Hivi kwanini chumvi huwa haipandi bei

Ushawahi kuona/kusikia mtoto kalamba chumvi Mkuu Zero IQ?
 
Comments za mabaharia ndo zimenileta hapa, eti kuzama chumvini 10k.... salute kwa Uvinza FC. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Mimi nadhani sababu ni pamoja na gharama za kutengeneza chumvi siyo kubwa, pia kuna maeneo mengine hawanunui kabisa chumvi wanachota tu mtoni kama singida huko, pia kiwango cha matumizi ya chumvi ni kidogo kulinganisha na sukari na hata mafuta, mfano sufuria ya kilo mbili ukipikia chai utahitaji sukari vijiko vikubwa mathalan 5, lakini sufuria hiyo hiyo ukipikia chakula unaweza usimalize chumvi kijiko kimoja, hayo ni mawazo yangu.
 
Jibu rahisi sana. Mosi, uzalishaji wa chumvi hauna gharama kubwa ukilinganisha na sukari. Pili, chumvi hutumika kwa uchache. Mboga ya watu 5 huweza kuwekwa chumvi nusu kijiko wakati sukari kila mtu hujijazia kwa kikombe yake. Aidha, sukari hutumika kwa vyakula vingi zaidi kuliko chumvi na hivyo kuongeza uhitaji.
 
Mi nadhani uzalishaji wake ni mkubwa kuliko hata mahitaji na hii inatokana na sehemu nyingi kuzalisha chumvi ya kutosha,ni sawa na PEMBA wanazokula wanawake miaka yote hazipandi bei kwa kuwa uzalishaji ni mkubwa kuliko mahitaji

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Chumvi this year January ilipanda kiasi na ilikuwa haipatikani wingi.

Siku moja nilikuwa nahitaji mifuko mitatu nilisumbuka sana kuipata nilikuwa nakutana na chumvi ya kwenye packet tu.

Toka kipindi hicho mfuko wa chumvi ulipanda kutoka 6500 mpaka 8000.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Watu wanaosema gharama za kuzalisha chumvi ni ndogo hawajafika kiwandani, Kuna kiwanda kimojawapo hapa Tz kuna jamaa angu nilikuwa namdodosa yeye alikuwa mtumishi pale, Walikuwa wanatumia tani 10+ za kuni daily hadi pale serikali ilipo wapiga stop.

So njia nyingine ni ya kutegemea Jua kiangazi ni gharama kwa sababu uzalishaji ni muda mchache wakati order walizo nazo ni kubwa na Targets wanazojiwekea hawazifikii.
 
Chumvi ina matumizi mengi na hivyo hata demand yake ni kubwa. Kwa sababu ya kuwa na demand kubwa, tungerajia pia bei yake kupanda mara kwa mara, lakini jambo linalofanya chumvi kuwa na bei ya kwaida au bei yake kutopanda licha ya kuwa inahitajika sana na matumizi yake ni mengi ni upatikanaji wake.

Chumvi hupatikana kwa urahisi na ipo katika maeneo mengi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nikiwa gheto nikinunua packet 3 za chumvi za 1500 natumia almost mwaka mzima.. lakini sukari sasa.

Nadhani demand ni ndogo pia uzalishaji wake ni sio ghali sana + ipo ya kutosha.
 
Nadhani ni kwa kuwa tu serikali haijaweka mkono wake,siku serikali ikisema chumvi ishuke bei utashangaa bei yake itakavyolipuka,hata sukari ilitulia kwenye bei yake kwa muda mrefu sana,ila mzee alipotia mdomo tu kwanza wauzaji wakaificha,ikaadimika,ikawa bidhaa adimu hence bei ika sky rocket,hata chumvi ikiadimika pia itakuwa bidhaa adimu,kisha itakuwa bidhaa ghali, suala la gharama za uzalishaji si kwa bidhaa zote,mfano mbolea ya minjingu uzalishaji wake ni rahisi kuliko chumvi,ila inauzwa bei ghali kuliko cement,mbolea ya minjingu ni unaichota,unaichekecha,kisha unajaza kwenye mifuko tayari kwa matumizi,ila ni ghali.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
mkuu Zero IQ mambo ya kuchakata mbunye umeishia wapi ??? maana siku hizi umeokoka na mada zako ni za GT

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…