kisa wahuni wachache wamekaa kujadiliana kumfutia uanachama mbunge
Uzuri umesema maamuzi ya Ndugai kma Ndugai ila kma ni sheria tu, hiyo kitu hairuhusiwi.
 
Hivi unawezaje kuweka chama mbele dhidi ya wananchi wako!?

Kosa lenu CHADEMA ndio hilo na adhabu yake tumewapa kwenye uchaguzi huu.

Mmekuwa na kawaida ya kuheshimu chama kuliko wapiga kura wenu....Sasa safari hii sisi Watanzania tumewapa dozi ambayo imewazika kabisaaaa. Hatutaki wahuni kwenye Bunge letu!

Kaeni kwenye lichama lenu na muendelee kumtukuza yule mzee wa Faru Joni tuonane mtafika wapi kisiasa.

Huyo dada kwa hekima anapaswa kuheshimu wapiga kura wake kisha ndio chama kinafuata. Wapiga kura ndio kila kitu kwenye siasa. CCM wanalijua hilo CLEARLY.
Kasema ataungana na wenzake sasa ww toa povu hapa,mnajali nn Kama mkiwa peke yenu bungeni mlete maendeleo mliyosema
 
Back
Top Bottom